Kwanini idadi ya mbwa sio kubwa ukilinganisha na idadi ya mifugo kama ng'ombe?

Saguda47

JF-Expert Member
May 1, 2016
11,133
19,867
Habari zenu wakuu natumai mu wazima hakika, ila kwa wenye shida kiafya Mungu atawaponya.

Nimeleta uzi huu ili kupata ufumbuzi wa kitaalam kuhusu hili,
Kwa nini idadi ya mbwa (wawe wa mitaani au wa nyumbani) sio kubwa ukilinganisha na idadi ya mifugo kama ng'ombe? Utata uko katika hoja kama hizi:-

1. Mbwa huzaa watoto wengi kuliko ngombe (uzao mmoja).

2. Mbwa huzaa mara nyingi kwa mwaka kuliko ng'ombe lakini idadi haiwi kubwa ukilinganisha na ya ng'ombe.

3. Vifo vya ng'ombe (kuchinjwa) ni kila siku na idadi ni kubwa, lakini mbwa hawafi kila siku kwa idadi kama ya ng'ombe.

4. Ng'ombe huhitajika kuchinjwa kwa kitoweo lakini bado idadi yao ni kubwa ukilinganisha na mbwa.

5. Ng'ombe huchukua miaka mingi kukua lakini mbwa ni miezi kadhaa tu na bado mbwa wanakuwa wachache?

Mjadala uko huru wakuu ili kutegua hii paradox.
 
Ungejua kwanza ni familia ngapi zinafuga mbwa Tanzania, na ni ngapi zinafuga ng'ombe. Kwa mfano, Dar wanaofuga ng'ombe ni wengi kuliko wanaofuga mbwa, vivyo vivyo kwa miji mingi nchini. Hata ukienda usukumani na umasaini unakuta mtu ana ng'ombe 3,000 na mbwa watano.

Anyway, ngoja maafisa mifugo waje watatujuza vena.
 
Dah, umetoa logic mapema sana mkuu
 
Mbwa hula watoto pindi apatapo njaa halafu wafuga mbwa ni wachache
Sawa mkuu lakini hula wangapi? Nnavyojua mbwa hula mtoto mmoja pindi akizaa ila wengine hujitahidi kuwa kuza na hata huwatafutia chakula majalalani (kwa wasio na matunzo)
 
Back
Top Bottom