Kwanini JWTZ isipewe kazi ya kupigana na vita ya adui njaa?

Mtazamaji

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
5,937
1,437
Nimekua nikjiuliza na kutafakari maswali mengi na kutafakari baadhi ya majibu yanayoweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Nimetafaaki utendaji wa keshi letu la JWTZ na namna ambavyo kama wenye maamuzi, maono na washauri wakijaribu tunaweza kushinda japo vita moja kama nyingine zimekuwa ni ngumu.

Kwa uelewa wangu mdogo na uchambuzi wa haraka sioni kama tanzania ina tishio halisi na kubwa la adui atakayetumia silaha within 10 or 15 yrs to come .

Kwa mtazamo huu nadahani ingekuwa vizuri JWTZ ikawa na mtazamo kiamaendeleeo zaidi . na kama kazi kubwa ya jeshi ni vita basi amiri jeshi mkuu atangaze kuwa adui anayetakiwa kupigwa ni NJAA.

JWTZ likiungana vizuri na wanavijiji katika nagzi za wilaya na vijiji linaweza kua chanzo ka kutokomeza huyu adui. wakiwa na mashamba ya mifano na matreka ambayo wanaweza kuwakodisha wanavijiji huyu adui atakuwa historia

Kuna watu watasema ipo JKT lakini ninepnda hii Vita ipewe JWTZ na kama JKT basi tunaomba tuwe wabunifu. Sio kwa sabau Jeshi la USA hawalimi basi tuseme Sio kazi ya JWTZ.

Labda vita ya NJAA inaweza kuwa rahis kuliko vita ya UFISADI na zaidi ya hapo itafanya JWTZ kuwa ya wanachi zaidi kuliko kohofiwa .
 
Kuiba Vocha za Bilioni 23 za pembejeo muibe nyinyi halafu mnataka kuwatupia wanajeshi kazi kwa sababu ya UFISADI WENU?

you are hitting the wrong target.
 
Waache kazi ya kulinda nchi waende kulima? You must be kidding me! Na nyie wakulima mtafanya nini? Kama mmeshindwa kuwathibiti mafisadi shauri yenu.
 
mtazamaji idea yako ni nzuri il inahitji mambo mengi ya kuyaangalia, but it is possible, au unaweza kusema liwe jeshi la production, katika dunia ya sasa ambayo dunia ni kama kijiji kazi ya wanajeshi inabidi ibadilishwe sana, japokuwa their main purpose inabidi ibaki pale pale.

majeshi ya wenzetu yanatumika kufanya research, na kuzalisha mali, japo si lazima iwe kilimo.
 
mipaka walinde saa ngapi?, mafunzo wafanye saa ngapi?. Una dhani adui anatoa toa taarifa?. Fikiri kabla ya kusema!
 
"Kwa uelewa wangu mdogo na uchambuzi wa haraka sioni kama tanzania ina tishio halisi na kubwa la adui atakayetumia silaha within 10 or 15 yrs to come ."

Mkuu jeshi linakaa stand by kuwa na adui or not. Je akitokea ghafla? Au unadhani adui ana chukua muda kuji tokeza. Pia adui ana tumia opportunities. Akiona jeshi lime lala tu basi ana ibuka.

"Kwa mtazamo huu nadahani ingekuwa vizuri JWTZ ikawa na mtazamo kiamaendeleeo zaidi . na kama kazi kubwa ya jeshi ni vita basi amiri jeshi mkuu atangaze kuwa adui anayetakiwa kupigwa ni NJAA."

Hiyo si kazi ya jeshi. Dalili ya nchi kuendeshwa vizuri ni good organization...meaning kila taasisi na kazi zake. Hi si kazi ya jeshi. Unless kama unashauri jeshi livunjwe kabisa ianzishwe kitu badala yake itakayo deal na mambo ya njaa.
 
Tuache ku-crame kwa nguvu na kwa kujiamini

1. Jeshi linapaswa kufanya zaida na mbalisana kuliko wengine

Internet tunayotumia imekuwa invented jeshini (usa) mwaka 1960!!

GPS imekuwa invented jeshini,!

Digital photography tunazotumia leo hii!

Research nyingi sana za uhandisi zinafanywa jeshini,

Infact ilibidi US Army copr os Engineers waanzishe research bureau inayojumuisha na raia, na hizi ni kazi wanazofanya;

Planning, designing, building, and operating locks and dams. Other civil engineering projects include;

flood control, beach nourishment, and dredging for waterway navigation.

Design and construction of flood protection systems through various federal mandates .

Design and construction management of military facilities for the Army and Air Force and other Defense and Federal agencies.

Ni nadra sana kukuta kitu cha uhandisi hasa wa ujenzi kuwa hakijaanzia jeshini.

Hii sio USA tu, Germany, Soviet, Israel wote majeshi yao yanapiga kazi kwenda kwa mbele, na sio kufyeka nyasi Lugalo!. USA wamenza hii ishu tangu 1775!

Nashangaa sana mtu anaposema kazi ya jeshi ni kulinda mipaka eti hatujui adui anakuja lini! wa kuipiga Tanzania nani mwaka 2010!

Lazima jeshi letu libadilike na liwe la kisasa zaidi, mtoa maada kaeleza vizuri tu japo pengine hakuweka sawa lakini he has done good job at least kuonyesha kuwa we can do something

ref; wiki
 
Mkuu jeshi linakaa stand by kuwa na adui or not. Je akitokea ghafla? Au unadhani adui ana chukua muda kuji tokeza. Pia adui ana tumia opportunities. Akiona jeshi lime lala tu basi ana ibuka.

Adui gani mkuu tunaye sasa hivi? Maadui zetu wapo humuhumu ndani miongoni mwetu. Unategemea nani aje achome pesa zake kuleta jeshi kuivamia Tanzania? Ilikuwa zamani tu sio sasa. Mipaka yetu hailindwi lolote analinda Mungu mwenyewe. Ungejua ufisadi unaofanyika humo ndani ya jeshi wala usingesema. Kwa mtazamo mpya wanatakiwa kweli wabadilishiwe kazi japo sio lazima iwe ni kilimo kwani hizo pesa zilizoliwa kwa mbolea zikipelekwa huko ndo utasikia makubwa zaidi na watasema ni usalama wa nchi so msiulize. Philosolofia za ulinzi zinabadilika na majeshi yanatumika kwa faida zaidi kila mambo yanapobadilika la kwetu bado linatumia zile technology na mbinu za Vita vya II vya dunia. We need reforms in kila sector hapa nchini. Lingekuwepo jeshi la maana uongozi ungepata challenge na et least aibu ingekuwepo na uoga kidogo. Mafisadi wana ujasiri wa kufanya lolote kwa vile wanalijua jeshi lilopo na capacity yake kiutendaji, technologia, uzalendo na akili za viongozi wa jeshi lenyewe.

Hiyo si kazi ya jeshi. Dalili ya nchi kuendeshwa vizuri ni good organization...meaning kila taasisi na kazi zake. Hi si kazi ya jeshi. Unless kama unashauri jeshi livunjwe kabisa ianzishwe kitu badala yake itakayo deal na mambo ya njaa.[/QUOTE]

Vyombo karibu vyote havifanyi kazi zao mkuu vinapata maelekezo ya kuilinda CCM kwa nguvu zote. Ingekuwa vinafanya kazi zake tusingekuwa hapa tulipofika. Usalama ungekuwepo tusingeibiwa benk kuu kiasi kikubwa cha fedha kiasi hicho na wao wapo kila mahali. System zote zipo rotten na zinaundwa through ethnic networks unategemea nini jema lifanyike? Kulindana tu ndo kazi ya serikali ya sasa hamna kipya chochote. Kila mahali unapotazama labda useme tunafanya vizuri unajisikia kutapika oovyooo! Sasa tunaitegemea mahakama huu mtihani wa mgombea binafsi tuone kama na majaji nao wanaweza kuburuzwa then tujue sasa hakuna palipobaki na tusubiri mwanguko mkuu unaotufuata baada ya hapo. Hatuna cha kijivunia Tz angalau cha kuonyesha mfano tunafanya vizuri hata kimoja. Tangu utaalamu hadi michezo labda tunafanya vizuri sana kwenye rushwa, ufisadi, uzembe, uvivu, na ujambazi!
 
Tuache ku-crame kwa nguvu na kwa kujiamini

1. Jeshi linapaswa kufanya zaida na mbalisana kuliko wengine

Internet tunayotumia imekuwa invented jeshini (usa) mwaka 1960!!

GPS imekuwa invented jeshini,!

Digital photography tunazotumia leo hii!

Research nyingi sana za uhandisi zinafanywa jeshini,

Infact ilibidi US Army copr os Engineers waanzishe research bureau inayojumuisha na raia, na hizi ni kazi wanazofanya;

Planning, designing, building, and operating locks and dams. Other civil engineering projects include;

flood control, beach nourishment, and dredging for waterway navigation.

Design and construction of flood protection systems through various federal mandates .

Design and construction management of military facilities for the Army and Air Force and other Defense and Federal agencies.

Ni nadra sana kukuta kitu cha uhandisi hasa wa ujenzi kuwa hakijaanzia jeshini.

Hii sio USA tu, Germany, Soviet, Israel wote majeshi yao yanapiga kazi kwenda kwa mbele, na sio kufyeka nyasi Lugalo!. USA wamenza hii ishu tangu 1775!

Nashangaa sana mtu anaposema kazi ya jeshi ni kulinda mipaka eti hatujui adui anakuja lini! wa kuipiga Tanzania nani mwaka 2010!

Lazima jeshi letu libadilike na liwe la kisasa zaidi, mtoa maada kaeleza vizuri tu japo pengine hakuweka sawa lakini he has done good job at least kuonyesha kuwa we can do something

ref; wiki

Asante mkuu. Je unaweza kutoa mifano ya vitu vilivyo buniwa na majeshi ya nchi maskini? Maana hapo umetaja nchi zilizo endelea ambazo zina resources. Sasa wenzetu na sie bajeti yetu ikoje mpaka jeshi lifanye research zote hizo?
 
mkuu ikiwa kila tunaposhindwa huku uraiani basi hiyo kazi ifanywe na jeshi itakuwa ni kulitumia jeshi vibaya.

nadhani sahihi ni kuendelea kulitumia jeshi kwa dharura na mambo ya utafiti kama huo uliofanyika katika US Army hadi kuzalikana kwa iternet na menginewe. Nadhani mimi na wewe tutaicheka hiyo hiyo US Arny ikwa itaanza kuendesha kazi ya kutoa huduma ya internet mfano kuwa na internet service provider company badili ya kufanya utafiti na kutuboreshea hiyo huduma na kisha kuwaacha raia kufanya hizo day to day stuff katika hiyo industry.

kwa mantiki hiyo jeshi, JWTZ lingeweza kuwa na vitengo vya utafiti wa mbegu, kilimo bora n.k. na siyo lenyewe kuanza kumiliki mashamba na kulima.

respect anyway...............
 
Nimekua nikjiuliza na kutafakari maswali mengi na kutafakari baadhi ya majibu yanayoweza kuleta mabadiliko ya kweli.

Nimetafaaki utendaji wa keshi letu la JWTZ na namna ambavyo kama wenye maamuzi, maono na washauri wakijaribu tunaweza kushinda japo vita moja kama nyingine zimekuwa ni ngumu.

Kwa uelewa wangu mdogo na uchambuzi wa haraka sioni kama tanzania ina tishio halisi na kubwa la adui atakayetumia silaha within 10 or 15 yrs to come .

Kwa mtazamo huu nadahani ingekuwa vizuri JWTZ ikawa na mtazamo kiamaendeleeo zaidi . na kama kazi kubwa ya jeshi ni vita basi amiri jeshi mkuu atangaze kuwa adui anayetakiwa kupigwa ni NJAA.

JWTZ likiungana vizuri na wanavijiji katika nagzi za wilaya na vijiji linaweza kua chanzo ka kutokomeza huyu adui. wakiwa na mashamba ya mifano na matreka ambayo wanaweza kuwakodisha wanavijiji huyu adui atakuwa historia

Kuna watu watasema ipo JKT lakini ninepnda hii Vita ipewe JWTZ na kama JKT basi tunaomba tuwe wabunifu. Sio kwa sabau Jeshi la USA hawalimi basi tuseme Sio kazi ya JWTZ.

Labda vita ya NJAA inaweza kuwa rahis kuliko vita ya UFISADI na zaidi ya hapo itafanya JWTZ kuwa ya wanachi zaidi kuliko kohofiwa .

Nampongeza mchangiaji kwa kujaribu kufikiria kwa upana (out ot the box). Ila mimi nisingeshauri wapewe kazi ya kulima badala yake ningeshauri wa pewe kazi ya ulinzi wa raia. Sasa hivi tunaambiwa tusisafiri masaa ishirini na nne kwa sasabu ya utekaji wa mabasi na unyang'anyi.

Nadhani tungetangaza vita dhidi ya ujambazi na uporaji na kulipa Jeshi kazi ya kuhakikisha kuwa hakuna basi la abiria wala gari la binafsi linalotekwa ndani ya mipaka ya nchi yetu ili watu waweze kusafiri kwa masaa ishirini na nne. Hii lingesaidia kuinua uchumi na kupunguza tatizo la misongamano ya magari hasa nyakati za mchana kwani mengine yangeondoka usiku.

Hili wangelifanya kwa kuweka kambi katika maeneo korofi kwa utekaji nyara wa mabasi ya abiria na malori na kufanya patrol muda wote wa siku.

Wakifanikiwa hilo tungeweza kwenda hatua moja zaidi na kutumia vikosi vya ujenzi vya jeshi kufanya kazi za ujenzi wa barabara vijijini ili kuwezesha wakulima wetu wasafirishe mazao yao kwa mda wote wa mwaka. Wangeweza pia kusaidia katika ujenzi wa shule za kata, vituo vya afya na mahakama vijijini.
 
Asante mkuu. Je unaweza kutoa mifano ya vitu vilivyo buniwa na majeshi ya nchi maskini? Maana hapo umetaja nchi zilizo endelea ambazo zina resources. Sasa wenzetu na sie bajeti yetu ikoje mpaka jeshi lifanye research zote hizo?

Mmh! sijajua, na kutokuwepo sio gia ya sisi kutoiga yale mazuri, kumbuka wamenza 1775, kufanya tafiti zao na matokeo kupeleka uraiani.

Mkuu this is not new Idea kwa Tanzania , kwa wanajeshi kuwa innovator, researchers n.k Tuliwahi kuwa na mradi wa magari ya Nyumbu kama utakumbuka sijui umefikia wapi. Kambi ya Mzinga Morogoro mpaka leo wanafanya kazi ya ku-assamble civil explosive (baruti)ambazo zinatumika kwenye construction na migodini. Tunaweza tukitaka kulitumia jeshi katika mambo mengi ya kimaendelea

Na hii haimaanishi unapokuwa na wanajeshi 100, basi wooooooote wahamie kwenye ishu tunazozisema hapa

Kuna ka-nchi kamoja kadogo,africa jina lake nimelisahau, ambaye rais wake ana tuhuma za udikteta, wanajeshi wanapiga mzigo, I dont rember that country for now.

mkuu ikiwa kila tunaposhindwa huku uraiani basi hiyo kazi ifanywe na jeshi itakuwa ni kulitumia jeshi vibaya.

nadhani sahihi ni kuendelea kulitumia jeshi kwa dharura na mambo ya utafiti kama huo uliofanyika katika US Army hadi kuzalikana kwa iternet na menginewe. Nadhani mimi na wewe tutaicheka hiyo hiyo US Arny ikwa itaanza kuendesha kazi ya kutoa huduma ya internet mfano kuwa na internet service provider company badili ya kufanya utafiti na kutuboreshea hiyo huduma na kisha kuwaacha raia kufanya hizo day to day stuff katika hiyo industry.

kwa mantiki hiyo jeshi, JWTZ lingeweza kuwa na vitengo vya utafiti wa mbegu, kilimo bora n.k. na siyo lenyewe kuanza kumiliki mashamba na kulima.

respect anyway...............

Unachanganya mkuu, sijasema service provider, ule ulikuwa ni mfano wa vitu gani wanajeshi wanaweza kugundua na vikawa useful uraiani! sikusema wafanya unachokisema! Volkswagen baada ya kugunduliwa ilikuwa ni kama sera ya jeshi kila raia aweze kununua kwani lilikuwa bei rahisi sana!

Halafu unataka kusema Jeshi likiingina kufanya baadhi ya mambo ya kiraia basi ina maana wengine wameshindwa? au unamana unataka kulitumia jeshi wakati wa matatio tu? sijakuelewa. Jeshi kuji-engage kwenye shughuli za research, innovations na uzalishaji mali ni kwa faida yao! mbona JKT wanafanya??

hivi leo kuna mtu anaweza kusema kuna uwezekano wa kuvamiwa na nchi jirani???

Nampongeza mchangiaji kwa kujaribu kufikiria kwa upana (out ot the box). .

Me too!

Kwa nchi maskini kama yetu Jeshi linaweza likatumika positively kwa manufaa ya Taifa!

tukumbuke sisi ni maskini kma wanaweza kukaa na kufyeka nyasi lugalo! they can be used in more than that, for God sake, si kuwa wanajeshi hawana wataalamu, is another society with all professionals kule!
 
Asante mkuu. Je unaweza kutoa mifano ya vitu vilivyo buniwa na majeshi ya nchi maskini? Maana hapo umetaja nchi zilizo endelea ambazo zina resources. Sasa wenzetu na sie bajeti yetu ikoje mpaka jeshi lifanye research zote hizo?

Naamini una taarifa pia kuwa Jeshi lilijiingia au liko kwenye biashara ya madini. je madini ni adui au madini ni vita rahisi ya ya kweli kuliko njaa.
 
Tuache ku-crame kwa nguvu na kwa kujiamini

1. Jeshi linapaswa kufanya zaida na mbalisana kuliko wengine

Internet tunayotumia imekuwa invented jeshini (usa) mwaka 1960!!

GPS imekuwa invented jeshini,!

Digital photography tunazotumia leo hii!

Research nyingi sana za uhandisi zinafanywa jeshini,

Infact ilibidi US Army copr os Engineers waanzishe research bureau inayojumuisha na raia, na hizi ni kazi wanazofanya;

Planning, designing, building, and operating locks and dams. Other civil engineering projects include;

flood control, beach nourishment, and dredging for waterway navigation.

Design and construction of flood protection systems through various federal mandates .

Design and construction management of military facilities for the Army and Air Force and other Defense and Federal agencies.

Ni nadra sana kukuta kitu cha uhandisi hasa wa ujenzi kuwa hakijaanzia jeshini.

Hii sio USA tu, Germany, Soviet, Israel wote majeshi yao yanapiga kazi kwenda kwa mbele, na sio kufyeka nyasi Lugalo!. USA wamenza hii ishu tangu 1775!

Nashangaa sana mtu anaposema kazi ya jeshi ni kulinda mipaka eti hatujui adui anakuja lini! wa kuipiga Tanzania nani mwaka 2010!

Lazima jeshi letu libadilike na liwe la kisasa zaidi, mtoa maada kaeleza vizuri tu japo pengine hakuweka sawa lakini he has done good job at least kuonyesha kuwa we can do something

ref; wiki

Hata NYUMBU imeanzia na jeshil etu, jana nimeona Kikwete anasema eti wata adopt technology inayotumiwa na jeshi la JORDAN huko kwenye kiwanda cha NYUMBU, siasa bwana
 
mipaka walinde saa ngapi?, mafunzo wafanye saa ngapi?. Una dhani adui anatoa toa taarifa?. Fikiri kabla ya kusema!

Schedule inayofaa ya kazi ya, uzalishaji, ulinzi, mafunzo, ndio jibu. Pia vita hutangazwa hivyo taarifa zinakuwepo, halafu kuna nchi km China, South and North Korea ambapo jeshi hujihusisha na uzalishaji. Hata hapa kwetu tuna Nyumbu (imekufa?), ni sehemu ya uzalishaji ati.
Ila nakuunga mkono kua haya yote itakua mzigo mkubwa ndani ya vichwa vyepesi vyepesi vya serikali ya CCM. Ninachojua kama wafadhili wataamua kujitolea zana, pesa za posho na uendeshaji ambazo zitasimamiwa na serikali ya CCM basi ni kesho tu JK anaweza tangaza kuanzishwa kwa mashamba jeshini.
 
labda hoja ni kuwa hatujalitumia Jeshi letu vizuri wakati wa amani.. hao Wamarekani pamoja na vita zao zote, kulinda mipaka yao n.k bado jeshi lao ni sehemu kubwa ya utafiri na maendeleo ya Sayansi na Teknolojia..

Kwa mfano.. kwanini COSTECH isiwe sehemu ya jeshi?
 
mipaka walinde saa ngapi?, mafunzo wafanye saa ngapi?. Una dhani adui anatoa toa taarifa?. Fikiri kabla ya kusema!

Muhimu ni schedule inayofaa kwa uzalishaji, mafunzo, ulinzi nk Kuna nchi km China, South and North Korea ambapo majeshi yao yanajihusisha na uzalishaji wa kilimo na mambo mengine. Hapa kwetu pia tunajihusisha na uzalishaji nyumbu (haijafa? eti) na majiko ya mkaa.
Vijana wa kulinda mipaka tunao wengi tu na hawana kazi ila nakuunga mkono kua hivyo vichwa vyepesi vyepesi vya serikali ya CCM hawayawezi hayo mambo, maana ni zaidi ya uwezo wao kupanga na kufanikisha. Ninachojua mimi kama wafadhili wataamua kujitolea zana, pesa ya posho na uendeshaji na ambapo hiyo pesa itasimamiwa na serikali ya CCM, basi ni kesho tu JK anaweza tangaza kuanzishwa hayo mashamba Jeshini. Lakini uzalishaji utakua hamna kitu maana ufisadi ni DAMU ndani ya mishipa ya serikali ya CCM.
 
Jana nilimsikia Waziri Wassira akitamka kwa mdomo wake kuwa hatuna tatizo la chakula kwa sasa kwa sababu mvua za vuli zimenyesha. Nikawaza kuna uhusiano gani kati ya mvua za vuli zilinyesha na hali nzuri ya chakula?

Hivi Waziri ameshindwa kuelezea kwa upana kwa nini hatuna tatizo la chakula? au Waziri anajua kuna tatizo la chakula ila anaficha? au hakuwa na jibu hivyo akaamua kujibu chochote? Ama kweli, Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!
 
Back
Top Bottom