Kwanini kati historia mkoloni hakuwahi kufanikiwa kuwatawala wamasai kama makabila mengine

Nimeona niulize swali hiyo kwenye ukurasa huu wa Historia pengine kuna watu walionizidi umri kama kina mzee Mohamed Said wanaweza kuchangia

..Wamasai walikuwa na bahati kwamba Mkoloni hakutamani chochote kile ktk jamii yao.

..hiyo ndiyo sababu iliyopelekea kusiwe na maingiliano au migogoro kati ya Mkoloni na Mmasaai.

..vilevile Mkoloni alikuwa anatawala kwa mbinu tofauti kati ya jamii moja na nyingine.

..kuna maeneo Mkoloni aliona atapata faida kubwa zaidi akitawala kwa mkono wa chuma, na kuna maeneo aliona atafaidika kwa kuepuka mabavu.

..kuna maeneo ambayo Mkoloni alichukua manamba, kuna maeneo aliacha wananchi walime yeye akakusanya kodi na kununua mazao kwa bei kiduchu, na kuna maeneo ali-recruit askari, etc etc. Wote huo ulikuwa ni ukoloni lakini kwa mbinu tofauti. Na legacy ya mbinu za kikoloni ktk maeneo husika bado iko mpaka leo tunavyozungumza.

NB:

..ila naweka angalizo kwamba ipo ARDHI ya Wamaasai ilichukuliwa na mkoloni kwa upande wa Tanganyika na Kenya.
 
Nadhani ni kwasababu wamasai walithamini sana utamaduni wao,
Njia rahisi ya kumtawala mtu ni kumharibia utamaduni wake
 
Nimeona niulize swali hiyo kwenye ukurasa huu wa Historia pengine kuna watu walionizidi umri kama kina mzee Mohamed Said wanaweza kuchangia

Katika somo la historia nilifundishwa kuwa moja ya makabila ambayo hayakutawaliwa lilikuwa ni la wamasai. Sababu kubwa tuliyopewa ni utamaduni ana staili yao ya maisha ya upinzani na kuhamahama.

Sio wakoloni tu ambao walishindwa kuwatawala. Hata serikali za mwanzo zilishindwa kuwabadilisha staili yao ya maisha. Kwa mfano mpaka wa Kenya na Tanzania kwao ulikuwa haupo.
 
Bila shaka unamaanisha;

Kwa nini jamii ya wamasai hawakukamatwa,kuuzwa,kasafirishwa na kutumikishwa kwenye shughuli za uzalishaji mali na wakoloni kama makabila mengine?

Wamasai wa Kenya wako hapa,

Kama Tanganyika ilitawaliwa na wakoloni means makabila yote ndani yake yalikuwa chini ya mkoloni
 
Nimeona niulize swali hiyo kwenye ukurasa huu wa Historia pengine kuna watu walionizidi umri kama kina mzee Mohamed Said wanaweza kuchangia
Sikweli kwamba wamasai hawakutawaliwa!! Iko hivi wakoloni baada ya kuligawana bara la africa 1885, Koloni la Ujerumani Afrika mashariki (leo hii Rwanda, Burundi na Tanzania bara) likawa chini ya kampuni la kijerumani la Afrika mashariki(GEACO) mpka 1890. Sasa kipind hiki yaan 1885-1890s kilikuwa kipindi cha kusimika utawala wa kikoloni, hapa ndipo maeneo mengi yalipinga kutawaliwa, maana jamii hizo ziliamin kuwa zitapoteza mali, ardhi, uongozi(kwa wafalme), na umaarufu ktk jamii. Lakin kuna jamii ambazo ilikuw rahisi kuzitawala bila mapigano hasa jamii za wafugaji (pastoral societies) mfano maasai na wawindaji(hunters) mfano hadzabe. Maana wakoloni hawakutumia nguvu nyingi sehemu ya jamii ambazo hazikuonyesha upinzani. Ndoo maana historia inaandika sana maeneo ambayo jamii zilipigana vikali mfano, kina mkwawa, mangi meli, mangi sina, mareale, abushiri, isike, machemba, kinjekitile, mazengo, na wengineo wengi. Kiufupi nikwamba Maeneo ambapo wakoloni walipata upinzani mkali ndio yameandikwa zaidi ila jamii zote zilizokuwa kwenye koloni la ujerumani Afrika Mashariki (Leo hii Rwanda, Burundi na Tanzania bara) zilitawaliwa.
 
Nimeona niulize swali hiyo kwenye ukurasa huu wa Historia pengine kuna watu walionizidi umri kama kina mzee Mohamed Said wanaweza kuchangia

Hujui historia ya ukoloni kwa wamasai huko Kenya. Wao na Wakikuyu ndio makabila yaliyopoteza ardhi kubwa yenye rutuba kwa ma-settler wa kiingereza. Bado kiasi kikubwa cha ardhi hiyo kiko mikononi mwa wazungu mpaka leo. Kumbuka kwamba, hata mji wa Nairobi ulipo ni ardhi ya wamasai.
 
Nimeona niulize swali hiyo kwenye ukurasa huu wa Historia pengine kuna watu walionizidi umri kama kina mzee Mohamed Said wanaweza kuchangia
Mkuu

Hapo sio kweli, wamasai ndio watu dhaifu sana kuhusiana na ukoloni na ndio wanaoendekeza hadi leo, wanawaabudu kupita kiasi chunguza utaamini na kubadilisha tango pori unalolazimisha kila mmoja akuamini. Chukua mfano mdogo tafuta mmasai awe morani, olegwanani au mzee kisha wakutanishe wa wazungu wowote unaofikiri huwa ni katili kama wajerumani, wabeligiji, wataliano nk halafu chukua kabila jingine na uwakutanishe na wazungu jinsi hiyo atakayebaki na urafiki naye ni masai pekee kwa sababu wanalaghaika sana wanapoambiwa utamaduni umewafurahisha (impress) . Lakini wengine wanapokatisha uhusiano huo ni kwa sababu ya kutoa viashia vya kuwadharau na kujiona wenyewe ndio tegemeo kitu ambacho hawawezi kukubali
 
Mashuka wanayovaa Ni utamaduni wa wazungu
Mkuu, kila siku uwa najiuliza hilo swali.

Inakuaje tunasema/wanasema kuvaa mashuka ni utamaduni wa Kimasai/wamasai?

Sijawai kusikia kuna kiwanda kilichokua/kilichopo chini ya Wamasai ambacho kinatengeneza hayo mashuka.

Na kama hawatengenezi hayo mashuka inamaanisha wanayanunua toka nchi/sehemu nje ya Wamasai, hivyo sioni kwanini kuvaa mashuka tuseme ni utamaduni wao.
 
Huo utamaduni wameiga tu,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom