Kwanini kuna baadhi ya watu hupenda kumwaga maji yaliyotumika njiani/barabarani?

Blue Bahari

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
1,207
1,109
Wakuu kwema!
Katika tembea yangu mikoa/maeneo mengi ya Tz, nimeshuhudia bahadhi ya maeneo kuna watu hupenda kumwaga maji yaliyotumika njiani au barabarani ktk eneo aidha analofanyia shughuli za kibiashara au nyumbani kwake.
Katika uchunguzi wangu nimebaini kwamba wamama/wakina dada ndiyo wanaongoza pakubwa ktk kufanya hivyo, hii ni kwa kuwa maji yale yaliyotumika ni aidha yametokana baada ya kufanyiwa usafi wa kudeki, kufua au kuosha vyombo.
Swali:
Kwa nini wanapenda kumwaga maji hayo barabarani au njiani ilihari unakuta maeneo kama ya biashara kuna mifereji ya wazi ya maji taka? Au vile vile kama ni nyumbani unakuta kuna majalala na pengine sewage system za mitaa zipo lakini bahadhi hupenda kumwaga njiani/barabarani.
(1) Je, lengo ni kusafisha njia/barabara (kuondoa vumbi)?
(2) Je, lina uhusiano na ushirikina ktk biashara?
(3) Je, ni mazoea tangu enzi na enzi (haina haja ya sewage systems)?
Karibu tufahamishane wajuvi wa masuala mtambuka kama haya, kwa kuwa binafsi nimeshindwa kupata jawabu la moja kwa moja.
cc Mshana Jr

Note:
Tuendelee kuchukua tahadhari dhidi ya Covid-19.
 
Uwelewi nini sa apo bwana bahari

Sent from my SM-A105G using Tapatalk
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom