Kwanini kila kitu serikali ndio ilaumiwe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini kila kitu serikali ndio ilaumiwe?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mamzalendo, Jul 5, 2011.

 1. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ndugu zangu nafikiri kuna kulaumu serikali kulikozidi,wananchi pia tuna wajibu wa kutenda na kuisaidia serikali,mfano katika suala la umeme je wahandisi umeme wa nchi nzima wakijitolea kutafuta suluhu ya hili jambo hata kama ni njia nyingine mbadala kweli hatutapata majibu kwani lazima wazungu tunasomesha vijana wa nini?mfano wa pili ni mtu anayelalamika njaa wakati maji yanapita hapo mdomoni kwake anapewa chakula sawa na m2 aliyepo sehemu yenye jangwa pasipo kuwajibishwa?kweli serikali inatakiwa kutembea na viboko kufundisha wananchi kila kaya kulima mboga kwenye bustani zao je elimu ya sayansi kilimo tuliyopata haitoshi kila mtanzania kulima bustani ya mboga?mfano wa tatu mtu umeajiriwa lakini mara nyingi unakuta ofisini ni internet na zogo serikali ifanyaje,ingawa serikali ina mapungufu lakini hata sisi wananchi tuna mapungufu,kama hata mitaro kando ya barabara ya kwenda kwako huwezi kuzibua ili mvua ikinyesha usidhurike unasubiri serikali kuna tatizo,jamani huu ndio mtizamo wangu mwenye hoja tofauti,nyongeza au masahìhisho nawakaribisha tujadili pamoja tusonge mbele.
   
 2. n

  nmiku Member

  #2
  Jul 6, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Serikali inalaumiwa kwa sababu uchumi wa nchi na maisha ya wananchi kwa ujumla kichocheo ni serikali. Mipango yeyote ya maendeleo bila kuwa na serilkali thabiti na yenye malengo mazuri yanayotekelezwa na kwa kufuata sheria halali zilizopo, hakuna kitakachoonekana au kufanyika.Serikali ikipindisha sheria kwa ajili ya waliopo madarkani tutasonga mbele? Raia mmoja ataweza kufanya nini kuliondoa taifa katika hali mbaya bila support ya serikali? Mfano ni huo wa umeme. Je, wahandisi wote nchini wakikaa pamoja na kuja na projects nzuri za kutatua tatizo la umeme watafanikiwa bila mkono wa serikali? Jibu ni kwamba watakwama kama report nzuri kibao zinazootea vumbi makabatini kwa kuwa wao wenyewe hawana capital ya kutekeleza hayo mawazo yao mazuri. Kwa hiyo serikali ndiyo ya kulaumiwa kwa kutoweka interest za taifa mbele badala yake ubinafsi ndio uliokidhiri- they talk on principle, but act on interest. Kilimo cha mchicha kitaliinua taifa kutoka hapa tulipo kutupeleka kwenye faraja? It is more than that. Kwa hali ya nchi ilivyo sasa hivi, serikali lazima iwe ya kulaumiwa penda usipende.
   
 3. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kwa serikali ambayo rais wake kila siku analalamika tu pasipo kuchukua hatua
  unategemea nini? Serikali inayoweka sheria lakini ikashindwa kuzisimamia unategemea
  nini kama si kulaumiwa? Serikali ambayo inashindwa kuwawajibisha viongozi wanaofanya
  makosa na kuhujumu taifa pamoja na kuwepo ushahidi wa wazi unataka isilaumiwe?
  Hata pale wananchi wanapoonekana wazembe au hawataki kujitolea ni kwa sababu ya
  serikali isiyo na uzalendo kwa watu wake, iliyowakosesha watu wake moyo wa kizalendo
  wa kulitumikia taifa lao (rejea habari ya mabondia waliogoma). Siku hizi hata ule wimbo
  mtamu wa Tanzania Tanzania, nakupenda kwa moyo wote... hauimbwi tena!

  Kwa serikali ya kifisadi inayoua watu wake na isiyojali wanyonge kwa kuwaondoa
  kwenye ardhi yao na kuwapa wageni kwa kisingizio cha uwekezaji, lawama zitaendelea
  daima dumu.
   
 4. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wananchi wana kila sababu ya kuilalamikia serikali kwakuwa inatekeleza sera ambayo imetoa fursa kwa watu wa chache kwa kushirikiana na mabeparei wa kimataifa wanatumia rasilimali ya nchi hii kwa manufaa yao wenyewe wakati umma waq watanzania unaendelea kudidimia kwenye dimbwi la umasikini
   
 5. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  nashukuru wote kwa michango yenu lakini naomba kuuliza baba akiwa mzembe watoto nao wanatakiwa kuwa hovyo kwa sababu baba ni mzembe?je watoto hawana wajibu wakujishughulisha na kumuinua huyo baba mzembe kwa njia yoyote? nakubali serikali ina mapungufu tena mengi lakini hata wananchi tuna mapungufu kwa sababu hao viongozi wabovu serikalini wanatumia wananchi, watu wangeamua kutokutumika ubovu ungetoka wapi?bosi hawezi kuiba mwenye lazima atawashirikisha watu kibao kutekeleza azma yake. kuna sehemu wananchi tunajipotezea ajira wenyewe mfano unaajiriwa mahali unaiba kazi ya ofisi unaenda kuifanya na watu wengine hivi kuna mtu atakuwa tayari kuajiri je serikali inatakiwa itafutie ajira watu kama hawa? kwa nini wawekezaji wanaajiri zaidi wakenya kuliko watz lazima kuna sehemu utendaji ni mbovu wa watumishi?
   
 6. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #6
  Jul 6, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  there is lack of vision and self initiative among us the citizens.
   
 7. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #7
  Jul 6, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mfano mwingine mtu ametoa msaada kajenga kituo cha watoto yatima lakini akasema mimi nitatoa nusu ya chakula na wananchi watoe nusu wote wanaozunguka kituo wakabaki wanang'ang'ana atoe zote yule mtu ameacha kutuma na kituo kimefungwa je serikali sehemu kama hii ilitakiwa ifanya nini?
   
 8. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #8
  Jul 6, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Siyo kweli. Yote yaanzia kwenye serikali isiyo na maono, yenye viongozi wabinafsi wanaojineemesha
  wao na familia zao. Pia mfumo wa elimu uliopo unawajenga vijana kuwa mafisadi kuliko kuwa
  wazalendo na nchi yao. Mfumo uliopo wa elimu yetu ni wa mwanafunzi kufaulu mitihani na si
  kuelewa, ndiyo maana ukiomba kazi unaulizwa vyeti, ndiyo maana wanaopewa mikopo ni wale
  wa daraja la kwanza, ambao kwa vyovyote ni watoto wa vigogo waliosoma kwenye shule bora
  na si hizi za walalahoi (za kata). Ndiyo maana wanafunzi kwa kushirikiana na wazazi wao wanaiba
  mitihani ili wafaulu na kupata daraja la kwanza, hapo hakizingatiwi kuelewa bali kufaulu.

  Sijui unategemea nini kwa mtu aliyeiba mitihani tangu shule ya msingi hadi chuo kikuu
  anapokuja kupewa madaraka? Si atakuwa fisadi? Tusidanganyane bhana, ubovu wote unaanzia
  serikalini.

  Kama si serikali, ulitaka alaumiwe nani? Wao kwa wao hawaheshimiani, rais anatoa maagizo
  wasaidizi wake wanayadharau...

  Shameless country!
   
 9. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #9
  Jul 6, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Usiwe na mawazo mgando, kama wakubwa wanapeana posho na mishahara minono huku wakibugia hata kodi
  ambazo wananchi wanakatwa ili zilete maendeleo, unategemea nani atakuwa na moyo wa kujenga nchi.
  Kwanza serikali iwaombe radhi wananchi na ikiri makosa, kisha wote kwa pamoja (serikali na wananchi) waanze upya.
  Vinginvyo hakuna anayeweza kujitolea wakati kodi alizokatwa hajui zinafanya nini!
   
 10. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #10
  Jul 6, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kituo kimejengwa na mzungu aliyejitolea baada ya kufika kijijini na kuona tatizo na ikatumwa kupitia kanisa sasa serikali wapi hapa?
   
 11. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #11
  Jul 6, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,628
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Nakushauri ujifunze kwanza! Siku utakapojua role ya serikali ktk maendeleo ya nchi na ustawi wa wananchi..,na siku utakapojua wajibu wa wananchi na asasi za zingine za kiraia na zisizo za kiraia ndipo utakapojua yupi anatakeleza wajibu wake au anapashwa kutekeleza wajibu gani...ndipo utajua kama serikali inalaumiwa na kwa yapi inapaswa ilaumiwe na kwa nini?Kwa sasa ama afraid huna ufahamu mzuri sana. Let me hope kwamba ww si mwanasiasa na kama ni mwanasiasa natasikika kwa kuandika hii thread..Mwisho nikuulize honest question ambalo linareflect hayo nilioeleza hapo juu...je umeshawai sikia serikali inawalaumu wananchi au azaki nk? Kama umewai sikia ni kwa nini ifanye hivyo?Wakatabau
   
 12. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #12
  Jul 6, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  tatizo hamnielewi ninachosema serikali na wananchi wote wanawajibu na majukumu yao na haiwezekani kabisa upande mmoja ndio ilaumiwe tu na wewe naomba kuuliza serikali inaundwa na akina nani kama wananchi hawapo? ni wazungu ndio viongozi? viongozi wa vijiji ni wananchi au wazungu?kama mwananchi bila uongozi ni corrupt akiwa kiongozi je? je viongozi hawatumii wananchi kuiba?
   
 13. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #13
  Jul 6, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,628
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Kwanza toka nje ya chupa kama analivyojisemea mbunge mmoja. Pili ukiona watu hawakuelewi jaribu kujichunguza kwanza wewe kwanini haueleweki..toka nje ya chupa kwa sababu ya mtazamo mgando. Twende na tafsiri yako kuwa serkali ni wananchi sijui ulikuwa unamaanisha kuwa serikali ni ya wananchi au.. Je unamaanisha kuwa haipaswi kulaumiwa au ni kiwango kipi ambacho wewe unakikubalikuwa mpaka hapa ni sawa serikali ilaumiwe? Kabla sijaendelea kujibu maswali yako ambayo nasikitika yameonyesha kutotaka kujifunza au kubadilika. Je unafahamu role ya serikali?
   
 14. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #14
  Jul 6, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,628
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Kuna mfano umetolewa hapo juu kuwa mtu anajenga kituo cha watoto yatima na kuwatakla walengwa kuchangia nusu ya mahitaji.

  Kwa mtu anayefahamu mchakato wa maendeleo... ile approach tu inaweza kuleta malalamiko makubwa na hata kupelekea hicho ambao mtu au watu waanafikiri ni msaada mzuri uonekane si kitu mbele za watu..

  Kwa hili niseme tu kuwa avarage binadamu ni rational irrespective amepata elimu dunia au la? Na mara zote huwa sahihi ktk incidence kama hii ambayo inasound kuwa ushirikiano ktk hilo jambo la maendeleo ulikuwa mdogo sana.
   
 15. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #15
  Jul 6, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hivi ni wapi huko wasipoilalaikia serikali ikishindwa kutekeleza wajibu wake?
   
 16. data

  data JF-Expert Member

  #16
  Jul 6, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,786
  Likes Received: 6,558
  Trophy Points: 280
  hailaumiwi serikali.. ianalaumiwa CCM....!!!????
   
 17. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #17
  Jul 6, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,628
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  I have a strong feeling kwamba ww ni mwanasiasa..let's hope you are not one of the MPs we see on TV praising the government day in day out..nakuuliza hivi who told you kwamba ni serikali ndio inalaumiwa peke yake? Unless somebody told you ortherwise usingeuliza swali hili hapa?Kingine ni kwamba feeling kwamba serikali inalaumiwa kwa mambo fulani inategea uko upande gani...kwa wananchi kulaumu serikali (nafikiri labda neno kulaumu ndio shida hapa) kwa mapungufu wanayoyaona nadhani ni sahihi tu...kwa upande mwingine kwa aliye serikanini its a bitter pill..kwani atakuwa anatarajia kusifiwa kama baadhi ya wabunge wanavyofanya...badala ya kuisimamia matokeo yake tunashindwa kuaddress properly issue that matters most kama ya umeme.
   
 18. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #18
  Jul 6, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mimi si mwanasiasa ila nina mitizamo yangu tu kwa hiyo nisaidie kubadilisha mitizamo yangu kwani mpaka sasa hujafanikiwa inawezekana nina tatizo la kutoelewa haraka embu weka hapa role za serikali na wananchi unavyoelewa wewe?ili kunielewesha zaidi
   
 19. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #19
  Jul 6, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Sikuwa nimepanga kupoteza muda kwenye hii thread ila kwa kuwa inaonesha kuwa una mapungufu sina budi nikuweke sawa. Unajua maana ya neno "Mamlaka", Authority?. Kama unajua haya basi hukupaswa kuanzishwa thread hii. Serikali ina mamlaka ya kukusanya kodi, kuzilinda na kuhakikisha hazitumiwi visivyo. Serikali ina mamlaka na kwa kuwa ina mamlaka basi kila kitu kinapoenda mrama wa kulaumiwa ni serikali ambayo inashindwa kutumia mamlaka iliyopewa kuhakikisha mambo yanaenda vizuri.

  Unataka wahandisi wajitolee suala la umeme kwa mamlaka gani waliyonayo?, Anyway, kajifunze kwanza kama mtu mmoja alivyokushauri hapo juu.
   
 20. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #20
  Jul 6, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Serikali yetu haina aibu, huwa inadai hata visivyo halali yake... mfanbo pesa za rada
  halafu wakizitia mkononi wanajineemesha wao na familia zao. Acha walaumiwe kwa
  kuwa hata wakijenga barabara wanajisifia wakati ni wajibu wao. Ni ajabu baba anajisifia
  kuwanunulia kaptula watoto wake!
   
Loading...