Kwanini inatumika nguvu nyingi kumvika Rais Samia sifa na vilemba vya ukoka?

Kwanza kabisa, naweka wazi ya kwamba mimi ni mpenzi wa chama cha mapinduzi.

Pia ni mfuatiliaji mzuri wa siasa za nchi hii ,za chama cha mapinduzi na za vyama mbadala vya siasa.
Nimeiona niliweke swali hili hadharani ili wajuvi wa mambo watueleze kulikono?.
Maana sasa Nyuzi za masifa ni "too much",hii ni kumpotosha Rais Samia.

Ieleweke kwamba Rais Samia haitaji kusifiwa sifa danganya toto,Rais Samia anatimiza wajibu wake kwa mujibu wa katiba ya nchi kinachohitajika ni ashauriwe,akosolewe,aelekezwe kwa staha ya hali ya juu sana, ili kumtia moyo dhidi ya kibarua hiki kigumu sana cha kuliletea taifa utulivu na ustawi.

Ni ukweli ulio dhahiri,Rais Samia ana muda mchache sana kashika hatamu ,ni vigumu kumtolea hukumu kwa sasa.

Ifamike ,ukiacha teuzi alizofanya na mabadiliko ya baadhi ya uongozi ,ni kwamba zinduzi zote anazofanya ni za awamu iliyopita,kwa sababu chama na serikali vina mipango ya muda mfupi,kati na mrefu,yeye bado yumo ndani ya ahadi za uchaguzi iliyopita.

Ninachosubiri mimi kama mpenzi kindaki wa CCM ni mabadiliko aliyoyafanya kwenye wizara ya NISHATI,kama yataleta tija kwa taifa ama lah! na maeneo mengineo ambayo atayafanyia marekebisho kwa lengo la kuleta ufanisi.lakini kazi nyingi za serikali siku zote ni "on going process activities"

USHAURI
naomba nitoe ushauri wangu kwa Rais Samia na Serikali juu ya chanjo ya uviko 19.

Ifahamike Serikali imeandika proposals nyingi sana za kuomba fedha world bank na taasisi ya fedha ya kimataifa,aidha kujenga viwanda vya dawa ,kuchakata raslimali zetu, source of energy na mengine mengi mazuri ,lakini taasisi hizi hutosa kabisa.na maandiko hayo yanaozea huko ughaibuni.

Leo fedha za chanjo ya uviko zipo nje nje bila mashariti yoyote,

sipingi , Ni kweli kwamba afya ndio kila kitu, tujiulize kama watanzania, Uviko ndio kipaumbele chetu kwa sasa ?

Tumepewa chanjo milioni moja na marekani mpaka leo hazijaisha,china kaongeza tena .

Swali, ni watanzania wangapi kama nguvu kazi yetu hawazalishi kwa sababu ya Uviko-19? ,mpaka sasa hatuzidi watanzania milioni moja kati ya milioni 60 na ushee ambao wamechanja. je? tumeathirika pakubwa kiasi gani?,mpaka tuzamishe matrilioni ya fedha kwa kulazimishwa?,

lini kama taifa tutajisimamia na kuwaeleza hao mabwana hili hapana?

Kwa maana hiyo hii fedha ya mkopo kwa ajili ya matibabu ina riba sio ,hamuoni huko ni kulididimiza taifa ?,ni bora mikopo kwa miradi yenye ustawi kwa taifa sio haya machanjo yenu,sisi Corona tuliishinda toka enzi hayati Magufuli akiwa hai .

Viongozi wetu mnapewa dhamana ,kwa uoga wenu mnashindwa kutufikisha kwenye ahadi ya neema.ifahamike kufa mtakufa tu,ila ni bora ukafa kwa kusema kweli

Bila nyinyi viongozi kujitoa tutandelea kuburuzwa na hatutaweza kuwa huru kiuchumi daima,sana tutajaziwa misaada na kusifiwa sifa za kung'ong'wa kisogoni.

Wajinga ndio waliwao,nchi hii haitajengwa na wageni bali ni sisi wenyewe kwa kujitoa kwa hali zote ,maisha ni mapito.

RIP_Julius Kambarage
John Magufuli
Pole! The "S" - gang in action.
 
Hata kama Watanzania hawajali ugonjwa wa COVID 19, lakini wawekezaji wanaotoka nchi zingine wanajali, watu wa NGO zinazofanya kazi hapa wanajali, watalii wanajali, kwa hiyo inabidi serikali nayo ianze kujali.
Nchi hii yanakuja majizi kwa slogan ya wawekezaji
 
Naona waweke na vipaza sauti kabisa news iwe Ni moja tu amesema, ametoa, ameweka, ameongoza, anachapa kazi .....kila kitu Agandi
 
Tatizo lipo kwa anae sifiwa masifa ya uongo n akawa kimya. Wanaosifia wanafanya hivyo kwa masilahi yao wabaki madarakani tonge liende kinywani lkn hawamsidii , hawapo tayari kusema ukweli ili kubadili kwenye udhaifu.
Sijui kama utaeleweka
 
Ifamike ,ukiacha teuzi alizofanya na mabadiliko ya baadhi ya uongozi ,ni kwamba zinduzi zote anazofanya ni za awamu iliyopita,kwa sababu chama na serikali vina mipango ya muda mfupi,kati na mrefu,yeye bado yumo ndani ya ahadi za uchaguzi iliyopita.
Kwenye chama chetu usishangae wanamsifu Mama kwa mtoko wa siku hiyo, sifa za kazi nzuri huwa za kibenderabendera, uwe makini katika kung'amua vitendawili
 
mama samia anasifiwa kuliko mungu aliyeumba mbingu na ardhi ndio maana ukame umeikumba tanzania ya misifa
 
nani katumia nguvu nyingi? kuna nguvu nyingi zilizotumika kama kwa hayati?

halafu sisi hatuburuzwi wewe ndo unabuluzwa landa

kunywa sumu ufe
Mbona lugha yako ni ya kimama mama sana kulikoni?
 
Back
Top Bottom