Kwanini kukiwa na msiba maduka ya majirani yanafungwa

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
3,401
1,604
Ni kawaida kuona maduka yakifungwa endapo kuna mtu amefariki na msiba upo jirani na maduka hayo.

Swali langu ni kwamba, kwanini maduka yafungwe? kuna uhusiano gani kati ya msiba na maduka?

Utakuta watu waliopo msibani wanashida ya kununua vitu dukani lakini wanaenda mbali sana kununua kwakuwa maduka ya majirani yote yamefungwa. Hata chumvi mtu anaenda kununua mbali kweli yote ni sababu maduka yamefungwa.

Unakuta pengine hao wenye maduka wamefunga maduka sio kwamba wapo msibani, wengine wanafunga kisha wanaenda kwenye mihangaiko mingine na hiyo inadhihirisha kwamba hakuna logic yoyote ya kufunga duka ila ni mazoea tu.

KWANINI KUKIWA NA MSIBA MADUKA YA JIRANI YANAFUNGWA????

Posted by: MCHUNGUZI HURU (Associate Professor)
 
Last edited by a moderator:
Yaani utakua kauzu balaa...ufungue duka wakati jirani kuna msiba?
 
Mkuu mbona lipo wazi hili suala uingize pesa wakati watu wanaomboleza kwa kuondokewa na mpendwa wao? Ni utu ndio unawafanya wafunge maduka
 
Khaa!! Siyo hivyo bana hii inategemea ni msiba wa kabila gani. Kuna makabila mengine hata kama una bucha karibu wewe fungua kisha weka pombe utauza balaa :glasses-nerdy:
 
Mkuu mbona lipo wazi hili suala uingize pesa wakati watu wanaomboleza kwa kuondokewa na mpendwa wao? Ni utu ndio unawafanya wafunge maduka
Hapana bana. Hii ni kuleta usumbufu tu. Kukiwa na duka mmoja anaingiza pesa na mwingine anapata huduma. Tena ukiwa unatoa huduma ya vinywaji utauza sana na kufanya wataka huduma wasiende mbali :glasses-nerdy:
 
Misiba hasa ya wachaga ikitokea maduka yote ya majirani huongeza bajeti ya pombe maana ndo siku za mauzo. kufa kufaana
 
ni ujirani na utu wema...yaani in short unataka kufaidika kifedha kwa kufiwa kwa mwenzio, labda kama haukai maeneo hayo...
 
mbona hujiulizi kwanini akifa kiongozi mkuu wa nchi kuna mapumziko ,unatokea wapi kwenu kuna ustaarbu kweli
mambo mengine ni uungwana
 
Ngoja nijaribu hii njia, pengine Mzee wa Maswali anaweza akawa na majibu leo.

CC lukelo sakafu
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mbona lipo wazi hili suala uingize pesa wakati watu wanaomboleza kwa kuondokewa na mpendwa wao? Ni utu ndio unawafanya wafunge maduka
Kwa hiyo wafiwa wakanunue sanda mbaali kisa muuza sanda kafunga duka lake kwa kuwa ni jirani?
 
Ni kawaida kuona maduka yakifungwa endapo kuna mtu amefariki na msiba upo jirani na maduka hayo.

Swali langu ni kwamba, kwanini maduka yafungwe? kuna uhusiano gani kati ya msiba na maduka?

Utakuta watu waliopo msibani wanashida ya kununua vitu dukani lakini wanaenda mbali sana kununua kwakuwa maduka ya majirani yote yamefungwa. Hata chumvi mtu anaenda kununua mbali kweli yote ni sababu maduka yamefungwa.

Unakuta pengine hao wenye maduka wamefunga maduka sio kwamba wapo msibani, wengine wanafunga kisha wanaenda kwenye mihangaiko mingine na hiyo inadhihirisha kwamba hakuna logic yoyote ya kufunga duka ila ni mazoea tu.

KWANINI KUKIWA NA MSIBA MADUKA YA JIRANI YANAFUNGWA????

Posted by: MCHUNGUZI HURU (Associate Professor)

Ngoja ufiliwe na mtu unayempenda ndio uje na huo mswali wako...manyokoo
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom