Kwanini JK aliamua ghafla kukubali uundwaji wa katiba mpya? Je tume aliyoiunda yaweza kutupa hints? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini JK aliamua ghafla kukubali uundwaji wa katiba mpya? Je tume aliyoiunda yaweza kutupa hints?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chintu, Apr 10, 2012.

 1. C

  Chintu JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2012
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 3,403
  Likes Received: 857
  Trophy Points: 280
  Kuna mijadala mingi inayosuport na kupinga composition ya wajumbe wa tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya kwa sababu mbalimbali. Lakini mimi nadhani swali la kujiuliza ni kwamba. Ilikuwaje mwenyekiti wa chama (CCM) ambacho hakijawahi kuona umuhimu wa kuunda katiba mpya kwa madai kuwa katiba iliyopo sasa inafaa sana, ghafla bin vuu akatangaza kuyatambua na kuyakubali madai ya CDM na wadau wengine kuwa ipo haja ya kuunda katiba mpya?

  -Mimi nadhani kuna watu walimshika sikio Raisi wetu na kumwambia kuwa suala la kuunda katiba mpya halikwepeki hata kama chama hakipendi (which was absolutely true) na kumwambia kuwa achana na mawazo ya chama kwa maana ni afadhali tuunde katiba wakati wewe mwenyewe "mwenzetu" upo madarakani na kutumia mamlaka unayopewa na katiba hii poa, kupitisha yale "matakwa yetu" kuliko akaja mtu mwingine ambaye hatujui atakuwa ni wa kundi gani na kutumia mamlaka ya katiba hii hii kuyakataa matakwa yetu. Watu hawa hawawezi kuwa ni wanaCCM na kama ni wanaCCM basi hawakuwa wakiwasilisha maslahi ya CCM wala serikali, kwa maana tulisikia kauli za mwanasheria mkuu Mh Werema na waziri wa sheria na katiba Mh Celina Kombani wakiongea kwa kujiamini kabisa kwamba katiba iliyopo ni poa mno!
  Kazi ya tume itakuwa ni kukusanya maoni kuyaorganize na kupriotize.

  Hebu tufikirie hawa wajumbe ni "wanawake" watupu. Ni dhahiri hakuwezi kuwa na mgogoro katika kukusanya maoni wala kuyaorganize, mgogoro ni wazi utakuwepo kwenye kupriotize kwa sababu composition haijabalance na hasa kunapokuwa na mazingira ambayo yanajenga hisia za kuwepo ajenda ya siri kutokana na uamuzi huo wa kuanzisha katiba mpya kutolewa ghafla bin vuu na mtu ambaye jana yake tu alikuwa akikataa kuunda katiba mpya. Na hapo ndipo hoja ya uwakilishi sawa inapojitokeza. Ni wazi hatuwezi kuweka uwakilishi sawa kutoka kila kundi lakini kuna makundi makubwa ya dhahiri yanayojulikana, kwa mfano gender na dini kubwa mbili ukristo na uislam. Kuyapuuzia haya na kusingizia upuuzi wa kuwakilisha wazanzibari ili kupenyeza maslahi fulani (kwa sababu ya "common character ya wazanzibar hao") katika nchi ambayo kuna wazanzibari wengi sana Tanganyika wanoishi kwa furaha na amani na ambao hawabaguliwi kwa chochote kutokana na uzanzibari wao, kunaweza kutupa hints za ni nani waliomshika sikio Rais wetu na kwa lengo la kupenyeza maslahi gani?

  Tusubiri tutayasikia na kuyaona.
   
 2. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwamba CCM haikuwa na ajenda ya Katiba mpya ni kweli kwa sababu Serikali ya CCm ambayo ndiyo iko madarakani na viongozi wake kwa sasa hawana Dira, wanaongozwa na hisia tu. Wanatumia staili ya uongozi ya "Management by Crisis" na siyo "Management by Objectives".
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kinachotakiwa sasa ni Katiba mpya, mjadala wa nani alisema watanzania wanataka katiba mpya na nani anaongoza upatikanaji wa katiba hiyo ni upofu wa mawazo, majungu na mwisho wake ni kuunda Katiba mbovu kwa sababu watu walijikita huko badala ya kutoa mawazo ya katiba inayotakiwa.
   
 4. C

  Chintu JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 3,403
  Likes Received: 857
  Trophy Points: 280
  ...upofu umeanzia na JK kwa upuuzi wa kuwa na wazanzibari 15 na watanganyika 15. kwa maoni yangu wazo hilo lenyewe si la kimuungano bali linatufanya tusijifikirie utanganyika na uzanzibari badala ya kufikiria uTanzania wetu wakati wa mchakato. Rais anaanzisha mchakato kwa kutuambia sisi si wamoja.
   
 5. n

  ngulla Member

  #5
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muungano umekuwa ukilalamikiwa sana kila siku, tume iliyoudwa inalalamikiwa sana hasa na watanganyika katika misingi ya muungano, je katika kupiga kura ya referendum watanganyika watakuwa tayari kupiga kura? watakuwa wamesahau hoja zao za msingi kuhusu muungano? Je kuna haja ya kuendelea na muungano?
   
Loading...