Kwanini Kikwete anawababaikia sana DIASPORA na kuwapa nafasi?

LEMONT BISHOP

Member
Oct 29, 2014
85
88
Cabinet yake kajaza hawa watu wa diaspora

Lawrence Masha
Adam Malima
Omari Nundu
Anna Tibaijuka
John Mashaka (Wanasema huyu alikataaa unaibu waziri)

kwenye mashirika ya Umma

huyu jamaa mpya wa TPDC
bosi wa TIC

etc...

Halafu wakishapewa hawaishi kuharibu na wengine dizaini za akina nundu huwa wanakuja kutaka mambo straight na haki bin haki mwishowe nadhani mnajua ilibidi aondolewe

Hivi inamaana mtu ukitaka kupanda juu inabidi usome nje ya nchi au?
 
Kazi ya TPDC ilitangazwa rais ana endorse recomendation ya waliofanya usaihili.
 
Utumwa wa fikra ni tatizo ambalo ni very deep rooted kwa jamii ya kiafrika. Kuna imani kubwa kwamba wageni ndiyo bora na vivyo hivyo aliyesoma na kukaa nje kwa muda ni bora zaidi ya mwenyeji. Msingi wa umasikini wa nchi unaanzia hapa.
Hata hivyo, ni muhimu sana kuwatumia wataalamu waliobobea kutoka ndani na nje ya nchi kuongeza tija katika uzalishaji ili kupata maendeleo ya haraka, lakini siyo kuwapa vyeo vya kisiasa!
 
hao wasomi wa nje ndio mwiba .mfano ni tibaijuka katoka umoja wa mataifa kaja kuiba hela za umma anasema mchango kwa shule yake yakitajiri
 
Nadhani mleta mada ulikuwa unakimbia kipindi cha hesabu darasani

Umeweka hapo mfano wa Diaspora waliopewa kazi ulitakiwa sasa upande wa pili uweke watanzania wa hapahapa ambao wapo kwenye nafasi nyeti serikalini halafu uweke percentage ndio utoe ka conclusion kako.

Naona umelewa togwa!!!!
 
Acha wivu wa kijinga kwan hao sio watanzania.kama wana sifa wacha wapewe ulitaka upewe wewe na wakat hata shule hukwenda
 
I really think we should not look at the Diaspora/Non Diaspora, but the knowledge and work experience in the respective field. I do not think currently we have people with both right knowledge and experience in the field of Oil and Gas in country.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom