Kwanini Jeshi la Polisi limekubali kutia saini mkataba na China wa kupambana na matukio ya kihalifu kwa vyombo vya usafiri ikiwemo Bajaji na Pikipiki?

Festo Ndibanje

New Member
Jun 25, 2019
4
2
Dar es Salaam

Kampuni ya Tamoba ya nchini Tanzania imetiliana saini ya makubaliano ya kibiashara na kampuni ya Hytera ya nchini China kwa lengo la kupambana na matukio ya kihalifu kwa vyombo vya usafiri ikiwemo Bajaji na Pkipiki.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya kutiliana saini hiyo, Mkuu wa mawasilino kanda malum ya Dar re Salam ACP Angela Kibiriti wakati akimuwakilisha Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa, amesema kuwa, madereva wa boda boda wamekua wakikabiliwa na changamoto ya matukio ya kihalifu.

“Madereva wa Bajaji na Pikipiki wamekua wakikabiliwa na changamoto kubwa ya matukio ya uhalifu, hivyo wakifungiwa vifaa hivyo katika vyombo vyao vya usafiri vitaweza kuwasaidia sana, kwani vina uwezo wa kutoa taarifa nzima ya tukio linalotokea tena kwa wakati” amesema ACP Angela Kibiriti.

Amesema kuwa, kazi ya Jeshi la Polisi ni kuhakikisha wanalinda raia na mali zao, hivyo kuwepo kwa mfumo unaofunguwa katika Pikipiki na Bajaji kutaweza kuwasaidia kuweza kupambana na matukio ya kihalifu kutokana na matukio ya kihalifu yanayotokea kwa madereva wa Bajaji.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tamoba, Joseph kimisha amesema kuwa, vifaa hivyo vitaingia nchini Tanzania baada siku 40 vikitokea nchini China huku, akibainisha kuwa makubaliano hayo yamelenga kuwanyanyua madereva wa boda boda na Pikipiki kutoka kiwango cha chini na kuweza kupata kipato cha juu.

Amesema kuwa, vifaa hivyo vitaweza kuwasaidia madereva hao kuwapa ulinzi madereva hao kwa masaa 24 ambapo vitakua vikionesha tukio linapotokea moja kwa moja na kuweza kupata msaada wa haraka.

“Vifaa hivyo vinauwezo mkubwa sana kwani vinarekoda ambayo inaweza kurekodi matukio yote pamoja na huduma ya WhatsApp ambayo itawasaidia wakuu wa vituo wote kuweza kuona matukio moja kwa moja” amesema Kimisha

Ameongeza kuwa, mfumo huo utaanza kuanzia kituoni ngazi ya Kata, wilaya hadi Mkoa ambapo madereva hao watavaa unifom maalum ambazo pia zitaweza kuwaingizia kipato kutokana na mabango yatakayokuepo nyuma ya uniform hizo.

“Tulikubaliana sisi na Jeshi la Polisi, Kampuni ya mawasiliano ya TTCL na kampuni ya Hytera kwamba unifom hizo zikachukuliwe nchini China kwa Bei ya shilling 100,000 ambapo madereva wataweza kulipia kidogo kidogo kwa muda wa miezi minne ” amesema kimisha
Naye, Afisa Habari wa Bodaboda Wilaya ya Ilala Ally Bakari amesema kuwa, wanaishukuru sana Kampuni ya Tamoba kwani wamekuja kwa lengo la kuwasaidia madereva wa Bajaji na Pikipiki katika matukio ya kihalifu ambayo yamekua yakiwakumba siku hadi siku.

Habari zenu ndugu wanajamii wa hapa. Mimi ni mgeni hapa kama mnavyoweza kuona majina yangu halisi hapo juu. Nimelazimika kutumia jukwaa hili huru kufikisha dukuduku langu kwa waheshimiwa ili kuepuka vikwazo ambavyo huenda ningekumbana navyo kama ningetumia njia nyingine.

Naamini wengi wenu mmepata dukuduku pia kuhusu swali langu hapo juu na labda kuhusu nia ya muuliza swali, naomba subira zenu, najaribu kuwa mwangalifu ili niweze kueleweka vema.

Kwanza nianze kwa kulipongeza jeshi letu kwa hatua hiyo waliyofikia, kumbe wanajali na kuzingatia hali halisi iliyopo katika usafiri wa bodaboda, kwa kweli kwa upande wangu nilikuwa na uhakika mkubwa sana tena kwa asilimia mia moja kuwa hawajali chochote kinachotokea katika usafiri wetu huo, hawajali chochote kuhusu ajali za kila siku zinazotokea; hawajali kuhusu wizi na uporaji wa pikipiki uliotapakaa kila kona ya nchi; hawajali chochote kuhusu sifa na utambuzi wa madereva wa bodaboda, hawajali chochote kuhusu sare na kofia za kukinga majeraha n.k, kwa hakika mimi niliamini hivyo, lakini sasa angalau wamejaribu kunibadili mtazamo, lakini pamoja na hilo bado na simama na swali langu hapo juu, kwa nini mkataba huu na “wachina” na sio ule wa machi 2017?

Nimeuliza swali hili kutokana na uhusiano wangu mkubwa na masuala haya ya “matatizo ya bodaboda” hapa inchini, na hasa kuhusu namna ya kukabiliana na matatizo haya yanayoonekana kujenga usugu.

Ningependa kusema tu hapa, huenda mimi ndiye mtanzania niliyetafiti zaidi ya wengine wote kuhusu masuala haya ya bodaboda na kufauru kwa kiasi kikubwa kuona njia ya kuyakabili matatizo haya. Nilitafiti na kuandaa mfumo wa kukabiliana na matatizo haya na kuuwasilisha kwa taasisi saba za serikali, miongoni mwao, tatu zinalihusu jeshi letu hili la polisi. Mfumo huo nimeuweka hapa, Nakupa nafasi upitie alafu nitahitimisha dukuduku hili.

Sasa tuangazie kuhusu mkataba huu uliotiwa saini mwezi juni 2019.

Kwanza imesemwa kuwa ni mkataba kati ya Tanzania na China?!, halafu yakatajwa makampuni mawili, moja la kienyeji na lingine la kichina?! Lakini hapo hakuna raisi, waziri au mabalozi kutoka katika nchi hizo mbili?!

Lakini muhimu zaidi imesemwa ni kifaa kinachofungwa kwenye pikipiki. Na mwisho nililoliona hapo wanasema ni mkataba wa kibishara. Sasa sijui ni biashara gani hiyo inayotaka kufanywa katikati ya madhila haya yanayogharimu roho za watu kama sio viungo vyao?. Tuache hayo, tuzungumze la msingi kuhusu “kifaa”.

Ningependa kukumbusha, mimi nilitafiti suala hili kwa miaka, kwa kifaa hiki kinachoelezewa hapa, hakiwezi kuwa na tija yoyote, kwanza kina gharama za kuhudumia, lakini hata ikiwa kwa bahati kikajaribu kufikia lengo lake, bado kina lengo la kutatua tatizo moja pekee la kurekodi uhalifu badala ya kuuzuia usitokee.

Matatizo ya bodaboda ni mtambuka; kuna matatizo ya bodaboda wenyewe kama kugoma kuvaa sare na kofia ngumu, kukosa sifa, wizi na uporaji wa pikipiki, ulevi, uvutaji bangi n.k; kuna matatizo ya kimamlaka kushindwa kuratibu bodaboda kwa mfano, pikipiki kuzagaa hovyo mjini na trafiki kushindwa kusimamisha bodaboda au kukamata zinapovunja sheria za usalama barabarani. Lakini pia kuna matatizo ya abiria kushindwa kutofautisha kati ya bodaboda walioidhinishwa na wavamizi wa shughuli hizi na hivyo kujikuta wakiingia matatizoni bila kujua.

Matatizo yote haya kwa ujumla wake yanafanya suala la bodaboda kuwa tata sana, ndio maana hali imebaki kuwa hivyo ilivyo tangu usafiri huo uanze hapa nchini yapata miaka kumi na miwili sasa. Na hali hiyo si hapa Tanzania pekee, Kenya, Uganda, Nigeria n.k hali ni hiyo hiyo. Mfumo huo wa machi 2017 umeshughulika na matatizo yote hayo kwa ukamilifu

Sasa, kwa tofauti hii kubwa kati ya kifaa hicho cha mchina na mfumo niliouwasilisha kwao, kwa nini nisiwe na dukuduku moyoni, na wala sio wivu au choyo ya kiswahili iliyonizonga, kwa kuona mchina kapata dili kiulaini tena kwa kidude tu anachodai kuwa anacho huko kwao.

Nimetafakari jambo hili kwa zaidi ya siku 50, nikaona hapana, lazima niondoe dukuduku.


Ndugu wanajamii, upi mtazamo wenu kuhusu kadhia hii?View attachment KAZI KUU 3.pdf
 
Document hiyo inasema:

“Tulikubaliana sisi na Jeshi la Polisi, Kampuni ya mawasiliano ya TTCL na kampuni ya Hytera kwamba unifom hizo zikachukuliwe nchini China kwa Bei ya shilling 100,000 ambapo madereva wataweza kulipia kidogo kidogo kwa muda wa miezi minne ” amesema kimisha
 
Document hiyo inasema:

“Tulikubaliana sisi na Jeshi la Polisi, Kampuni ya mawasiliano ya TTCL na kampuni ya Hytera kwamba unifom hizo zikachukuliwe nchini China kwa Bei ya shilling 100,000 ambapo madereva wataweza kulipia kidogo kidogo kwa muda wa miezi minne ” amesema kimisha
Rudi Nyumbani Kumenoga Sasa Kazi ni Kwako hakatwi mtu hapa na tunatwanga kote kote kama vipi wakupe unachotaka.
 
Pikipiki 10,000 kwa lakini moja moja =100,000×10,000
=1,000,000,000/- si haba.
 
Sarakasi ingine kama ilivyokua mambo ya Speed Governor.
Lengo ni zuri tatizo halitatekelezwa vizuri..kwa ufupi huu ni mradi wa kuingiza pesa kama miradi mingine.
 
Document hiyo inasema:

“Tulikubaliana sisi na Jeshi la Polisi, Kampuni ya mawasiliano ya TTCL na kampuni ya Hytera kwamba unifom hizo zikachukuliwe nchini China kwa Bei ya shilling 100,000 ambapo madereva wataweza kulipia kidogo kidogo kwa muda wa miezi minne ” amesema kimisha


Imekaa kiulaji zaidi na siyo kuwasaidia hao madereva kama wanavyojipambanua
 
Kila siku mambo mapya, wameshindwa kukamata simu zinazoibiwa kila siku leo wataweza bajaji na pikipiki!!
 
Akili zetu zinagonga mwamba sana haziwezi kupambana katikati ya soko la kimataifa
Hivi kila kitu ni lazima kitoke ughaibuni?
Hivi inamaana Jeshi la Polisi limeshindwa kabisa kupambana na uhalifu huo mpaka uanze kutozana mabweni hayo?
Tunakwama mahali 'mark my words'!!!
 
FURSA FURSA FURSA...Definition of an Entrepreneur : The capacity and willingness to develop, organize and manage a business venture along with any of its risks in order to make a profit. ... In economics,entrepreneurship combined with land, labor, natural resources and capital can produce profit. In other words : Exploiting the needs of the people in order to make money...
 
... usishangae ukapelekwa mswada kwa hati ya dharura Bunge la Septemba ili litungiwe sheria kwamba ni LAZIMA bodaboda na bajaji zote zifunge hivyo vifaa! Hakuna cha kuwasaidia wala nini, the motive behind this move is kodi, kodi, kodi! As simple as that!
 
Akili zetu zinagonga mwamba sana haziwezi kupambana katikati ya soko la kimataifa
Hivi kila kitu ni lazima kitoke ughaibuni?
Hivi inamaana Jeshi la Polisi limeshindwa kabisa kupambana na uhalifu huo mpaka uanze kutozana mabweni hayo?
Tunakwama mahali 'mark my words'!!!
hili ni janga Chief
 
Watu wanajua kuona fursa ..mtu kaishafunga hesabu za billion apo kuanzia kampuni hadi viongozi ..mzigo anakuja kubeba bodaboda
 
Asante mods kwa kuyapanga vizuri maelezo hayo, lkn dukuduku langu hapo ni kuhusu tofauti kati kifaa hicho kutoka China na mfumo wa kizalendo uliwasilishwa serikalini tangu machi 2017 ambao ninaamini una unauwezo mkubwa wa kukinzana na matatizo mtambuka ya bodaboda,lkn mfumo huo umekaliwa kimya kwa muda wote huo na badala yake mchina anapewa kazi tena kwa lengo la kutatua tatizo moja pekee (wizi wa pikipiki)na kuacha matatizo mengine kama yalivyo.
 
Bajaji na pikipiki basi zingepigwa marufuku kuingizwa nchini.....
Tujue moja

Ova
 
Back
Top Bottom