Kwanini kamati ya Mwinyi inamlazimisha Sitta kumuomba msamaha Lowassa?

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2008
2,268
333
Mambo bado mazito Kamati ya Mwinyi

Na Mwandishi wetu
21st February 2010

headline_bullet.jpg
Ilimwita Spika Sitta amwombe radhi Edward Lowassa

headline_bullet.jpg
Kwa kuchelewesha kufunga mjadala wa Richmond

headline_bullet.jpg
Kuruhusu makombora kuelekezwa kwa Lowassa na mawaziri

headline_bullet.jpg
Spika akataa kuomba radhi ili kutunza hadhi ya wabunge


Mwinyis(2).jpg

Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi

Kamati iliyoundwa na Halmashauri Kuu (NEC), ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka jana kwa ajili ya kutafuta chanzo cha uhasama na chuki baina ya wabunge wa chama hicho huenda isifanikiwe kupatanisha makambi mawili yanayotuhumiana.

Habari za ndani zinasema kuwa awali kamati hiyo ambayo inaongozwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, ilimwita aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Spika wa Bunge, Samuel Sitta, na kumtaka Spika Sitta kumwomba radhi Lowassa juu ya sakata la Richmond.

Nia ya Sitta kutakiwa kuomba radhi ni kutokana na kuchelewa kufunga mjadala wa Richmond na kuruhusu makombora kuelekezwa waziwazi kwa Lowassa na mawaziri wengine waliohusishwa na kashfa ya zabuni tata ya kufua umeme wa dharura ambayo kampuni ya Richmond ilipewa.

Taarifa zaidi zinasema kuwa Spika Sitta alikataa kuomba radhi kutokana na kashfa hiyo na kuhoji sababu za kufanya hivyo badala ya Serikali yenyewe kuwachukulia hatua watumishi wake waliolisababishia taifa hasara kutokana na kampuni `tata' ya Richmond.

Chanzo chetu kimedai kuwa, Sitta aliigomea kamati ya Mwinyi na kuhoji wananchi watalielewaje Bunge kuhusiana na sakata zima iwapo Lowassa na wenzake wangesafishwa bila kuwataja na kuwakemea wahusika wa Richmond.

"Tumejiuliza Bunge litawaeleza nini Watanzania ambao waliumizwa na Richmond, ziko wapi milioni 152 zilizokuwa zikilipwa kwa Richmond kila siku kama ‘capacity charge' au nani alihusika…Sitta ameitaka kamati hiyo kujibu maswali hayo na mengine mengi ambayo wananchi wanahoji kuhusiana na Richmond kabla hajaomba radhi," kilisema chanzo chetu.

Aidha, imedaiwa kuwa kitendo cha Spika Sitta kukataa kuomba radhi kimeendelea kuiumiza kamati ya Mwinyi pamoja na chama kwa kuwa sakata la Richmond ndio chanzo cha mpasuko ndani ya chama hicho.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema wiki hii baada ya kumalizika kwa mkutano wa NEC mjini Dodoma, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa, alisema kazi iliyobakia ni kuwakutanisha vinara wa makundi mawili yanayosuguana yaani Lowassa na Sitta. Hata hivyo, alisema mazungumzo ya usuluhisho baina ya makundi hayo mawili yanaendelea vizuri na kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kupata muafaka.

Msekwa ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya Mwinyi, alisema mvutano ya makundi hayo ulianza baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya Richmond na kueleza kuwa walichobaini ni wabunge hao kulinda nafasi zao majimboni kwa kuwa wabunge wamekuwa wakituhumiana kwa kila mmoja kudai kuwa kundi moja linataka kuliong'oa lingine jimboni.

Msekwa alisema hawana nia ya kukemea wala kumvua mwanachama wake yeyote uanachama na badala yake kazi waliyonayo ni kujenga umoja na mshikamano ndani ya chama.

Huku akinukuu kifungu cha Biblia na Quran, alionya kuwa kundi ambalo halitakubali kupatanishwa na lingine, 'litaandamwa'.

Tayari Kamati ya Mwinyi imeongezewa mwezi mmoja ili iweze kuyakutanisha makundi hayo mawili na Msekwa aliahidi kuwasilisha ripoti ya kazi hiyo kwenye kikao cha Kamati Kuu kitakachofanyika mwishoni mwa Machi, mwaka huu.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Lakini mwishini akafyata mkia na akafunga mjadala huo na kuizika issue ya Rich-mond
 
Kwa sababu Kamati Teule ya Bunge ilimwonea sana Lowassa ndio maana maazimio ya Bunge kuhusu Richmond hayajazaa matunda hivyo kupelekea kufungwa rasmi kwa mjadala huo Bungeni!
 
Haya mambo yasiokwisha yanatia kichefuchefu hata kuyaangalia. Tuangalie mambo mengine sasa. Tunapoteza muda mrefu kudeal na personalities tunasahau hata mambo ya msingi kabisa ya maendeleo ya nchi yetu.
 
Haya mambo yasiokwisha yanatia kichefuchefu hata kuyaangalia. Tuangalie mambo mengine sasa. Tunapoteza muda mrefu kudeal na personalities tunasahau hata mambo ya msingi kabisa ya maendeleo ya nchi yetu.

Mambo "ya msingi kabisa ya maendeleo ya nchi yetu" yamekuwa 'personalized' ndugu yangu hivyo huwezi kuzikimbia hizi 'personalities' zilizoshika hatamu za nchi!
 
Mambo "ya msingi kabisa ya maendeleo ya nchi yetu" yamekuwa 'personalized' ndugu yangu hivyo huwezi kuzikimbia hizi 'personalities' zilizoshika hatamu za nchi!
Well, enzi zile tulikuwa tunaimba chama kushika hatamu kuongoza nchi. Kumbe siku hizi ni vigogo kushika hatamu kuongoza nchi!
 
usilolijua ni sawa na usiku wa giza, sidhani kama kuna mgogoro hapo ila ni njama ya CCM kutufanya waTz tusiwe na mawazo ya kudai maendeleo
 
Kwa mda sasa sina imanin na credibility ya hicho chanzo cha habari, it has a purpose to serve............
 
Haya mambo ya Lowasa na Sitta hayana maana tena kwa watanzania,mwaka mzima Richmond lakini mwisho wake ni huo wa kufunga mjadala bila ya wahusika kuwajibishwa,mimi nina sema mtendaji mkuu wa serikali awe na msimamo na ache usanii na atimize wajibu wake.

Katika kuongoza nchi haitakiwi undungunaizesheni(Nepotism na favouratism) hii inaadhiri katka kutoa maamuzi ya msingi.Lowasa alivurunda yeye akae mbali na watanzania hawezi kujiosha.

Na tunamshauri Mzee Mwinyi atumie hekima kusuluhisha hili na sio kumladhimisha Sitta kumuomba msamaha Lowasa.

Kwa sisi ambao tumesomea kozi za utatuzi wa migogoro- Msuluhishi hatakiwa kuegemea upande wowot.ni lazima awe neural - hii kamati haitafikia maamuzi yenye mafanikio.

Na Sitta akizubaa hiki kitakuwa ni kitanzi kwake,maana Lowasa ni rafiki mtendaji mkuu - hapa kazi ipo.Lakini Mungu akiwepo upande wetu tutamhofia na ni?

Lazima haki itapatikana Tanzania - Tunaiombea nchi dhidi ya hawa wavurugaji na wafujaji wa mali za watanzania

Elisante Yona
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom