Kwanini Kitambulisho cha Taifa kinakuwa na muda wa kuisha?

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
1,206
2,701
Vitambulisho vyetu vya utaifa vimewekewa mda wa kuisha serikali imemaanisha nini kuweka ukomo wa kitambulisho au ni njia ya upigaji ambao umezoeleka.

Serikali ililenga nini kutupa vitambulisho vya aina hiyo kwa hiyo kikisha mda nitengenezewe kingine, mimi nachofahamu taarifa zangu hakuna mtu mwingine atakayezitumia hadi naondoka duniani iweje kuwepo ukomo wa kitambulisho hicho.

watanzania waliowengi hawajapata vitambulisho vya utaifa wengi wao wana namba za vitambulisho hivyo sasa hii naona kama haijakaa sawa hata kidogo!

Tunajuwa kuwa kunakufariki je hivi ni vigezo walivyoona vinafaa kuweka ukomo wa vitambulisho hivyo?

Mimi maswala ya vitambulisho hivi kuwa na mda wa kuisha bado sinauelewa wakutosheleza naomba wajuzi wanifafanulie kwani kuuliza siyo dhambi.
 

HIMARS

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
53,886
61,826
Ndani ya Miaka 10 kuna watu hufa, watu hubadili makazi, watu huoa na kuolewa, watu hubadili majina, watu hubadilika sura

Hivyo serikali inataka iwe na uhakika wa mtu husika ndo maana kitambulisho huhuhishwa
 
3 Reactions
Reply
Top Bottom