Kwanini kuna kila sababu ya serikali kulaumiwa juu ya utekaji na kupotea kwa raia?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Kumekua na watu wakitokwa na mapovu kujaribu kutetea uovu unaoendelea juu ya kutekwa na kupotea kwa raia wasiokua na hatia, hili jambo liko wazi na hatuwezi kuacha kuilaumu serikali kwa namna yeyote ile iwavyo.Wanaojaribu kupotosha watu wapitie haya kwa makini.


1.Wanaokamatwa na kutoweka ni wakoasoaji na walio kinyume na misimamo ya serikali yetu, na ndio wenye misimamo tofauti na watawala ambapo pia wanajitoa kuyasema ambayo wengine wanaogopa kuyatamka.

2.Kama zimekua zikifanyika jitihada mbali mbali kupitia vyombo vyetu vya usalama kwa kutumika teknolojia kuwafuatilia na kuwakamata wahalifu wa kimitandao,ikumbukwe tu alipotoweka ndugu Ben Saanane mwanzo kabisa ilionekana kua ukurasa wake wa Fb ulikua ukitumika kiashiria cha kwamba simu yake kuna wakati ilikua ikitumika,Juzi tu baada ya kutekwa msanii Roma simu yake pia ilikua ikiita bila kupokelewa,tuseme nini zaidizi ya hapo?vyombo vyetu vimeshindwaje kujua walipo raria hawa kupitia simu na teknolojia wanaoyoitumia kukamata wahalifu?

3.Juzi wakati anatishiwa maisha kwa bastola ndugu Nape Nnauye, waliomtisha waliambatana na wanausalama wengine wa serikali na baadae Waziri Mwigulu akatoa tamko kua aliyemtishia Mh Nape bastola hakua polisi, Je, alikua ni nani na yuko wapi? Kwanini asiwe miongini mwa watesi wanaolalamikiwa hivi sasa? Sura yake inajulikana na sura ikishajulikana na jina lazima lifahamike, tatizo nini hapa kutomkamata?

4.Katika tukio la kuvamiwa kwa studio za vituo vya luninga na redio Clouds,kwanini tusiamini kua hawa hawa ndio waliovamia studio alipokua msanii ROMA na wakamkamata na kisha kutoweka naye? Kwani hawajulikani?Tutaaminije kua kule Clouds hawakua na lengo la kukamata na kumpoteza mtu lakini hawakumkuta waliomtarajia?Kwani si waliongozwa na kiongozi mkubwa tu wa serikali ya sasa?

5.Kuna kipindi nilimsikia Mh Tundu LISSU akisema kua kuna shimo ambalo wamekua wakiteswa wakosoaji wa serikali, Je, ni kina nani wanaoteswa kule? Wanaotesa watu ni hawahawa wanaolipwa kwa kodi zetu au ni akina nani hasa?


6.Msanii Nay wa Mitego alikamatwa na polisi,kila mtu alijua kua yuko kwenye mikono ya polisi,mlitegemea apotezwe waziwazi hivyo? Kwa Nay wa Mitego hakukua na namna zaidi ya Mahabusu na mahakamani.
 
1.Wanaokamatwa na kutoweka ni wakoasoaji na walio kinyume na misimamo ya serikali yetu, na ndio wenye misimamo tofauti na watawala
Okay.

Roma yuko kinyume na msimamo gani wa watawala?
 
Inawezekana ndio mara yako ya kwanza kusikia jina la ROMA.

Ambayo ubaya wake ni nini kama sijasikia jina la Roma?

Unadhani kila mtu kwenye jamii ni show business junkie anaefuatilia wasanii wote wa kizazi kipya?

Hata hao watawala wenu mnaowashuku wengine hawamjui hata huyo Roma Mkatoliki kwa sababu maofisini mwao they have bigger fish to fry. Watanzania wangapi wanasikiliza, much less be swayed, na nyimbo za Roma Mkatoliki?

Alikuwa na msimamo gani kinyume na watawala huyo Roma? You can't even articulate what he stood for. Vi media vyetu third world viko nyuma sana.
 
Back
Top Bottom