Kwanini kumshitaki Mbowe ni ngumu kuungwa mkono wa watu

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,601
8,741
Watanzania tuna utamaduni wa kujuana hivyo kama unamjua mtu ni vigumu sana kubadilisha msimamo wako

Mbowe kwa wakazi wengi wa Dar-es-Salaam wanajua na ni kati ya wale watu ambao wamejulikana kabla hata ya siasa. Mbowe tofauti na wanasiasa wengi kasoma Dar es-salaam, wazazi wake walikuwa wafanyabiashara wa muda mrefu Dar, kaka yake alikuwa afisa mkubwa jeshini kwa miaka mingi na ameanza kufanya biashara tangia akiwa na miaka 20's.

Amekuwa akifanya biashara za muziki toka miaka ya 1980's alikuwa na club ya muziki wa vijana, kampuni ya magazeti na biashara nyingine za kuachiwa na Baba yake. Hivyo Mbowe pamoja na kwamba alikuwa mbunge wa Hai ni mtoto wa Dar mjini amekuliwa Dar na amekuwepo toka wakati wa Nyerere.

Mbowe baba yake alitaifishwa mali zake wakati wa nyerere pamoja wa wahindi wa kule upanga miaka ya 1970's hivyo wafanyabiashara wengi wanaiheshimu sana familia yake na ndiyo maana huta ona wafanyabiashara wakimuongea vibaya mbowe na familia yake.

Hizi kesi zinazokuja sasa ka kigaidi hata ziwe na ushahidi gani ni vigumu kubadilisha watanzania mawazo kwasababu Watanzania wengi kwa mazuri au mabaya wanamjua Mbowe. Mbowe hawezi kuishi miaka 40 kwenye macho ya watu eti leo abadilike kwasababu ya watu kama wakina Sabaya.

IGP Siro na viongozi wengine ambao wameshidwa kufanya uchunguzi wa kesi ya Lissu kwa jamii hawawezi kuaminika kuliko Mbowe mtu ambaye amekulia machoni mwa watanzania wengi na wakazi wa Dar. Watanzania wanajua watu kwa undani kutokana ha historia yao na siyo maneno pekee.

Tatizo hata watu wa CCM ambao wanajua Mbowe wanajua kesi hii ni ya kupikwa. Hakuna kiongozi hata mmoja wa usalama au chama ambaye watanzania wanamjua kuliko Mbowe. Hata Rais Samia familia yake haijulikani kuliko familia ya Mbowe.

Hivyo ni ngumu sana wananchi kuwaamini Serikali kwenye hili. Tofauti na watu wengine huyu ni mmoja ambaye huwezi kufuta historia yake na hii ndiyo sababu mpaka leo ni mwenyeketi.
 
Mashtaka mahakamani hayajitaji popular opinion..
Inahitajika evidence tu..
Kama evidence zipo basi kesi ipo..
 
Kuna ntu alitaka kumfuta Mbowe lakini leo hii ntu yule hayupo tena dunia hii.
 
Mbowe kugoma kuwa mateka wa CCM miaka yote ya mapambano yake ya demokrasia Tanzania ndio yanamsababishia matatizo na kina Sirro.

Sirro anasema walikuwa na ushahidi wa Mbowe kutaka kuchoma moto vituo vya mafuta wakati wa uchaguzi mkuu uliopita, walikuwa wapi muda wote huo zaidi ya miezi sita kumpeleka mahakamani mpaka alipoanza mapambano ya kudai Katiba Mpya isiyompendeza mwenyekiti wa CCM?

Hapa lazima kujiuliza, ni nini kimemsukuma Sirro kuja na hili tamko leo akijua fika hili suala liko mahakamani na anachofanya ni sawa na kuingilia uhuru wa mahakama?

Jibu ni simple tu, amekuja kujihami dhidi ya wale waliosema watahudhuria siku ya usikilizwaji kesi ya Mbowe, amekuja na tamko la kuwatisha ili wasijitokeze hiyo siku ikifika, nothing else.

Sirro ni vyema aache kutumika kwenye masuala ya siasa, atulie ofisini kwake atimize majukumu yake kulinda raia wa Tanzania bila kujali itikadi za vyama vyao, hizi mbinu anazotumia kuwabeba CCM zimepitwa na wakati.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom