Kwanini komredi Polepole na Jaji Warioba waliokuwa wajumbe wa Tume ya Katiba wanasema huu siyo wakati muafaka wa kutengeneza Katiba?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,867
141,803
Komredi Polepole alisema kimsingi Katiba huandaliwa na Rais anayetoka madarakani kama ilivyokuwa mzee Kikwete lakini siyo aliyeingia madarakani.

Jaji Warioba anasema Katiba ni sheria ambayo hubadilishwa wakati kwa wakati kulingana na mahitaji na kwamba sasa siyo muda muafaka kwa sababu hatutaweza kufanya kura ya maoni kutokana na janga la kidunia la Covid 19.

Je, Jaji Warioba na Komredi Polepole wana hoja?

RIP Dr Sengodo Mvungi!
 
Naamin kwel hakuna mkate mgumu mbele ya chai bwashee
Ni kweli kabisa.

Hivi Jaji Warioba haoni umuhimu wa Katiba mpya, huku nchi ikipita kipindi kigumu kabisa cha wapinzani kuwa "treated" kama wahaini ndani ya nchi yao??

Hivi huyo Polepole aliyekuwa akiipigia debe Sana Katiba mpya, wakati uke kabla hajapewa "ulaji" wa kuwa msemaji mkuu wa CCM, hivi haoni namna mfumo wa utawala haujakaaa sawa, kiasi ambacho chama tawala kilivyo hata na uwezo wa kumbambikia kesi ya ugaidi Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini??
 
Komredi Polepole alisema kimsingi Katiba huandaliwa na Rais anayetoka madarakani kama ilivyokuwa mzee Kikwete lakini siyo aliyeingia madarakani

Jaji Warioba anasema Katiba ni sheria ambayo hubadilishwa wakati kwa wakati kulingana na mahitaji na kwamba sasa siyo muda muafaka kwa sababu hatutaweza kufanya kura ya maoni kutokana na janga la kidunia la covid 19...
Kumwita polepole komredi ni kuikosea adabu hiyo taito.
 
Pale Polepole anapokataa kwenda polepole😁😁😁
 
Huyu mzee Warioba baada tu ya mwanaye Kippi kupewa uDC akabadikika kabisa. Amebadilika kwasabb yeye na mwanaye wanashiba na kusaza kwa katiba hii mbovu.
 
Hivi Jaji Warioba haoni umuhimu wa Katiba mpya, huku nchi ikipita kipindi kigumu kabisa cha wapinzani kuwa "treated" kama wahaini ndani ya nchi yao??
Mzee Warioba ni muumini mzuri sana wa Katiba mpya, nafikiri mleta hoja kaongeza chumvi - Mzee warioba yupo tayari hata leo kutuongeza kumalizia mchakato wa katiba mpya ambao kilichosalia ni kuileta KATIBA pendekezwa ili wananchi tuipigie kura.
 
Komredi wako ni muongo wa kutupwa, Katiba ya mwaka 1977 tunayoitumia ilipatikana Nyerere akiendelea kubaki madarakani kwa miaka nane zaidi.

Kenya walipigia kura za maoni katiba mpya mara mbili katika vipindi viwili vya Mwai Kibaki
Komredi Polepole alisema kimsingi Katiba huandaliwa na Rais anayetoka madarakani kama ilivyokuwa mzee Kikwete lakini siyo aliyeingia madarakani...
 
Kwasababu chadema wanataka kuitumia kurudi bungeni baada ya kukataliwa nawananchi kwenye sanduku la kura

Katiba itapiganiwa na wananchi sio wanasiasa
 
Komredi wako ni muongo wa kutupwa, Katiba ya mwaka 1977 tunayoitumia ilipatikana Nyerere akiendelea kubaki madarakani kwa miaka nane zaidi.
Kenya walipigia kura za maoni katiba mpya mara mbili katika vipindi viwili vya Mwai Kibaki
Nimekuelewa bwashee.

Umeshakata tiketi ya gari moshi?
 
Gharama mnazotumia kuandaa maigizo ya uchaguzi ni kiasi gani?
Sawa! hayo unayoyaita maigizo yaligharim pesa nyingi.

Mwaka 2020 ilikuwa kwa kukadiria ni Bil 331 na maandalizi Bil 157. Embu fuatilia uthibitishe kwenye nyaraka.

Haya jibu swali langu, gharama za kufufua mchakato wa katiba mpya unafikiri ni kiasi gani?
 
Sawa! hayo unayoyaita maigizo yaligharim pesa nyingi.....

Mwaka 2020 ilikuwa kwa kukadiria ni Bil 331 na maandalizi Bil 157. Embu fuatilia uthibitishe kwenye nyaraka.

Haya jibu swali langu, gharama za kufufua mchakato wa katiba mpya unafikiri ni kiasi gani?
hauzidi bilioni 150
 
Back
Top Bottom