Kwanini Kikosi Kazi na siyo Rasimu ya Warioba, Serikali inaiogopa nini Rasimu ya Warioba?

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,400
4,073
Wadau bado Najiuliza kwanini Serikali imetumia kodi za Wananchi kuunda kikosi kazi kufanya kazi ambayo ilikwishafanywa na tume ya Warioba kwa gharama?

Isitoshe tume ya Warioba ilikusanya maoni na mapendekezo ya wananchi wengi nchi nzima tofauti na hiki kikosi kazi ambacho kimekusanya maoni ya Wakubwa na Watu Wachache Wakati Suala la katiba mpya ni la wananchi.

Mikutano ya hadhara ni la Wananchi na tume huru ni ya Wananchi lakini kikosi kazi kimewakwepa wananchi walio Wengi.

Serikali isidhani wananchi tumesahau kuwa fedha zilizotumika kuwalipa wabunge wa bunge la katiba ni kodi za Wananchi Masikini, lakini Pamoja na Kulipwa katiba mpya ya wananchi haikuweza kupatikana na hilo ni deni.

Serikali tumieni rasimu ya Wariona na siyo Maoni na Mapendejezo ya Wachache ya kikosi kazi.
 
Kuna ujanja ujanja unafanyika hapa, watu wanatumia kila hila kulinda madaraka na maslahi binafsi.......hawajali maslahi ya nchi na wananchi.
 
Back
Top Bottom