Kwanini kesi zote dhidi ya mashirika na taasisi za serikali zisiendeshwe na mawakili wa serikali?

nyundo2017

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
1,439
859
Habari wadau

Nimeona kwa mawazo yangu hakuna maana ya kesi za jinai au madai dhidi ya mashirika na taasisi za serikali ziendeshwe na wanasheria wa mashika na taasisi hizo kwani wamekuwa wakitengeneza mazingira ya kupiga hela.

Kama wanasheria wa serikali wataendesha kesi hizo basi ni wazi wanasheria wa mashirika na taasisi wa serikali wabaki tu kuwa washauri na wasimamizi wa maswala ya sheria kwani wamekuwa wakichelewesha kesi au kuwaonea watu ambao hawataendana nao kmakubaliano

Nawasilisha
 
Kuna conflict of interest maana huwezi endesha kesi upande wa mtu aliekuajiri kwa mawakili hautakua impartial bali itakua kesi yako personally na sio ya mteja
 
Kuna conflict of interest maana huwezi endesha kesi upande wa mtu aliekuajiri kwa mawakili hautakua impartial bali itakua kesi yako personally na sio ya mteja
Kwani unapopewa instructions na mteja unakuwa sio mwajiriwa wake?
 
Bwana sajo, katika mazingira hayo huwi mwajiri wake yaani 'employer' ila utakuwa mteja wake kwa tafsiri ya 'client'. Hakuna uhusiano wa mwajiri na mwajiriwa mwa hicho ulichosema bali ni mtoa huduma kwa maana ya service provider and client.
 
Mashirika yatapata hasara sana. Mawakili wa serikali hawapo serious kabisa. Hawafanyi maandalizi yoyote na ni rahis sana kuwa-corrupt.

Nafuu hata polisi km ni jinai kuliko hawa mawakili wa serikali.
 
Back
Top Bottom