Kwanini iendelee kuwa Quality Plaza hata baada ya kuuzwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini iendelee kuwa Quality Plaza hata baada ya kuuzwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JoJiPoJi, Mar 23, 2010.

 1. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,464
  Likes Received: 1,404
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  NIMESUBIRI kwa muda wa kutosha kuona kama yatafanyika mabadiliko ya jina la jengo la Quality Plaza ambalo miaka kama miwili hivi lilinunuliwa na taasisi ya umma katika mikataba ambayo wengi walihoji kuwa ilikuwa na utata au kugubikwa na rushwa.

  Ninafahamu na kukubali kuwa jina ni jina na nitategemea wahusika kujibu hoja yangu kwa njia nyepesi hivyo, lakini ikumbukwe kuwa jina zuri humtangaza vizuri mwenye jina.
  Jengo hilo liko katika Barabara ya Nyerere, ambayo ndiyo njia kubwa na pekee ya kuingia na kutoka Dar es Salaam, kwa wasafiri watumiao usafiri wa anga ambao ndiyo kwa kiwango kikubwa wenye kupata na kutoa taswira ya jiji letu huko nje ya nchi hasa kwa wale wageni kutoka mataifa ya nje.
  Kama huo ndio ukweli, kwa nini kumbe jina la jengo hilo liendelee kuwa lile alilochagua mmiliki wa zamani?
  Yote kwa nchi hii yanawezekana, inawezekana katika mkataba wa kuuziana, kwa makusudi kabisa kiliwekwa kifungu kinachozuia kubadilisha jina la hilo jengo.
  Hiyo haiwezi kuwa ilifanyika bila kuwapo mpango wa kitu kidogo. Jingine linalowezekana ni kwamba baada ya kuuziana, viongozi wa taasisi iliyonunua jengo hawajatambua kuwa hilo jina linawakilisha masilahi ya mmiliki wa zamani hivyo yafaa jengo lipewe jina linalotoa taswira na kuwakilisha masilahi ya umma ambao katika hali halisi na busara ya kawaida ndio unaopaswa kuwa mmiliki wa jengo hilo.
  Lakini pia inawezekana ofisa msimamizi wa mali (Estate Officer) wa taasisi hiyo kwa makusudi hajataka kuwasilisha hoja hiyo kwa uongozi ambao bado umo katika usingizi wa pono.
  Hilo jengo linaendelea kuinua hadhi ya muuzaji (investment profile) kwa gharama ya wanachama wa mfuko (PSPF) na walipa kodi wa nchi hii kwa ujumla.
  Sisi tukiwa ni binadamu, tena wenye kujihusisha na mustakabali wa nchi yetu, tuna matarajio yetu kwa jinsi mambo fulani yanavyopaswa kwenda au kutendeka.
  Hili ni mojawapo kati ya mengi mengine. Kwa hiyo, jambo lisipotokea na ikatokea kutokuwepo na maelezo ya wazi juu ya hayo, sisi tuna haki ya kutengeneza taswira ya kwetu juu ya mambo hayo.
  Hakuna anayeweza kunihoji kwa nini ninahisi kuna mbinu chafu na zinazolenga kujinufaisha binafsi kwa kutokubadilisha jina la hilo jengo ili liwe ni lile linalotoa taswira ya mmiliki mpya ambao ni umma.
  Bado wanayo nafasi ya kutupatia maelezo lakini yasiwe ya ubabaishaji, ni kwa nini hadi leo hii Quality Plaza bado haijabadilishwa jina?
  Vipo vitu vingine vinafanyika kwa wazi mno, lakini haviwasaidii mameneja wa hizo taasisi kuonekana kama viongozi makini, jirekebisheni mnadhalilisha taaluma zenu!
  Hivi karibuni nimeshangaa kusoma kwenye gazeti la Daily News, tangazo la zabuni ya uendeshaji wa jengo hilo likitajwa bado kwa jina la zamani (Quality Plaza). Kweli hii ni sahihi?
  Kinachonikera na kunitia kichefuchefu ni ukweli kwamba taasisi za umma zina ajiri wataalamu, wasomi wazuri lakini wasio makini, na wasio na uzalendo wala mapenzi kwa nchi yetu.
  Ni hao hao wanaolipwa mishahara minono na marupurupu lukuki, lakini ndio hao wanaoongoza kwa uhujumu wa masilahi ya umma.
  Wakiongozwa na bodi za wakurugenzi hujirundikia masilahi manono, ikiwa ni pamoja na mikopo isiyokuwa na riba.
  Ofisa mmoja anakopeshwa gari la sh milioni 50 kwenda juu kila baada ya miaka mitano! Lakini ni hao hao bado wanaofanya hujuma kwa nchi. Kwa nini tunawekeza kwa wahujumu wa masilahi yetu?
  Ninapenda nikiri kuwa hili suala la jina linaweza kuonekana ni jambo dogo lakini si kweli.
  Watakaodhania hivyo ninawapa pole, lakini mambo makubwa yanayoliangamiza taifa letu yametokana na kudharau kila jambo kwa kuliona ni dogo.
  Ndivyo hivyo, hata barabara zetu zinapoanza kutoboka kidogo tunadharau kuwa ni kashimo kadogo, hatufanyi matengezezo, baada ya muda barabara inakuwa haipitiki kabisa.
  Anayebisha leo hii apite ile Barabara ya Uhuru, maeneo ya Bungoni, Ilala alafu aje atueleze kama kweli ile barabara inapaswa kuendelea kuitwa hivyo kwa jinsi ilivyo katika hali mbaya.
  Umuhimu wa barabara hii hauwezi kusisitizwa. Miaka ya nyuma wageni wote kutoka nje hasa wakuu wa serikali ilikuwa ni kama ada kila wakifika nchini walipokewa na kupitishwa Barabara ya Uhuru.
  Hii ndiyo barabara inayopita mbele ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Ukweli mtu akitaka kujua jinsi tunavyothamini Uhuru wetu, apite kwenye hii barabara, ndipo atapata picha ya ni hatua gani tumeipiga tangu tumepata Uhuru.
  Huu ni mfano mmoja na mdogo. Nimetoka kidogo nje ya mada yangu lakini kwa nia ya kusisitiza jinsi ya kudharau mambo kunavyoleta hatari.
  Watanzania tubadilike, tuwe na moyo wa kuipenda nchi, dharau na kutafuna tu havitujengei misingi ya kuandaa maisha mazuri kwa vizazi vijavyo.
  Tunaoishi leo yatupasa kutambua wajibu wetu huo, tuishi tukitambua na kuthamini kuwa watakaozaliwa baadaye watambue na kufaidika na maandalizi mazuri yaliyofanywa na waliowatangulia.
  Hii sasa imekuwa ni nchi ya kila anayepata mwanya anautumia kwa kujinufaisha yeye kwa mtizamo finyu unaoongozwa na ubinafsi.
   
 2. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,464
  Likes Received: 1,404
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 3. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Uliwahi kujiuliza kabla ya kuitwa Quality Plaza lilikuwa linaitwaje na ni nani alikuwa mmiliki wake? Na je, lilijengwa kwa msamaha wa kodi chini ya TIC? Huyo mmiliki wa kwanza yuko wapi, na ana mahusiano yoyote na mmoja wa vigogo? Ukipata moja ya majibu ya maswali haya, basi hutoshangaa ni kwanini halibadilishwi jina.
   
 4. Baridijr

  Baridijr Member

  #4
  Mar 23, 2010
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaaaazi kweli, ukitaka kufuatilia hii nchi unaweza ukajikuta umepoteza uhai wako bure
   
Loading...