Kwanini JK hakuongea na 'wazee' wa Dar es salaam wakati wa mgomo wa madaktari?

kabuga

Member
Nov 19, 2011
78
14
Ndugu wanaJF, rais amekuwa akitumia style ya kuongea na wale wanaojiita 'wazee' wa Dar es salaam kila anapotaka kujibu mapigo katika masuala mbalimbali. Sikuona akifanya hivyo kwa wakati wote ambao madaktari walikuwa kwenye mgomo. Pamoja na kwamba mgomo umekwisha, naomba kupata maoni yenu kuhusu hili. Naomba kuwasilisha.
 
Mkuu,
Huu ni mtihani live na challenge iliyoutikisa utawala wake!
JK ana akili sana, alijua kuwa kwa suala la tiba hata wazee wangemponda!
 
Hao wazee wameshamchoka na ftari yake coz wao wakiwa na matatizo anasepa ila yy naji yakiwa shingoni ndo anawaita na kuwapa maji ya soda tu.pia hao wazee wana ndugu na jamaa na wao pia wanaumwa ss wakienda pale karimjee na kuanza kupiga makofi we unadhani mmoja wao hawezi kwenda muhimbili kutibiwa mifupa?
 
Ndugu wanaJF, rais amekuwa akitumia style ya kuongea na wale wanaojiita 'wazee' wa Dar es salaam kila anapotaka kujibu mapigo katika masuala mbalimbali. Sikuona akifanya hivyo kwa wakati wote ambao madaktari walikuwa kwenye mgomo. Pamoja na kwamba mgomo umekwisha, naomba kupata maoni yenu kuhusu hili. Naomba kuwasilisha.

Hebu tukumbushe ni masuala mangapi na yapi aliyoongea na wazee wa Dar es Salaam na kuhusu mgomo ulitaka aongee na nini?
 
Mkuu,
Huu ni mtihani live na challenge iliyoutikisa utawala wake!
JK ana akili sana, alijua kuwa kwa suala la tiba hata wazee wangemponda!
make keshaona kuwa kila akiongea wachambuzi wa hutuba na matamko yake wakichambua inazidi kushusha credibility, hivyo dawa ni kukaa kimya ambapo 'strategically' imekaa vizuri

Angeongea nao awaambie nini wakati na wao ndo wahanga wakubwa? Jamani JK is not that dumb, well though he isn't smart!
 
Jamani kile kilikuwa kipindi chake cha kudondoka jukwaani,hivyo alishauriwa na mtaalamu wake wa nyota asijitokeze hadharani kuepuka mieleka ya hapa na pale majukwaani.
 
Mi nadhani ametekeleza ule usemi wa mzee Mkapa nanukuu "siwezi kuzuia masikio kusikia ila naweza kuuzuia mdomo wangu usiongee" mwisho wa kunukuu!

ameshaongea sana na sasa kamuachia mtoto wa mkulima (MP) AONGEE NA WATAALAM
 
Ndugu wanaJF, rais amekuwa akitumia style ya kuongea na wale wanaojiita 'wazee' wa Dar es salaam kila anapotaka kujibu mapigo katika masuala mbalimbali. Sikuona akifanya hivyo kwa wakati wote ambao madaktari walikuwa kwenye mgomo. Pamoja na kwamba mgomo umekwisha, naomba kupata maoni yenu kuhusu hili. Naomba kuwasilisha.

Wazee ni wateja wazuri sana wa madaktari. Kuwaita na kuwatumia kuwananga watu wanaowategemea katika afya zao za kila siku(wengi wana ageing deseases na kuhitaji uangalizi wa madaktari walau moja kwa mwezi). Wazee kushabikia siasa dhidi ya madaktari ingekuwa ni sawa na kuwachonganisha na madaktari, wangekuwa wanaambiwa mahospitali kuwa kama wanaona hawapati huduma bora waombe Ikulu iwapeleke India.

Mgomo wa madaktari ni issue ambayo mwendawazimu pekee angeufanyia mipasho kwa kuita wazee. Ni issue ambayo inahusu maisha ya watu bila kujali nafasi zao. Madaktari wana siri nyingi sana za afya ya watu mbalimbali hata kuhusu hao viongozi wenyewe, Ndiyo maana mwandishi mmoja maarufu wa redio alijiingiza wakapublish file lake na mkewe akakaa kimyaa. Ni issue sensitive sana. JK kukaa kimya alijua fika kuwa he's the last resort. Kujihusisha mwanzomwanzo kungefanya issue unsolvable. Ndiyo maana akawa anamtumia Pinda na kumpatia maagizo ya nini cha kufanya. Alianza kumuagiza awatishe ika-backfire, akaona ni bora warudi mezani. Kama Pinda angekosa legitimacy kwa maagizo mabaya kutoka kwa JK hapo sasa JK angeingia mwenyewe na kuchukua nafasi ya 'Last resort'.
 
Back
Top Bottom