Kwanini inasemwa kuwa mshahara wa mtu ni siri?

Kwa sababu yeye ndie aliyeùfanyia kazi.
Pia mkataba wa ajira ni baina yake na mwajiri. Mwingine yeyote sio sehemu ya mkataba.
Chukulia watumishi wa umma. Wanalipwa kwa kodi za wananchi. Wananchi hawana haki ya kujua kodi zao zinatumiwaje? Angalia kampuni yenye shareholders wengi, wenye share hawana haki ya kujua wafanyakazi wao wanalipwaje?
 
Hizo sababu hazina mashiko kisheria. Huo ni mkataba.

Vitu vingapi vinalipwa na kodi za wananchi na bado ni siri? Vifaru, ujasusi, matibabu ya viongozi nk.

Bajeti ya serikali ni matrilioni...unajua matumizi gani mpaka sasa?
 
Wakuu kwa nini inasemwa hivyo? Hii ni duniani kote au hapa kwetu tu?


Ni hapa kwetu tu, Wakubwa walikuwa wanapiga ela ndefu za mishahara ili kuficha madhambi/wizi ndipo wakaja na huo usemi kwamba mshahara wa mtu ni siri.

NB:
Ule uzi wako wa uzalishaji chuma, uulete kwenye jukwaa la habari mchanganyiko tuujadili.
 
Sababu hasa ni mishahara duni.
Hivi unadhani ingekuwaje kama notice board ya kazini kwenu ingeorodhesha mshahara wa kila mtu?
Ufisadi na wizi vingefanywa bila huruma.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom