Kwanini JamiiForums isitumiwe na mastaa wa Bongo kama wanavyotumia Facebook, Instagram kuweka mawazo yao?

Ibrahim augustine

JF-Expert Member
Nov 28, 2017
428
575
Kwa kipindi kirefu nilikua najiuliza na kutamani mastaa kutumia mtandao wa JamiiForums
Nilipenda sana kuwaona kina;
@Alikiba
diamond platnumz
wema sepetu
shilawadu
@Mr blue

*@Rais wetu*

Na wengine wengi kwani hii ni moja katika njia ya kukuza lugha yetu pia na kufanya JF ya kimataifa zaidi
Pia mastaa hao wapewe blue tick kama mitandao mingine

Lakini mastaa wengi wamejikita Facebook, Instagram na Twitter ambapo inaendeshwa na wazungu jambo ambalo sio zuri ila labda nisiwalaumu pengine labda hawaijui Jamii Forums.

Ningetamani sikumoja wa Tz wote waachane na Fb na kujiunga huku JF ingependeza sana.


Nawasilisha OVA!
 
Kwasababu hizi

Mastaa wengi wa Tanzania wanawaza chupi na wowowo, mfano diamond ana mawazo gani chanya aliwahi kutoa yakakusisimua?
Joti au mpoki wana mawazo gani ambayo we unayakosa hapa?

Wolper na sepetu wana mawazogani chanya ambayo umeona umeyakosa hapa mpaka ukaomba uwepo wao,

Nakuambia kwamba hivo hujagundua kwamba wao wanaenda sehem ambayo itakuwa rahis kuuza miili yao kwa watu wanaojulikana,

Sasa unategemea wema alete shobo zake hapa kumpata BAK tindo Lizaboni Shark Malcom Lumumba Au kumpata nani hasa?

Maana hajui kipato chao wala sura, hajui cheo chao wala kazi,

Wanasema kuwa mjanja katika kuchagua soko, na wao soko lao haliko hapa
 
huku hakuna show off " halafu wtu huwa wanalazimika kuongea vitu/kitu kwa fact "" huwezi kuthubutu kuwalisha matango pori wana JF halafu wakakuachia tu lazima wakuumbue "" utajuta kwanni uliingia kichwa kichwa " Humu hata ukipost kitu kwenye yale majukwaa ya umbea usishangae watakapo jitokeza watu wakukwambia kuwa wanataka evidence ama reference ""
JF ni makazi ya great thinkers akili ndogo not allowed here "" kina lemutuz wenyew wamepakimbia Humu ""
 
The thing is wasaanii wa bongo mawazo yao si mawazo yenye nguv ya kuhamasish amaendeleo.
Staha hawana, kutwa kujadili bifu zisizoo na kichwa wala miguu, alafu pia kujianika mitandaoni.

Wana hiitabia, mtu ameamka anapost, kaenda kuoga anapost, anakunywa chai anapost, katoka out anapost, anapata dina anapost.

Yaan maisha yao yote wamehamishia mtandaoni.

Jf hakuna mambo ya kuanika uchi, ikileta mada za kijinga unapigwa ban. Thats why?
 
Back
Top Bottom