Kwanini Kikwete hafai kupewa mhula wa pili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Kikwete hafai kupewa mhula wa pili

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ngongo, Oct 25, 2010.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Tarehe 31/10/2010 watanzania watapiga kura kuwachagua madiwani,wabunge na Rais wa JMT.
  Uchaguzi wa mwaka huu umekuwa tofauti na chaguzi zilizofanyika tangu siasa za vyama vingi viruhusiwe hapa Tanzania.Mwaka 1995 uchaguzi ulikuwa na heka heka nyingi zilizosababishwa na A L Mrema wakati huo akiwakilisha chama cha NCCR Mageuzi.Baada ya uchaguzi wa mwaka 1995 chaguzi zilizofuata zilikosa ushindani wa maana na kukiacha chama cha mapinduzi kikitawala siasa za Tanzania kwa muda mrefu bila upinzani wa wowote.

  CCM imejisahau pengine kwa kukosa chama cha upinzani tishio kwa muda mrefu.Upinzani wa maana ulitoka ndani ya CCM yenyewe.Wapo baadhi ya wanaCCM waliojaribu kurekebisha hali ya mambo wakaishia kutukanwa na kuitwa majina mabaya [Mwehu,wanawivu wa kushindwa na nk].Bado tunakumbuka jinsi wapigananji ndani ya CCM walivyopata msukosuko mkubwa hadi kutishiwa kupokonywa kadi za uanachama wa CCM kwa dhambi ya kumwadabisha Lowasa na Rostam Aziz.

  Mwenyekiti wa CCM Mheshimiwa J M Kikwete kaudhihirishia umma yuko upande wa mafisadi.Inawezekana watanzania wengi hawakuwa wakijua Rais wao yuko upande gani labda baraza la mawaziri,wajumbe wa NEC na kamati kuu walikuwa wanajua Kikwete anawaunga mkono marafiki zake waliokumbwa na kashfa kubwa zilizoitikisa Tanzania kiuchumi na kisiasa.Kitendo cha Rais Kikwete kuwapigia debe Bwana Basil Mramba ambaye kesi yake ipo mahakamani serekali yake kupitia ofisi ya mwendesha mashtaka wa serekali imemshtaki kwa kuisababishia hasara kubwa serekali kimedhihirisha Rais wetu [mpaka 31/10/2010] si makini kwa maslahi ya taifa bali ni mtu aliye tayari kuulinda urafiki kwa gharama yoyote.Kitendo cha kumpigia debe Lowasa kwamba hajaona kama yeye ni kulidharau bunge [wakiwemo wabunge wa CCM] kwamba hawakuwa makini kumwadabisha na pengine walimwonea au walikuwa na chuki na cheo chake cha uwaziri mkuu.

  Rais Kikwete sasa anatabirika kwamba akipewa tena nafasi ya kuliongoza taifa [Tanzania] ufisadi utapaliliwa,utawekwa mbolea,utalindwa kwa gharama yoyote,rasilimali za nchi zitatapanywa kwa namna isiyokuwa na maelezo.Mafisadi watakuwa na nguvu za ajabu watarudishwa tena na safari hii watahakikisha hakuna wa kuwasema tena watajiwekea ulinzi madhubuti [kisheria,kisiasa,kimafia].

  Watanzania muda wa kuondokana na udhalimu ni sasa tusisubiri mwaka 2015 kwa visingizio vya ajabu yamkini hatutapa tena sababu nzuri za kufanya mabadiliko kama mwaka huu.Tafakari chukua hatua tarehe 31/10/2010 nenda wewe,mke,mume,rafiki na jirani yako kapige kura kabla ya saa 10 jioni.Mpe kura yako Dr W Slaa kwaajili ya mabadiliko ya katiba,matumizi bora ya rasilimali za nchi[Tanzania],Elimu bure mpaka kidato cha sita,baraza la mawaziri dogo lakini lenye tija na kurekebisha mikataba mibovu [madini,EAC].
   
 2. Mussolin5

  Mussolin5 JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2016
  Joined: Apr 23, 2015
  Messages: 16,922
  Likes Received: 60,384
  Trophy Points: 280
  JK amestafu lakini sasa bado anatoa amri as if bado yupo Magogoni.
  Rejea alipotembelea Daraja la Kigamboni
   
Loading...