Kwanini Kigamboni haipo kwenye DMDP?

Mkwanzania

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,123
4,254
Nimekuwa nikifuatilia huu mradi wa Dar es Salaam Metropolitan Development Project kwenye Manispaa za Ilala, Temeke, Kinondoni (ikiwemo na Ubungo). Nimeshuhudia miradi mbalimbali ya miundombinu ya Barabara na Maendeleo ya Makazi kwenye hizi Manispaa na itatia moyo sana, zinapendeza kwelikweli.

Baada ya Serikali kuachana na mpango wa kujenga mji mpya wa Kigamboni, tulitegemea serikali ingewekeza katika kujenga miundombinu ya wilaya hii changa inayokuwa kwa kasi. Hii ingefanyika ili kuvutia watu kwenda kuishi Kigamboni sehemu ambapo kuna maeneo ya kutosha na upepo mzuri wa baharini. Lakini cha kushangaza Manispaa ya Kigamboni imetupwa kando hasa kwenye miradi ya uendelezaji miundombinu, mbaya zaidi imtengwa na miradi ya jumla kama huu wa DMDP kwa sababu ambazo sisi wakazi wa Kigamboni hatuzijui.

Kama Serikali imeshindwa kuendeleza mji mpya wa Kigamboni (which is shame anyways) basi ni kwanini basi isijitahidi hata kuboresha miundombinu ya wilaya hii? Lakini pamoja na hayo, hiyo miundombinu kidogo iliyopo bado tunalipia. Daraja unalipa, Ferry unalipa. Wakazi wa Kigamboni wameikosea nini Serikali? Serikali ina mpango gani na Kigamboni? Nayo imeachwa ijichafukie alafu baadae tuanze kuvunja?


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom