Kwanini kampuni nyingi zinapoteza nguvu ya kiushindani (competitive advantage)?

Jun 21, 2021
5
10
1639143301721.png

Pindi kampuni inapopoteza nguvu ya kiushindani, faida pia hushuka (profitability falls) japo si lazima Kampuni kufa. Kuna sababu nyingi zimekuwa zikielezwa kama chanzo kwa kampuni kupoteza nguvu/uwezo wake wa kiushindani sokoni. Lakini sababu kuu zinazosababisha hali hii ni kama ifuatavyo;

Inertia: sipati tafsiri sahihi kwa neno hili kwa lugha yetu ya Kiswahili, lakini ninachomaanisha hapa ni kwamba, mazingira katika biashara yanabadilika kila kukicha, kwa maana hiyo ili uweze kudumu sokoni, ni lazima nawe kama Kampuni uwe tayari kubadilika. Inertia inakuja pindi ambapo mazingira katika "industry" yako yamebadilika kutokana na kukua kwa teknolojia n.k, lakini wewe hutaki kubadilika. Kwa mfano; kipindi cha nyuma (kabla ya ujio wa simu janja "smart phones") biashara ya "Internet Cafe" lilikuwa na faida nzuri, lakini ujio wa "smart phone" and its associates kwa kiasi kikubwa umepunguza faida katiak biashara hili, hivyo kuna baadhi ya watoa huduma walibadilika kuendana na mabadiliko, lakini wengine wameendelea kuwepo, waliopo sasa katika biashara hii hawana tena nguvu ya kiushindani. Hali hii pia iliikumba IBM katika soko la "Mainframe Computers" pindi "Personal Computers" zilipoingia

Prior Strategic Commitment: Kampuni inapowekeza kiasi kikubwa cha rasilimali zake katika kitengo cha uzalishaji (production), usambazaji (distribution) n.k huwa na kitu tunaita "Strategic Commitment" yaani kujidhatiti na kujitoa kimkakati. Sasa pindi yanapotokea mabadiliko katika "industry", huiwia Kampuni ugumu kubadilika, kwa sababu mabadiliko ni lazima yaendane na ubadilishaji wa mifumo katika uzalishaji, usambazaji n.k ambapo kimsingi ni gharama zingine tena Kampuni itapaswa kuingia

Icarus Paradox: Hii dhana inatokana na hekaya ya Kigiriki ambayo inaeleza kwamba Icarus aliwekewa mabawa mawili na na Baba yake yaliyomuwezesha kupaa kiurahisi. Kwa sababu alikuwa na uwezo wa kupaa kiurahisi, hivyo aliweza kupaa mpaka akalikaribia jua lilounguza nta iliyoshikilia mbawa yake na hivyo kumfanya adondoke na kupoteza maisha. Kuna kipindi Kampuni inaweza kuwa inafanya vizuri sokoni kiasi cha kupumbaza "Management" kutokuona hatari ya mabadiliko inayoweza kutokea mbeleni (Hii ni kwa sababu mabadiliko katika biashara hayaepukiki) , kwa maana hiyo "Management" itashindwa kuwa na Mkakati wa kukabiliana na mabadiliko, hivyo pindi mabadiliko yanapotokea huikumba Kampuni na kupoteza nguvu yake ya Kiushindani.

NINI KIFANYIKE ILI KUEPUKA KUPOTEZA NGUVU YA KIUSHINDANI

Kampuni inapaswa kufanya yafuatayo:

Kuweka Mkazo kwenye Nguzo zinazojenga Nguvu ya Kiushindani: Nguzo zinazojenga nguvu ya Kiushindani hujumuisha ubora wa bidhaa zako/huduma zako (quality of your product/service), ubunifu (innovation), ufanisi katika utoaji wa huduma zako (efficiency) and mwitikio mzuri kwa wateja (responsiveness to your customers)

Kuwa na utaratibu wa kujifunza ndani ya Kampuni yako (Institute Continuous Learning) Kama tulivyoainisha hapo awali; mabadiliko siku zote yapo, hivyo kuwa na utaratibu wa kujifunza JUU na KUTOKANA na mabadiliko yanayotokea katika "industry" yako. Kampuni zenye mafanikio katika "Industries" mbalimbali ni zile zinazojifunza na kuja na bunifu mbalimbali katika uzalishaji, usambazaji, masoko n.k

Tafuta "practice" iliyo bora katika "Industry" na kuifanya kama kigezo/alama ya kujipima. "Good Practice" inaweza kuwa kwenye eneo lolote lile la mnyororo wa thamani (Chain Value) mf; usambazaji, uzalishaji n.k

Usiogope na nenda na mabadiliko pasina kujali kiasi gani cha rasilimali umewekeza katika Kampuni yako.

AHSANTE

HEINZ Consulting
Consultancy, Project Management, Strategy, Fundraising & Training
PC 12119
Email: heinzconsultancy@gmail.com
Dar es Salaam
 
Back
Top Bottom