Kwanini Kikwete alitembelea Australia?

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,870
Points
1,225

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,870 1,225
Habari
Ezekiel Kamwaga

Toleo la 416
29 Jul 2015

RAIS Jakaya Kikwete Jumatano wiki hii anamaliza ziara yake ya kiserikali ya siku nne nchini Australia lakini swali ambalo pengine Watanzania wangetaka kujua ni kwamba safari hiyo ilikuwa na umuhimu gani mkubwa kwa taifa letu.


Hili ni swali ambalo Watanzania wamekuwa wakihoji kila wakati inapotangazwa ziara ya Rais nje ya nchi. Kwa faida ya wasomaji, pengine ni vema kwanza nikaeleza kidogo kuhusu nchi ya Australia kiuchumi.

Taifa hili ni taifa la sita kwa ukubwa duniani. Kiuchumi, Australia ni nchi ya 12 kwa kuwa na uchumi mkubwa duniani. Hata hivyo, kwa maana ya uchumi wa raia mmoja mmoja, nchi hii ni ya pili duniani ikiwa nyuma ya Uswisi.

Pato lake la kila raia kwa mwaka ni wastani wa dola 66,000 (shilingi milioni 132) ambalo ni sawa na mara 60 ya pato la Mtanzania. Kwa vyovyote vile, hili ni taifa ambalo Tanzania inahitaji kuwa nalo karibu kama inataka kuendelea kiuchumi.

Hata hivyo, tangu kuingia madarakani kwa Tony Abbott kama Waziri Mkuu mwaka 2013, Australia imekuwa ikishutumiwa kwamba imetelekeza uhusiano wake na nchi nyingi za kiafrika hususani kwenye eneo la misaada.

Kimsingi, Rais Kikwete ndiyo kiongozi wa kwanza wa Afrika kufanya ziara nchini Australia tangu Abbott achaguliwe kuwa Waziri Mkuu. Kwa ziara hii ya Kikwete, bendera za Tanzania zilikuwa zikipepea nchini Australia na zimeitangaza nchi yetu kwa wananchi na wawekezaji watarajiwa.

Jambo ambalo nilijifunza nchini Australia ni kwamba serikali ya nchi hiyo ilimtaka Kikwete aende kwa sababu anachukuliwa kama mmoja wa viongozi mashuhuri wa Afrika. Kuna siri moja ambayo labda wengine hawaijui kuhusu Kikwete na Australia.
Nitaeleza kidogo kuhusu mtazamo wa raia wa Australia kwa Rais Kikwete.


Ni hivi, kwa sasa Australia inafanya biashara kubwa zaidi na China kuliko hata Marekani kama ilivyokuwa zamani. Hivyo, habari nyingi zaidi za kibiashara za China zinatangazwa kwenye vyombo vya nchi hiyo kuliko wakati mwingine wowote ule.

Tukio la Rais Xi Jinping wa China kutembelea Tanzania kabla ya Australia mara tu baada ya kutawazwa kuwa Rais kuliwafanya viongozi wa nchi hiyo kuitupia macho nchi yetu. Habari ile ilitangazwa kwenye vyombo vya huku na watu wakapata fursa ya kumfahamu Kikwete na Tanzania pia.

Katika mwaka ambao Xi alitembelea Tanzania, Rais Barack Obama naye alifanya ziara nchini kwetu. Ziara ile pia iliandikwa sana na vyombo vya Australia na maswali kuhusu Tanzania yakazidi. Umaarufu wa Kikwete kama kiongozi mashuhuri wa Afrika kwenye korido za kisiasa za Wa-Australia ulijengwa kwenye ziara hizi mbili za viongozi wa nchi kubwa na muhimu kwao.

Ndiyo maana, si ajabu kwamba Kikwete alifanikiwa kuonana na karibu viongozi wote wa juu wa taifa hilo, akiwamo Abbott mwenyewe ambaye kisiasa alitaka kuonyesha yuko karibu na viongozi wa Afrika, hususani Kikwete ambaye wananchi wa nchi hiyo wanamfahamu na kumheshimu.

Baada ya ufahamu huo kuhusu siasa za Australia, ngoja sasa nijielekeze kwenye mambo ambayo Tanzania itafaidika nayo moja kwa moja na ziara hii

Gesi na mafuta
Ripoti mbalimbali za kimataifa kwenye masuala ya mafuta na gesi zimeitaja Australia kama nchi kinara kwenye masuala ya uzalishaji wa gesi-maji (Liquefied Natural Gas-LNG). Huu ni usafirishaji wa gesi katika mfumo wa vimiminika.
Katika mwaka huu wa fedha (2015/2016), Serikali ya Tanzania imepanga kutumia takribani shilingi bilioni 12 kwa ajili ya maandalizi ya eneo utakakowekwa mradi wa LNG mkoani Lindi.

Mradi huo unatarajiwa kuiingizia Tanzania mabilioni ya shilingi mara utakapoanza kazi walau kwenye mwaka 2020. Kama nchi yetu inataka kujifunza kuhusu masuala ya gesi kwenye mfumo wa LNG, kuna sehemu chache za kujifunza zaidi ya Australia.
Ndiyo maana, katika safari yake hiyo, Kikwete alifuatana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Maendeleo ya Petroli (TPDC),

Dk. James Mataragio, ambaye ni mbobezi kwenye eneo hilo kwa ajili ya kuendesha mijadala na kufahamu zaidi kuhusu eneo hilo.
Ifahamike pia kwamba kumekuwepo na mikanganyiko mingi kuhusu suala la serikali kupitisha miswada miwili ya masuala ya gesi na mafuta bungeni ambayo ilisusiwa na wabunge wa Ukawa.

Baadhi ya wawekezaji nje ya nchi wanataka maelezo na ndiyo maana Mataragio alifuatana na Rais kwa ajili ya kueleza jamii ya wawekezaji kuhusu nini hasa kilichomo kwenye miswada hiyo na manufaa yote kwa pande zote mbili; yaani Watanzania na wawekezaji.

Kwenye safari hiyo, Rais Kikwete alifuatana pia na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Juliet Kairuki, ambaye alitumia nafasi hiyo kueleza kuhusu fursa za kiuwekezaji zilizopo nchini kwenye eneo hilo la gesi na mengine.

Ilikuwa muhimu kwa Tanzania kutumia umaarufu huu wa Kikwete kiuchumi kwenye nafasi hii. Australia inataka kuwekeza kwenye nchi zenye uongozi imara na kwa sababu ya heshima aliyonayo Jakaya kwao, ilibidi akina Kairuki waitumie nafasi hiyo vizuri.
Haifahamiki sana hapa nchini lakini ukweli ni kwamba Australia imeamua kupunguza misaada yake kwa nchi zinazoendelea. Hii ni kwa sababu yenyewe pia inapita katika kipindi kigumu kiuchumi.

Kwa mujibu wa magazeti na vyombo vingine vya habari nilivyovisoma nikiwa hapa, kuna vigezo vikubwa vitatu ambavyo nchi hiyo itavitumia kwa ajili ya kujua ni wapi watoe msaada na wapi wasitoe.

Mosi ni nchi ambazo zenyewe zinasaidia nchi nyingine. Ziko nchi ambazo ingawa zenyewe zilikuwa zikipokea msaada wa hapa na pale kutoka Australia, nazo zimekuwa zikitoa msaada kwa nchi nyingine. Mfano mzuri wa nchi hizo ni Indonesia.
Serikali ya Australia tayari imetangaza, kwa mfano, kwamba imepunguza msaada wake kwa nchi hiyo kutoka dola milioni 600 kwenye miaka ya nyuma hadi dola milioni 302 kwa mwaka huu wa fedha.

Pili ni kwa zile nchi ambazo zinaonyesha uchumi wake unakua vizuri. Nchi kama Tanzania zinaweza kuathirika na hali hii kwa sababu tunaonekana sasa kama nchi ambayo imeanza kujitegemea yenyewe.
Mfano ni kupungua kwa utegemezi wa wafadhili kwenye bajeti ya serikali ambapo kwa mwaka huu itakuwa ni tarakimu moja. Tatu imeamua kusaidia nchi zilizo jirani nayo. Bila shaka, hii ni kwa lengo la kuondokana na tatizo la wahamiaji haramu.

Australia inaisaidia nini Tanzania?
Kuna maeneo mengi lakini kubwa kuliko yote ni ufadhili kwenye masomo ya kiwango cha shahada ya kwanza na ile ya uzamivu. Katika miaka ya nyuma, Tanzania ilikuwa ikipata udhamini wa wanafunzi takribani 95 kila mwaka, 50 wa shahada ya kwanza na 45 wa shahada ya pili.

Kuna taarifa kwamba Australia itapunguza ufadhili huu kwa Tanzania katika sekta hii kwa sababu zilezile za kubana matumizi.
Ndiyo sababu, katika safari hii, Kikwete alifuatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Profesa Sifuni Mchome. Lengo hasa

lilikuwa ni kujadiliana na serikali kuhusu uamuzi huo na kwa kutazama mahitaji yetu, pengine Mchome angekuwa na mapendekezo mahususi kuhusu mahitaji ya kielimu ya Tanzania kwa sasa.

Kulikuwa na mazungumzo kuhusu masuala ya ufadhili katika maeneo ya Vyuo vya Ufundi mithili ya hivi vya VETA na maeneo mengine ambayo Mchome angeona yanafaa kwa mujibu wa mahitaji.

Ufadhili wa Australia kwenye elimu umekuwa msaada mkubwa kwa serikali na wakati nikiwa hapa, nilikutana na wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza na ya pili katika eneo la hifadhi na tafiti za wanyamapori.

Fursa za ufadhili kwa wanafunzi wa eneo kama hili zinaweza kupunguzwa katika wakati ambapo nchi yetu inakabiliwa na tatizo la ujangili na mauaji ya wanyama kama tembo.

Kwa aya moja tu, naweza kueleza safari ya Kikwete Australia ikiwa na malengo makuu matatu; kukuza wasifu wa Tanzania katika jumuiya ya kimataifa, kuvutia wawekezaji, kuiandaa nchi yetu na uchumi wa gesi na kuhakikisha wanafunzi wa Kitanzania wanapata fursa za kupata elimu ya juu katika nchi ambayo imekuwa ikifanya hivyo.

Hapo sijazungumzia kuhusu ile Shahada ya Heshima ya Uzamivu katika Sheria aliyotunukiwa na Chuo Kikuu cha Newcastle. Hiyo itasubiri siku nyingine katika mada nyingine.

- See more at: Raia Mwema - Kwa nini Kikwete alitembelea Australia?

 

Magimbi

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2011
Messages
1,361
Points
2,000

Magimbi

JF-Expert Member
Joined Oct 18, 2011
1,361 2,000
Umehesabu na hasara tunazopata kwa ziara za aina hii..unajua kuwa sio serikali iliyomualika. Na ameomba kuonana tu na hao viongozi sio wao wameomba. Amealikwa na General mstaafu na nguli wa Commonwealth..tuna machangamoto kibao safari zingine zaweza wakilishwa tu not flying over our expenses...
 

Forum statistics

Threads 1,392,245
Members 528,573
Posts 34,102,722
Top