Kwanini Jangwa la Sahara ni chanzo cha umasikini Tanzania

bahati93

JF-Expert Member
Aug 6, 2015
1,134
2,010
Hongereni kwa kuvuka mwaka wanajamii.

Hii hali ya kushindwa kukidhi mahitaji muhimu kwa binadamu imekuwa ikusumbua sana nchi maarufu zipatikanazo CHINI YA JANGWA SAHARA. Hali hii sasa inafafanuliwa kama hali ya kuishi chini ya dola moja na umoja wa mataifa hii hali ni umaskini. Kumekuwa na nakala nyingi sana zikitaka kudadavua kwamba kitu gani kinaleta umaskini huu majibu yaliyozoeleka kama usimamizi mbovu, kukosa maarifa, unyonywaji. Lakini huu umaskini una vyanzo vinavyoonekana na VISIVYOONEKANA ndio maana unakuwa mgumu sana kuutibu, sasa kuna hichi kizingiti nataka nikimulike leo kilichosababisha umaskini huu na nitatoa mikakati ya kukwepa kizingiti hichi

Jangwa la sahara hili lidubwana kwa namna moja au nyingine limepelekea sana nchi zilizo chini yake kukumbwa na umaskini. Ndio maaana zinapewa jina nchi kusini mwa jangwa la sahara na Tanzania ni mojawapo ya nchi zilizobahatika kuwepo kusini mwa jangwa hilo.

JINSI JANGWA LA SAHARA LINAVYOLETA UMASKINI.

KIZINGITI/KUTENGANISHA MWIINGILIANO. Hichi kitendo cha kutenganishwa nchi zetu na ulaya limefanikiwa kwa uwezo mkubwa sana mpaka kupelekea watu tupatikanao kusini mwake kuwa na rangi tofauti na wenzetu wapatikanao kaskazini na sehemu kubwa ya dunia, hii imepelekea kuwa wapweke na kunyanyaswa na binadamu angavu kwa ngozi. Endapo lisingekuwepo basi tungekuwa angavu kutokana na mwingilio na tusingechukuliwa kama viumbe chini ya binadamu, hivyo tungenyonywa kistarabu na madada zetu wangepata mashemeji wa nguvu kutoka kaskazini hivyo utajiri mahari na neema kibao.

KUTENGANISHWA KIBIASHARA. Sio tu limetenganisha muingiliano bali pia biashara limefanya kwa miaka mingi tangia enzi kufanya biashara na wazungu kitendawili, utapita wapi. Wakati wenzetu wakinufaika kwa kuwa na uwanja mkubwa wa biashara kuanzia china mpaka west Germany na nchi kaskazini mwa jangwa la sahara, kutokana na kuwa na wigo mkubwa wa kufanya biashara ilipelekea wanyama na mazao yenye faida kutumika vizuri ipasanyo mfano farasi ambaye hapatikani kusini mwa jangwa aliwapa boost kubwa sana hawa watu wa kaskazini, endapo kusingekuwa na jangwa basi na sisi tungefaidi kuwa na mnyama makini Farasi, mambo mengi tunakwama kwa sababu ya kuruka stage sasa jamii inakimbilia magari wakati stage ya kuendesha farasi haijapita ndo maana ata barabara za kueleweka hakuna.

KUTENGANISHWA KUITAMADUNI. Endapo hili jabali la jangwa lisingekuwepo basi jamii za kusini zingefahamiana na wamisri na falme yake kubwa jambo hili lingetuboost sana kwani utalamu wa kuandika tungejua kitambo sana tusingebabaishwa. BONUS kwa binadamu ambao wapo tanzania tungeabudiwa na wamisri kama miungu kwa sababu tupo na chanzo cha mto nile ambao uliabudiwa na juhudi za kupata chanzo chake zilishindikana kutokana na jangwa hili temi hapa duniani. Hivyo tumekuwa na utamaduni ambao umepitwa na wakati kutokana na kutokujua nini wanafanya wenzetu. utamaduni ndio bakora kubwa sana ya umaskini kwani huwezi lala uamke kesho useme unabadili utamaduni, utamaduni watu wa dini wanaweza sema unatoka kwa muumba, Lakini watu wa sayansi wanasema ni evolution of socialization ( inajengwa taratibu pasipo wahusika kutambua).

JINSI LA KUKABILIANA NA JANGWA HILI LILETAO UMASKINI

Hapa na majibu mawili ya kufikirika

KUHAMA TANZANIA. hii ni njia rahisi kabisa nashangaa kwa nini viongozi wetu hawajawahi ona hili kabisa, wakati ukisoma katika histori imejawa na movement kubwa za watu makaburu, waingereza, wahindi hawa tomeona jinsi walivyo kimbia makazi asili yao na kijisimamisha mahala pengine. Hapa sasa naona nchi sahii ya kuhamia iwe LIBYA kwa sababu wapo bize kupigana wenyewe tutumie upenyo huu kuingia kwa wingi wasichana theluthi mbili na moja iliyobakia wanaume wenye afya watanzania kama laki tano wanatosha sana kuijaza Libya ndani ya miaka michache. Nategemea serikani itatoa visa kwa haraka kufanikisha jambo hili. Hawa waliotangulia ndio wataanda mazingira ya wengine waliobaki kwenda miaka mia ijao. Na tanzania inabidi kujenga hoteli za kitalii tuu na kuacha misitu iote haina haja kuhatarisha mazingira ya mbuga zetu kwa kujenga vitu wakati wananchi wana mpango wa kuhama.

KUJITENGANISHA NA BARA LA AFRICA. Hili suala lipo kitekiniki na itabidi tufanye kwa siri ili umoja wa mataifa isijue maana madhara yake hayafamiki hili jambo halijawai fanywa. Ipo wazi kwamba bonde la ufa linasogea kidogo kidogo inakadiriwa ndani ya miaka laki moja kuna kipande mashariki mwa bonde kitajitenga na bara la Africa naturaly sasa sisi tunachotakiwa kufanya ni kufanyiza utekelezaji wa haraka katika kutanua miamba hio. Njia rahisi ni kuchimba mpaka kwenye plate zinapokutana na kutega vilupizi kwenye hili bonde mpaka somali alafu tunalipua kwa wakati mmoja hili litapelekea plate moja kusukumwa na matetemeko makubwa sana, kama zoezi halijafanikiwa tunarudia tena mpaka pale zoezi litakapofanikiwa.

Kama mlivyona na kushuhudia hili dubwana la umaskini haliepukiki mpaka pale hatua kali zidi yake zitakapochukuliwa.
 

Attachments

  • images (4).jpeg
    images (4).jpeg
    7.5 KB · Views: 4
  • images (5).jpeg
    images (5).jpeg
    45.5 KB · Views: 3
Mchagueni magufuli mwaka huu, atawaondolea jangwa la sahara muwe na maisha bora.

#Irani ya Chama...
 
Back
Top Bottom