Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,672
- 40,549
Katika mgongano wa kifikra swali jepesi kama hilo laeza kusababisha maoni mengi na ya ajabu sana. Tangia miaka ya enzi na enzi swali hilo limekuwa likipatiwa majibu tofauti kufuatana na ni nani anayetoa jibu hilo. Ukienda kwenye blogu ya michuzi utaona jinsi watu wanavyofikiri ni jinsi gani watu mashuhuru wamejaribu kulijibu swali hilo au ni jinsi gani wangejaribu kulijibu swali hilo. Swali hili lina falsafa iliyofichika na linahusu haki, uhuru, maono, mwelekeo na mtazamo.
Wewe ukiulizwa swali hilo, unafikiri ni kwanini "kuku aliamua kuvuka barabara"?
Wewe ukiulizwa swali hilo, unafikiri ni kwanini "kuku aliamua kuvuka barabara"?