Kwanini kila tukinunua umeme na maji tunakatwa kiasi fulani kwa ajili ya Taasisi nyingine za Serikali?

bubo

Member
Nov 7, 2012
45
32
Heri ya Mwaka mpya kwa wote hapa.

Hoja yangu ni moja tuu kwa nini kila tukinunua umeme na maji tunakatwa percentage flani kwa ajili ya Taasisi zingine za Serikali? madhalan EWURA

EWURA inafanya kazi gani mbona huduma na kiwango(quality) ya maji katika mamlaka nyingi za maji ni mbovu?
Ni mamlaka chache sana za maji mtu anaweza chota maji kwenye bomba akanywa direct.

Swala lingine ni umeme kukatika katika na kuharibu vifaa vya Watu EWURA wanalindaje wananchi dhidi ya mtoa huduma TANESCO?

Mimi kwa maoni yangu naona huu utitiri wa taasisi zinazonyonya mwananchi ni vema zingetolewa au kuunganishwa maana hazina tija.

Ukiangalia kwa sasa wamegeukia mafuta tuu kila baada ya siku kadhaa kupanga bei.....hivi hatuwezi kuwa na stock hata ya miezi 6 bei ya mafuta ikabaki constant walau kwa muda flani? Madhalan miezi 6 hivi hii itawezesha wengi kuweza kupanga vema especially wale Wa sekta za usafirishaji na uzalishaji viwandani!

Nimeongea tuu mawazo yangu kwa sauti
 
EWURA ni regulatory Authority
wanaunganishwa wote wanaofanya kazi za ivyo?
Zinakuwa ni departmets tofauti Ila Taasisi ni moja!
 
Si ndo kulipa kodi kistaarabu,badala ya kuviziwa barabarani kuombwa kipande

 
Pesa zote zinaenda serikali kuu, hakuna cha EWURA, MTANESCO wala nn, lazima nao wapige magoti kuomba ili wapewe hakuna pesa inayo ingia account ya shirika

Koo ni mojawapo ya kuongeza mapato tuu ya nchi na sio kingine.
 
EWURA ni regulatory Authority
wanaunganishwa wote wanaofanya kazi za ivyo?
Zinakuwa ni departmets tofauti Ila Taasisi ni moja!
Unajiona umetoa booonge la jibu na inaeleweka vizuri tu.
 
Back
Top Bottom