Kwanini kazi nyingi za kijasusi ni za kifamilia (Family-friendly)?

Ofcourse familia zinamchango wake lakini ukiwa hodari kwenye eneo fulani mbona easy tu..sema "Wengi" wetu tunafeli kwenye vetting pale..na ukute ndio uko mjeuri jeuri "unatupiwa tu' Extendend Vetting Process mae..unasaga lami bila kujua..2 yrs imenitesa!
You have an interesting case ila tuishie hapa hapa. You know they read you in here.
 
KITU KIKITUMIKA VIZURI NA KWA HAKI NI SUALA JEMA SANA ILA UDANGANYIFU UKIWEPO BASI NI DHAMBI.
Binafsi naheshimu ujasusi kwa sababu ni taaluma ya kale sana hata kwenye maandiko tuliona MUNGU alivotumia wapelelezi kuichunguza nchi ya kaanani wakati Musa na baadae Yoshua akiwatoa wana wa Israeli utumwani Misri (Hesabu 13:1, Yoshua 2:1-24).

Tatizo kubwa ni uongo huo ndio mkosi ila haki ikitendeka mkuu mambo hupendeza sana.
What is your point mkuu ? Hebu weka wazi haumaanishi sijasoma uzi wako la, nimesoma lakini comments zako hazi correlate na post yako ya mwanzo. Kwa maneno machache state your case
 
What is your point mkuu ? Hebu weka wazi haumaanishi sijasoma uzi wako la, nimesoma lakini comments zako hazi correlate na post yako ya mwanzo. Kwa maneno machache state your case
Lengo ni kuwasaidia watu mkuu wasipotee.
 
Ofcourse familia zinamchango wake lakini ukiwa hodari kwenye eneo fulani mbona easy tu..sema "Wengi" wetu tunafeli kwenye vetting pale..na ukute ndio uko mjeuri jeuri "unatupiwa tu' Extendend Vetting Process mae..unasaga lami bila kujua..2 yrs imenitesa!
Fafanua mkuu na wengine tupate somo
 
Bila kung'ata ng'ata Maneno.
Baba yangu mzazi, anajua fika dada zaake ni wataalamu wa nguvu za giza, za uharibifu ambazo zipo dhidi ya Mama, na mimi ndiyo proud ya Mama, but ana sisitiza niende kijijini kuwatembelea bila kinga ya tahadhari, wakati mimi nimepasua sana kipindi kuliko watoto- failure wa hao dada zake.
Duuu! nikamstukia!

Mbaya sana huyu dingi hakupenda nipate kazi fulani hivi nzuri sana, yenye heshima ktk jamii, badala yake anataka niwe simple mwalimu, tena kwa kuniponda sana, kuwa siwezi mambo makubwa.

So nikajishusha kama bonge la bwege kweli, nikamuibukia na bonge la fix, wakati mwingine ikibidi Danganya! unafiki unatumika pia, kufikia malengo, baba si akajaa! akanipa mapene/hela ya kutosha. nikajichimbia chaka kimya miaka takribani 3 nabukua chuo fulani hivi ughaibuni.

siku isokuwa tarehe nikamuibukia na kazi ile ile, aloniwekea kauzibe, akaomba joint venture, nikampa nusu, nusu ilobaki nikawa nayo mwenyewe!, But nikajifanya hamnazo kiaina.

daaah! mleta mada bana very good!
 
Usilolijua ni kama usiku wa giza. Asante sana Mchungaji umetukumbusha kitu kizuri sana" No Trust No Body"
 
Katika maisha ya binadamu ni watu wachache sana tena ambao ni vichaa, matahira au waliologwa ndio wanaoweza kwenda kinyume na wazazi wao au kwa kwa lugha rahisi kuwasaliti wazazi wao au kuwa ignore completely.

Ni jambo gumu sana kwa binadamu kulifanya kwani watoto huwapenda sana wazazi wao na ni kweli ni watu muhimu sana kwao. Wamewalea na kuwafikisha hapo walipo.

Sasa wazee wa kazi (KITENGO) wanachukulia fursa hii adimu kupata credible asset au watu wa kuaminika.

Ni rahisi kuwaamini bila mashaka.

Wazazi wao nao wanakua na details zao ndani ya hizo agency hivyo mambo yanakua mbwito mbwito.

Hii njia imewamaliza watu wengi sana na kwa bahati mbaya hawajitambui. Kwa hiyo wanaliwa kiulaini mno kwa kuwa brainwashed na wazazi wao wenyewe.

Kwa hili nawalaumu sana wazazi na mwisho wa siku malipo ni hapa hapa duniani tuu na motoni utalipa, Nalaumu hili iwapo kijana/mtoto ataingizwa chaka kwa kupitia wazazi wake.

Watoto wengine unakuta walishapangiwa siku nyingi sana na wazazi wao kuuawa kwa malipo fulani/kuuzwa.

Most intelligence agencies zote za huu ulimwengu hufanya hivyo, akina CIA, KGB, Mossad and so on…

Unaweza shangaa taifa kubwa kama marekani/USA lenye maadui kila kuona ya ulimwengu hadi kuzimu kwanini hawaangushwi/hawaadhibiwi? Lina kila aina ya races/jamii zote za ulimwengu so kutengeneza ma agent wa covert operation ni simple sana lakini kwanini hili linakua gumu?

Jibu ni fupi tuu hilo taifa lina watu wanalishikilia. Nafasi nyeti hawapewi watu tuu from no where.

Wapo watu wa kuaminika toka vizazi na vizazi ambao taarifa zao hazipo popote wala hawaongelewi kabisa hawa ndio roho ya hilo taifa.

Hizo nafasi nyingine sio deep na ikitoke shida mhusika anadhibitiwa mara moja.

Mataifa yanaendeshwa kiutaalamu sana. Hata wale wanaolalamika huku kwamba wana vipaji lakini hawapewi hizo nafasi wajue tuu wanajulikana vizuri sana ila hawafai kwani ni threat na pengine background ya wazazi wao ni mbaya pengine ni defector au wapinzani au walidhulumia. Kwa hiyo kupunguza visasi na matatizo yatakayotokea wanakua omitted mapema sana.

NB:Ndugu zangu kwa upendo wangu kwenu nawaombeni sana msimuamini mtu yeyote yule chini ya jua ila ishini na wato wote vizuri hata wabaya wenu. Binadamu ni dhaifu sana na niwaambieni tuu hakuna mtu atakaeweza kutoa uhai wake kwa watu wengine na wanaogopa onyo. Kaeni mbali sana na marafiki zenu wa karibu (damu damu) na ndugu zenu wa kuzaliwa. Kaeni mbali sana na girl/boy friend, wachumba, masela/washkaji, wake na waume zenu. Hao ni target/silaha ya maangamizi na njia ya kufikia target(Mlengwa wao). Watu wengi wameuawa na watu wao wa karibu kama Rais wa Burkina-faso marehemu Thomas Sankara (Aliuawa na rafiki/mlinzi wake mkuuu Blaise Compaore aliekuja kuwa Rais baada ya yeye, alipoulizwa alisema makomandoo wa ufaransa ndio waliohusika), Laurent Kabila uyu alikua rais wa Congo DRC aliuwawa na bodigadi wake, Fidel Castrol mkewe alitumiwa na CIA kumuwekea sumu kwenye kinywaji lakini Fidel alishtukia mchezo hivyo akakishinda kifo na wengineo.

Chunguzeni kwa kina tuu hata kwenye /mitaa/vijiji/miji/familia zenu vifo vya kitata/kishirikina/kichawi wahusika wakuu ni watu wa karibu hivyo ni vyema kuokoka mapema kuwa na kinga ya Mungu kwa maana maadui ni wengi na vita mipiganavyo sio vya kimwili bali vya kiroho. Mambo mengi huanzia ulimwengu wa kiroho ila sasa kama huna uelewa na haya mambo ni vyema uanze kuutafuta utukufu wa Mungu mapema sana. Tafuta wachungaji kwenu, mafundisho google, youtube, facebook, instagram hata hapa lipo jukwaa la dini/imani upate kujifunza.

It’s dangerous game to trust anyone even your lovely parents/children. Usiwe na aibu ya kuwatupilia mbali watu wako wa karibu eti kisa watakuona vibaya. That is wrong… ndipo watu wengi wanapoangukia kwa hofu ya kukwepa lawama. Ukiona shida sana ita mtu wako huyo wa karibu mwambie waogopa mabaya yatakayomkumba kwa kuwa karibu na wewe. Hata maandiko yanasema amuaminiye binadamu amelaaniwa.

Bora lawama kuliko fedhea/kifo”

Ni muhimu sana kuisikiliza sauti ya MUNGU kuliko binadamu, Na tatizo la binadamu hawaamini bila kushuhudia ila naama mhusika ukipuuzia sauti moja au mbili halafu ukaona madhara basi utajifunza kitu na utamuamini MUNGU siku zote za maisha yako.

Kua na positive mind. TRUST GOD ONLY!


Trust but verify - Ronald Reagan



Good luck! Mungu awe nanyi, wakuu.

Mika 7:5-6
ahsante
 
Back
Top Bottom