Kwanini kila kitu Tanzania lazima ununue kwa pesa tasilimu?

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,449
17,148
Kwanini kila kitu huku kwetu Tanzania lazima mtu anunue kwa pesa tasilimu(cash money)?

Tanzania ukitaka simu lazima uwe na cash, ukitaka gari lazima uwe na cash, ukitaka samani za ndani lazima uwe na cash money, yaani kila kitu ni cash.

Vitu kama simu mitandao ya simu hua na offa ya mtu kuchukua simu na kuanza na down payment kiasi fulani unachukua simu kisha unalipa kila mwezi kiasi fulani hadi deni linaisha.

Vodacom South Africa wana hiyo huduma, sio Ulaya ni hapa Africa ila ukija Tanzania huduma kama hizo hazipatikani, bila cash hupati huduma.

Makampuni ya simu kama Samsung au Apple huko nchi nyingine wana ofa ya kurudisha simu ya zamani na unalipipa kidogo kubadilisha simu mpya, huku kwetu hizo huduma hazipo.

Ikija mpya nunua hutaki acha. Hii haijalishi wewe ni mfanyakazi wala mfanya biashara. Wafanyakazi sekta rasmi wanaweza tu kuaminiwa na bank au taasisi za fedha tu hapa Tanzania.

Makampuni au wakala wa magari Tanzania ni lazima uwe na cash money. Ingawa sasa kuna makampuni machache yameanza kuuza magari on credit with some down payments kiasi fulani.

Hii ya kununua kila kitu on cash basis inatengeneza maisha yanakua magumu sana.

Je, nini kinasababisha nchi hii watu hawaaminiki kiasi hicho kwamba bila pesa tasilimu hupati huduma?
 
Kuna jamaa yangu mkorea by then alinunua simu sumsang S9 kipindi inatoka huko kwao kwa kulipa kidogo dogo, alisema kule kila MTU anajulikana anakaa wapi tatizo hapa Tanzania ni makazi ya watu hawatambuliki wengi wafanya kazi zisizo rasimi.
 
Mkuu usibeze, hiyo nayo ni hoja ya msingi ukiangalia life expectancy ya nchi za ulaya na afrika ni tofauti kabisa.
Afrika watu wanaishi muda mfupi sana!
South Africa ni Ulaya? Halafu sio lazima ununue bidhaa za mamilioni hata samsung mobile phone waweza nunua kwa installment
 
90% ya watu vijijini wanaishi bushmen life style.
Huko mijini wengi ni 'formalised' chokoraa.
Uaminifu, na kipato ni ngumu mno! Watu wanaishi kwa 'timing', atakayezubaa anapigwa, na maisha ya mwingine yanasoma kwa siku husika.
 
Back
Top Bottom