Dom boy
Member
- Jan 24, 2018
- 99
- 64
Habari wahenga, naomba ushauri wa kitaalamu kutoka kwenu hasa kwa wale ambao ni wafugaji wa kuku. Nina mradi wa kufuga kuku wa kienyeji, napata changamoto wakati kuku wanapoumwa ugonjwa wa homa ya tumboni, nilishauriwa dawa inayotumika kutibu ni Esb3 30%, lakini ajabu ninapochanganya na dawa inayoitwa Vitalyte baada ya muda mfupi kuku hupoteza uhai, pamoja na kufuata vipimo vilivyopendekezwa lakini bado anapoteza uhai, je nauliza hizi dawa hazitakiwi kuchanganywa katika chombo kimoja au kuna nini kinatokea? naomba ufafanuzi.