Kwanini itakuwa vigumu Upinzani kuchukua Dola hata tukishinda katika Uchaguzi Mkuu?!

Salvatory Mkami

Senior Member
Apr 17, 2013
146
244
Nimejaribu kurudia kuisoma kwa umakini mkubwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania lakini nimeshindwa kuona mahali ambapo panatoa mwongozo au kuonyesha utaratibu wa kufuatwa pindi inapotokea chama Tawala kushindwa katika Uchaguzi Mkuu na kutakiwa kukabidhi mamlaka kwa chama cha upinzani.

Kama Katiba haionyeshi au hakuna kabisa kipendele hicho basi ni wazi kwamba haitakuwa rahisi kwa Serikali iliyoko madarakani kukabidhi madaraka kwa chama kingine chochote mbadala kwasababu Katiba haitoi mwongozo wala kuonyesha utaratibu wowote unaofafanua jambo hilo.

Mbali na mapungufu mengine ya Katiba yetu

Swali langu ni Je,

Hatuoni kwamba pungufu hilo moja ni sababu mojawapo kubwa ambayo inatoa mwanya kwa mamlaka husika iliyoshika dola kutumia nafasi hiyo kuminya demokrasia ili kuendelea kubaki madarakani kadiri itakavyowezekana?!

Katika uhalisia usio na nguo nakubali kukubaliana kwamba Katiba yetu ina mapungufu mengi sana kutokana na ukweli kwamba bado katiba yetu iko katika mfumo wa chama kimoja na si vyama vingi kama jinsi tunavyoamini, na hiyo ndio sababu kubwa iliyopelekea uhitaji wa Katiba mpya ambayo hata hivyo ilihujumiwa kwa makusudi na kundi husika kwa kujua wazi kwamba mabadiliko hayo yangeweza kuimarisha demokrasia nchini na kuweka usawa kwa vyama vyote vya siasa na kupelekea chama tawala kukosa upendeleo ambao Katiba ya sasa inautoa kwa chama kilichoko madarakani.

Ni yapi maoni yako?
 
Katiba iko wazi,mshindi ndiye atakayeunda Serikali. Mambo ya taratibu za kuachiana madaraka si ya kikatiba. Ni ya Kanuni ambazo tayari zipo.Kumbuka, mshindi wa Urais hutangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Ikiwa wapinzani watashinda Urais, hakutakuwa na tofauti yoyote ya kuachiana madaraka kati ya Rais Mstaafu Mwinyi na Mkapa;Mkapa na Kikwete;Kikwete na Rais Magufuli na kadhalika. Kimsingi, hapo hakuna mapungufu yoyote ya kikatiba.
 
Viongozi wengi wakiafrika wanatawala kihuni,hata Kama katiba haina mapungufu yoyote wanatumia katiba za vichwani mwao.
 
Katiba iko wazi,mshindi ndiye atakayeunda Serikali. Mambo ya taratibu za kuachiana madaraka si ya kikatiba. Ni ya Kanuni ambazo tayari zipo.Kumbuka, mshindi wa Urais hutangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Ikiwa wapinzani watashinda Urais, hakutakuwa na tofauti yoyote ya kuachiana madaraka kati ya Rais Mstaafu Mwinyi na Mkapa;Mkapa na Kikwete;Kikwete na Rais Magufuli na kadhalika. Kimsingi, hapo hakuna mapungufu yoyote ya kikatiba.
Mapungufu yapo kwenye Tume ya uchaguzi ambayo sio huru,hivyo inaleta warakini kama kweli huyu mwenyekiti wa hiyo tume, ambaye ni mteule wa Rais anayekuwa madarakani anaweza dhubutu kutangaza kwamba chama cha huyu Rais kimeshindwa ikiwa ataambiwa asifanye hivyo.
 
Nimejaribu kurudia kuisoma kwa umakini mkubwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania lakini nimeshindwa kuona mahali ambapo panatoa mwongozo au kuonyesha utaratibu wa kufuatwa pindi inapotokea chama Tawala kushindwa katika Uchaguzi Mkuu na kutakiwa kukabidhi mamlaka kwa chama cha upinzani.

Kama Katiba haionyeshi au hakuna kabisa kipendele hicho basi ni wazi kwamba haitakuwa rahisi kwa Serikali iliyoko madarakani kukabidhi madaraka kwa chama kingine chochote mbadala kwasababu Katiba haitoi mwongozo wala kuonyesha utaratibu wowote unaofafanua jambo hilo.

Mbali na mapungufu mengine ya Katiba yetu

Swali langu ni Je,

Hatuoni kwamba pungufu hilo moja ni sababu mojawapo kubwa ambayo inatoa mwanya kwa mamlaka husika iliyoshika dola kutumia nafasi hiyo kuminya demokrasia ili kuendelea kubaki madarakani kadiri itakavyowezekana?!

Katika uhalisia usio na nguo nakubali kukubaliana kwamba Katiba yetu ina mapungufu mengi sana kutokana na ukweli kwamba bado katiba yetu iko katika mfumo wa chama kimoja na si vyama vingi kama jinsi tunavyoamini, na hiyo ndio sababu kubwa iliyopelekea uhitaji wa Katiba mpya ambayo hata hivyo ilihujumiwa kwa makusudi na kundi husika kwa kujua wazi kwamba mabadiliko hayo yangeweza kuimarisha demokrasia nchini na kuweka usawa kwa vyama vyote vya siasa na kupelekea chama tawala kukosa upendeleo ambao Katiba ya sasa inautoa kwa chama kilichoko madarakani.

Ni yapi maoni yako?
 
Tiba ni katiba mpya, ambayo imefungiwa kabatini na fungua kuwekwa kusiko julikana.
 
Back
Top Bottom