Kwanini kikwete na ccm wasitengwe kama ivory cost | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini kikwete na ccm wasitengwe kama ivory cost

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by niweze, Dec 8, 2010.

 1. n

  niweze JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Leo Tumesikia Jinsi Gani Umoja wa Mataifa, UN na Umoja wa Afrika Magharibi Kutomtambua Mgombea Uraisi wa Ivory Coast, Gbagbo Baada ya Kujipa Uraisi Mwenyewe. Kitu cha Kushangaza Kikwete Hakupata Kiboko Kama Hiki. Kuna Vitu vya Kuaangalia Hapa. Watanzania Kweli Tupo Slow Sana Kureact na Huu Utamaduni wa Upole na Kugeuzia Shavu la Pili Ukipigwa Ndilo Lina Tuangusha Hapa. Kama Watanzania Wangeoonyesha Kwa Nguvu Zote Hawakubali Kuonewa na Wizi wa Haki Yao ya Kupiga Kura, Kikwete Either Asingekuwa Raisi au Angekuwa Ametengwa na Afrika na Umoja wa Mataifa. Hizi Nchi za Ulaya na America Siku Zote Wanaangalia Reaction Toka Ndani ya Inchi na Kama Kuna Support Kubwa ya Kupambana na Udikteta Wangeweza Kutusaidia kwa Hali na Mali. Kwa Huu Uchaguzi 2010, Tumejimaliza Wenyewe na Itaendelea Kutokea Mpaka Watanzania Watafanya Mapinduzi Wenyewe. Leo Hii Kama Wananchi Wangeonyesha Nguvu Mitaani Dr Slaa Angetambulika Raisi wa Tanzania. Nafasi Nyingine Tumepoteza ya Kuondoa Uongozi Mbovu...Angalia Ivory Coast Watu Wapo Mtaani na Hakuna Kumtambua Kiongozi Alieiba Demokrasia. Siku Zote Tukae Tukijua CCM Sio Marafiki Zetu ni Maadui wa Wananchi na Tanzania na Akiondoka JK Atakuja Mwingine na Shati la Kijani Kuanza Upya Udikteta...

  Hivi Vyama vya Upinzania Haviwezi Kufanya Kazi Peke Yao Kama Wananchi Hawaonyeshi Kuchoshwa na Kuumizwa na CCM. Viongozi wa Chadema Wanafanyakazi Kubwa na Wamefanikiwa Kujenga Vision ya Inchi na Support ya Wananchi Bado Haijafikia Wengi Tunavyoona Hali Halisi Ilivyo. Watanzania Tunataka Nini Sasa? Kitu Kikubwa cha Kufanya ni Kuhakikisha Tunasupport Hii Iniative ya Katiba Mpya, Jiunge na Watanzania Kujenga Katiba. Mpaka Lini Mtanzania Atapewa Kanga na Miwani ya Kuonea ili Aipigie Kura CCM?
   
 2. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  ...soon this is will take palce!!!
   
 3. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #3
  Dec 8, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  tusijilfananishe na nchi ambazo wananchi wao wana uchungu na mali za nchi.
   
 4. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #4
  Dec 8, 2010
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Mkuu Wenger, unafahamu msemo wa maji yaliyomwagika hayazoleki? Violence begats violence and it I vicious circle. Nadhani hii inabidi iwe last resort when all other means fail. Mi nadhani CCM is doing a very good job ya kujimaliza, tena haraka. Kama mkuu Azimio Jipya alivyosema hao juu we are getting there! Na misaada ikiwa cut off ndipo tutaweza kujenga nchi yetu wenyewe maana in the eyes of Kikwete . "Tanzania bila misaada haiwezekani" lazima watatimuka!
   
 5. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #5
  Dec 8, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mkuu nimekuelewa kinachonitisha ni speed yao ya kuimaliza nchi hata huo mda ukifika wa ukombozi wetu itakuwa too late.
   
 6. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #6
  Dec 8, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Better too late than not at all!
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Dec 8, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Nadhani huwa mnasema kwa ushabiki zaidi ya kuwa na mantiki.
   
 8. v

  valour Senior Member

  #8
  Dec 8, 2010
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 167
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Tofauti ya Tanzania na Ivory Coast ni kwamba huku kwetu Tume ya Uchaguzi ilimtangaza Kikwete ndiye Rais, wakati Ivory Coast Tume ya Uchaguzi ilimtangaza Alassane Ouattara wa chama cha Upinzani. Hizi ni Tume ambazo kisheria ndio zinazo tambulika kumtangaza mgombea kuwa Rais.

  Hata kama kuna hisia za kuchakachua tume inayotambulika ikishatangaza vingenevyo hakuna cha kufanya Kwahio cha msingi ni kuendelea kupigania katiba mpya ili tupate tume huru.
   
 9. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #9
  Dec 8, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nachelea kuuita uchizi,
  Ivory Cost, upinzani umeshinda kwa 54%, hapa tanzania upinzai umeshinda kwa % ngapi? Kwa vyovyote vile, wapinzani hata TZ wapo JF tu huko uraiani hamna kitu.
  Nijuavyo, kama chadema wangeshinda nchi hii isingetawalika, jiulize tu majimbo machache ambayo walikuwa na nguvu kama mwanza mbeya na ubungo jinsi fujo zilivyokuwa, sote ni mashahidi, na vyombo vya habari (ambavyo vingi vinamilikiwa na wakristo) vikiwapamba kuwa wanadai haki
  Lakini kama CUF wangeshida wangepigwa virungu na kuitwa magaidi (huku vyombo vya habari vikiongezea msumari wa mote)
  Shame on you.
   
 10. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #10
  Dec 8, 2010
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Huyu ni sawa na Mchawi aliye anguka na ungo wake baada ya kapita juu ya paa la hekalu la "walokole". Kama huna hoja si ukae kimya kwani lazima uandike utumbo humu? Sasa wewe tukusaidieje? mi naona kakoj0e ukalale!
   
 11. n

  niweze JF-Expert Member

  #11
  Dec 9, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuna Baadhi ya Watanzania Hapo Juu Tunaona Wanasema Dr Slaa Hakundisha. Well Mnajuaje Kama Hakushinda Ushahidi Gani Utuonyeshe Watanzania Wote? Uundaji wa Tume CCM Wasimamie, Upigaji Kura CCM Wasimamie, Kuhesabu Kura CCM Wasimamie, Kuchallenge Kura Vituoni CCM Wasimamie, Kutunza Masanduku ya Kura CCM Wasimamie, Kutangaza Matokeo CCM Wasimamie na Mahakamani CCM Wasimamie. Je Watanzania Watasimamia Kitu Gani Tena? Kila Kitu Mnataka Msimamie Nyie...CCM Inataka Sana Vyama vya Upinzani Vishiriki Kwenye Uchaguzi kwa Sababu Huko Nje kwa Donors, EU na America Mnataka Waonekane Tanzania Inademokrasia Safi na Mikopo ya IMF na World Iendelee Kumiminika na Wao Kuendelea Kushop Magari ya Kifahari, Majumba ya Kifahari na Kuishi Maisha ya Ki-J-Z Wakati Wananchi Wao Wanakufa Mahospitalini Hivi Tunaongea.

  Kifupi ni Kwamba: Uchaguzi wa Tanzania ni Udanganyifu Mkubwa kwa Watanzania na Kweli Tunatumiwa ili Wao Waendelee Kututawala na Kutunyonya Milele. Tunajua Hili Kusupport CCM ni Kiss of Death...Hii Haitafly Tena na Iwe Mara ya Mwisho Kufungwa Kamba Kama Mbuzi.

  "CCM Imewashikilia Watanzania Hostage na Mpaka Sasa Hawataki Kunagotiate Chochote Wanaamini Wanahaki Kuwashikilia Mpaka Waamke"
   
 12. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #12
  Dec 9, 2010
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  We unaumwa kweli, hao JF wanakaa ndani ya JF. Tuko uraiani na huko uraiani unakosema hakuna wapinzani sijui ni wapi. lNahisi unaongelea magogoni

  Nasikitika kwamba hujui ni kwa nini hayo maeneo uliyotaja hali hiyo ilitokea. Sio kwa sababu ya CHADEMA, ila ni kwa sababu ya wajinga wenzako kutaka kuiba haki ya raia. Maeneo uliyotaja ni maeneo ambayo yanapaswa kupewa sifa ya pekee kimapinduzi maana yaliamua kukesha kupigania haki zao. Kama hujui msingi wa jambo, usilitolee mfano maana litakuaibisha na kuharibu mantiki yako yote.

  Waza kwa upana kabla hujaandika humu JF
   
 13. k

  kany Member

  #13
  Dec 10, 2010
  Joined: Feb 20, 2010
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nawaombeni Wanajamii tupiganie kwanza katiba mpya ya nchi ambamo hili la tume ya uchaguzi pia litarekebishika! Tume ikishakuwa huru hawa jamaa wa kijani watakuwa wameshakatwa mizizi na hivyo wataanguka tu wenyewe. Hapa ndipo pa kuanzia!
   
 14. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #14
  Dec 10, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Tofauti ni kuwa Tume ya Uchaguzi Cote D'Ivoire ilimtangaza Quattara mshindi na Gbagbo kushindwa lakini Bongo Lewis alimtangaza JK mshindi.
   
Loading...