Kwanini jiko la mkaa ukiwa ndani linaweza kupelekea vifo

Newbies

JF-Expert Member
Jul 13, 2018
1,449
2,113
Imekuwa sio ajabu kusikia watu wamekutwa wamefariki ndani baada ya kulala na kuacha jiko la mkaa likiwaka. Lakini swali ambalo watu wamekuwa wakijiuliza ni, nini hutokea na kusababisha kifo pale mtu anapoacha jiko la mkaa likiwa linawaka huku akiwa amefunga madisisha na vyanzo vingine vya kupitisha hewa chumbani.

Kama tujuavyo mwili wa binadamu huhitaji hewa safi ya oksigeni ili viungo naseli viendelee kuwa hai. Kunapotokea mchomo kwa viwakaji kama vile mkaaa huzalisha gesi ya sumu kali iitwayo gesi ya karboni monoksaidi. Kwakuwa vyanzo hewa vitakuwa vimefungwa itasababisha binadamu aanze kuvuta dutu hii hatari, inapoingia katika mwili wa binadamu hufanya muunganiko na haemoglobini nakusababisha kutokea muunganiko unaoitwa Carboxhemoglobin (CoHb) ambayo huchukua mahali pa oksigen jambo hili husababisha mwili wabinadamu kukosa oksigeni katika viungo na hupelekea ubongo, moyo na seli kuanza kuharibika bila mhusika kugundua. kwa lugha ya kikoloni wanaita silent killer . Huitwa hivyo kwasababu haina rangi, harufu, ladha, wala mchomo.

sii hivyo tu bali pia gesi hii ya sumu inaweza kuua hata wakati wamchana ikiwa binadamu ataivuta na kukawepo na upatikanaji mdogo wa oksigeni. Nnihatari kwakuwa hutaweza kuihisi
HZI HAPA DALILI ZA MTU ALIYESHAMBULIWA NA GESI HII
  • Kuumwa nakichwa
  • Kutapika
-Kubadilika kwa muono
- Mafua

Kuhisi udhaifu mwilini
dalili za hatari ni kamavile, shambulio la moyo, mapigo ya moyo bila mpangilio, kupooza na kushindwa kupumua.

Matibabu, ni hewa safi ya oksigeni.

Ufanye nini ili kuepuka kifo kinachosababishwa na gesi hii ya sumu

Mosi - Hakikisha viwakaji vinakaa mbali na sehemu ya kulalala na visiwe vinawaka

Pili - Weka kihisi hewa ya karbonmonoksaidi( carbonmonoxide ditector) kwaajili ya usalama wako, hiki kinaweza kufungwa katika sehemu za kulala na mazingira mengine.

Tatu - Hakikisha majiko yako ya gesi, mafuta yataa na viwakaji vyote vinachekiwa na kufanyiwa ukarabati

Nne - Usiwashe kiwakaji huku huku kukiwa hakuna uhakika wa hewa ya oksigeni kuingia

Mwisho nashauri Serikali na asasi nyingine zitoe elimu kuhusu jambo hili.
 
Kuna family moja zanzibar miaka ya nyuma kdg walikufa watu wanne wa family hio wao walilala na generator ndani likiwa linawaka
 
Umefanya jambo zuri kutukumbusha. Ili tahadhari ichukuliwe. Watu wa Nyanda za Juu Kusini, ni wahanga wakuu wa majiko ya mkaa nyakati za usiku kutokana na baridi kali hasa msimu kama huuu.

Wenyewe wanaita majiko yenye mkaa "VIGAE". Huviamini sana VIGAE kwenye kupunguza baridi, pasipo kujua hivyo vigae pia ni chanzo cha kifo.
 
nikweli mkuu
 
Shukran mkuu, topic yako imenikumbusha mbali , kuongezea tu ... Carbon monoxide ina affinity 200x kubond na haemoglobin kuliko Oxgen , yaan Kama oxygen na carbon monoxide zitafika kwa pamoja haemoglobin ita prefer kubond na carbon monoxide kuliko oxygen unless concentration ya Oxgen iwe kubwa
 
Imekuwa sio ajabu kusikia watu wamekutwa wamefariki ndani baada ya kulala na kuacha jiko la mkaa likiwaka. Lakini swali ambalo watu wamekuwa wakijiuliza ni, nini hutokea na kusababisha kifo pale mtu anapoacha jiko la mkaa likiwa linawaka huku akiwa amefunga madisisha na vyanzo vingine vya kupitisha hewa chumbani.

Kama tujuavyo mwili wa binadamu huhitaji hewa safi ya oksigeni ili viungo naseli viendelee kuwa hai. Kunapotokea mchomo kwa viwakaji kama vile mkaaa huzalisha gesi ya sumu kali iitwayo gesi ya karboni monoksaidi. Kwakuwa vyanzo hewa vitakuwa vimefungwa itasababisha binadamu aanze kuvuta dutu hii hatari, inapoingia katika mwili wa binadamu hufanya muunganiko na haemoglobini nakusababisha kutokea muunganiko unaoitwa Carboxhemoglobin (CoHb) ambayo huchukua mahali pa oksigen jambo hili husababisha mwili wabinadamu kukosa oksigeni katika viungo na hupelekea ubongo, moyo na seli kuanza kuharibika bila mhusika kugundua. kwa lugha ya kikoloni wanaita silent killer . Huitwa hivyo kwasababu haina rangi, harufu, ladha, wala mchomo.

sii hivyo tu bali pia gesi hii ya sumu inaweza kuua hata wakati wamchana ikiwa binadamu ataivuta na kukawepo na upatikanaji mdogo wa oksigeni. Nnihatari kwakuwa hutaweza kuihisi
HZI HAPA DALILI ZA MTU ALIYESHAMBULIWA NA GESI HII
  • Kuumwa nakichwa
  • Kutapika
-Kubadilika kwa muono
- Mafua

Kuhisi udhaifu mwilini
dalili za hatari ni kamavile, shambulio la moyo, mapigo ya moyo bila mpangilio, kupooza na kushindwa kupumua.

Matibabu, ni hewa safi ya oksigeni.

Ufanye nini ili kuepuka kifo kinachosababishwa na gesi hii ya sumu

Mosi - Hakikisha viwakaji vinakaa mbali na sehemu ya kulalala na visiwe vinawaka

Pili - Weka kihisi hewa ya karbonmonoksaidi( carbonmonoxide ditector) kwaajili ya usalama wako, hiki kinaweza kufungwa katika sehemu za kulala na mazingira mengine.

Tatu - Hakikisha majiko yako ya gesi, mafuta yataa na viwakaji vyote vinachekiwa na kufanyiwa ukarabati

Nne - Usiwashe kiwakaji huku huku kukiwa hakuna uhakika wa hewa ya oksigeni kuingia

Mwisho nashauri Serikali na asasi nyingine zitoe elimu kuhusu jambo hili.
kuna wakuu wa mikoa nawilaya zake wakiwa wanasimamia hadi watendaji wa serikari za mitaa, kuwe na program inchi nzima juu ya mambo kama haya.
 
Back
Top Bottom