Kwanini kuna pingamizi kubwa la kuchapisha noti mpya?

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,631
40,786
Nguvu kubwa sana inatumika kufisha uvumi wa uwepo wa zoezi la uchapishaji wa noti mpya.

Sijui ni kwanini nguvu kubwa sana inatumika kupambana na uvumi tu.

Taratibu za kufanyika kwa zoezi hilo zinafamika, kama kweli lipo.

Kumekuwa na uvumi kuwa baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakificha fedha zao nje ya nchi, na wengine kuhamishia huko nje na kuoperate biashara zao toka nje.

Naona hapa kuna vumi mbili zinakinzana, kwa wanaokataa fedha mpya zichapishwe na kututosha kuwa tunakwenda kuwa Zimbabwe ya Pili, na wale wanaosema kuwa kuna fedha zimefichwa na wafanyabiashara wakubwa.

Je, wanaokataa uchapishwaji wa fedha ni mpya ni wale waliozificha huko nje?? au kama hawajazificha ni sababu ipi kuu, inafanya nguvu kubwa sana itumike kufisha huo uvumi, maana bado ni uvumi tu. Wala sidhani kama ni kweli kuna noti mpya zinachapishwa.
 
Dawa ya kenge ni mpaka atoke damu ndio anasikia, wait. Kwanza una ruhusa ya kuzungumzia hayo mambo?
 
Kama B.O.T imekana kuwa haitachapisha noti mpya, maana yake nguvu inayotumika kuzima uvumi huo inatoka kwenye majengo yale mawili pacha pale Posta.

Na maana yake ni kuwa hazina inatumia nguvu kubwa kuzima uvumi, tafisi yake ni JIWE kaamua kuzima jambo hili kwa nguvu na sio wafanya biashara
 
Halafu wee mleta mada sitaki uchokozi wako ujue!!!
Unataka hizi hela nilizofukia chini ziende wapi?:oops::oops::rolleyes::rolleyes:
 
Unafikiri mtu akificha hela nje anafisha Tanzania shilingi?
Ulishajiuliza kwanini watu wana wasiwasi mpaka kuwe na uamuzi wa kuficha hela?
Ulishajiuliza kwa nini watu wanaendeshea biashara zao nje ya Tanzania?
 
Kuchapisha noti mpya kwa nia ya kuongeza mzunguko wa pesa ndani ya nchi ni kosa kubwa sana la kiuchumi na hakuna mtaalam atashauri jambo hilo kwa sababu ni kuficha kovu la usoni kwa kupaka make up! Kama nia ni ku replace note zilizo kwenye mzunguko kwasababu labda zinafojiwa kirahisi, fedha bandia zimezidi kwenye mzunguko, au noti zilizopo sio stahilivu hivyo kuchakaa kwa haraka, hilo ni jambo ambalo linakubalika
 
Nguvu kubwa sana inatumika kufisha uvumi wa uwepo wa zoezi la uchapishaji wa noti mpya.

Sijui ni kwanini nguvu kubwa sana inatumika kupambana na uvumi tu.

Taratibu za kufanyika kwa zoezi hilo zinafamika, kama kweli lipo.

Kumekuwa na uvumi kuwa baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakificha fedha zao nje ya nchi, na wengine kuhamishia huko nje na kuoperate biashara zao toka nje.

Naona hapa kuna vumi mbili zinakinzana, kwa wanaokataa fedha mpya zichapishwe na kututosha kuwa tunakwenda kuwa Zimbabwe ya Pili, na wale wanaosema kuwa kuna fedha zimefichwa na wafanyabiashara wakubwa.

Je, wanaokataa uchapishwaji wa fedha ni mpya ni wale waliozificha huko nje?? au kama hawajazificha ni sababu ipi kuu, inafanya nguvu kubwa sana itumike kufisha huo uvumi, maana bado ni uvumi tu. Wala sidhani kama ni kweli kuna noti mpya zinachapishwa.
Mkuu, mtu akificha hela nje anaweka in terms of shilingi au dola?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom