Kwanini idadi kubwa ya wanawake wasomi hawaolewi?

  • Thread starter Madam vivian original
  • Start date
Madam vivian original

Madam vivian original

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2018
Messages
404
Points
1,000
Madam vivian original

Madam vivian original

JF-Expert Member
Joined Jul 14, 2018
404 1,000
Hbr za w,keend wakuu

Najiuliza ni kwann wanawake wasomi hawaolewi, mfano: madoctor wakike, mahakimu wakike, wanasheria na hata walimu wengi was secondary hawaolewi shida nn hasa jaman

Nina marafiki zangu, na Dada zangu kadhaa ambao wamesoma lakin hawajaolewa na wanataman wapate waume wa kuwaoa

1) Huyu wa kwa kwanza ni muheshiwa hakimu anaheshimika sna ni jiran angu na best angu, hana mume ila ana mtoto na amezaa na mume wa MTU, nikamuuliza my kulikon unaishi na mume wa MTU anasema ntafanyaje sasa, wanaume wa kututongoza hakuna wengi wao wanatuogopa wanadhan tumeolewa akaniambia pale oficn waheshiwa wote hawajaolewa ni masingle mother tukacheka yakaisha hayo

2) Huyu mwingine ni doctor wangu specialist kabisaa wa mambo ya wanawake lakin hajaolewa amenunua Pete ya ndoa ameivaa utadhan kaolewa kumbe hajaolewa, ktk story story anasema hajaolewa na ana watoto wake wawili kamaliza, anakula maisha kinikamuuliza VP haumiss kuwa na familia anasema nataman hata kesho lakin tunaogopeka wanatuona high class.

Hao ni baadhi tu ambao nawafaham, ninakutana nao kwenye vikoba na kanisan ni wengi na wanamaisha mazuri najiuliza shida ni nn mbona warembo na wanaonekana wife material kakazangu mnakwama wapi,

Kwakweli namshukuru Mungu niliolewa cjui namm ningekua kwenye hz stress.

Shida nn wanawake wasomi hawaolewi wanaishia kuwa single mother's. Wapo wengi humu tujadili tuweze kuwasaidia Dada zetu wanakwama wapi.
 
Karma

Karma

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Messages
8,971
Points
2,000
Karma

Karma

JF-Expert Member
Joined May 20, 2019
8,971 2,000
Wanawake waliosoma wanaponzwa na
1. Ujuaji
2. Kiburi
3. Dharau
4. Ujeuri

Kiufupi hawaoleki, na ukiwaoa watakusumbua sana mpk utajuta.. Inaaminika kuwa kadri mwanamke anavyoongezeka elimu ndvyo anavyozid kuwa mjinga.. Na anapoteza sifa kabisa ya kuwa mke... WACHACHE SANA HASA WALE WALIOLELEWA KTK MISING MIZURI YA DINI NDYO HUOLEWA NA KUDUMU, KWA SABABU WAMEWEKA MBELE MISING YA ELIMU YA DINI KULIKO MISING YA ELIMU YA DUNIA..
Mkuu, bila shaka mnaposema mwanamke anavyozidi kuelimika ndivyo anavyozidi kuwa mjinga mnamaanisha kwamba ndiyo anazidi kufunguka akili kuhusu unyanyasaji wa mwanaume kitu ambacho ninyi hamtaki mwanamke awe aware nacho ndiyo maana mnaona kama kuelimika kwao ni tatizo.

Imagine mwanaume anataka akichepuka mke wake asimuulize chochote bali avumilie tu kitu ambacho hata mwanaume hawezi kukifanya endapo mke wake akichepuka, mwanaume anataka akichelewa kurudi nyumbani mke wake asimuulize chochote avumilie tu kitu ambacho hata mwanaume hawezi kukifanya endapo mke wake akichelewa kurudi nyumbani.

Kuna wanaume wengi tu huwa nawasikia wanasema eti "kuoa mwanamke asiye na elimu raha sana yaani unamdanganya tu kwamba unasafiri unaenda kufanya (anataja neno lolote la kiingereza hapa ambalo anajua mke wake hatalielewa) halafu mke anakubali tu kumbe unaenda kwa mchepuko unashinda naye wiki nzima", sasa hebu ona tu ni jinsi gani huyo mwanaume anavyojisifia upumbavu.

Tunajua wanaume wengi wanapenda kuoa wanawake wasio na elimu sababu wanawake wa aina hiyo hawana uwezo wa kuhoji chochote hata kama ni haki yao maana wanachojua wao ni kwamba mwanaume ni mungu akikosea hatakiwi kuambiwa chochote anatakiwa kuchekewa na kuachwa afanye anachotaka hata kama anachofanya ni kosa, lakini mwanamke akikosea anatakiwa apigwe au atalikiwe.
 
Karma

Karma

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Messages
8,971
Points
2,000
Karma

Karma

JF-Expert Member
Joined May 20, 2019
8,971 2,000
Ukisoma huu uzi, utagundua kwanini wanawake wasomi asilimia kubwa hawaoleki, uzi umejaa ushndani wa mwanaume vs mwanamke.. Imagine ushndani huu ndo uhamie ndani ya nyumba, si itakuwa balaa, kwa hyo wanawake wasomi wakiwa kwenye wanashndana na waume zao.. Yan ful ujuaj
Swala siyo kushindana ila tuambiane ukweli kwanini wanaume mjihalalishie makosa??

Halafu sijui kwanini mnapenda kutumia hiyo kama sababu yaani mfano eti mwanaume kuchepuka ni sawa na mwanamke hatakiwi kusema chochote eti kwa sababu tu mwanamke hatakiwi kushindana na mwanaume??
 
Kee_tah

Kee_tah

Member
Joined
Feb 26, 2019
Messages
62
Points
150
Kee_tah

Kee_tah

Member
Joined Feb 26, 2019
62 150
Wakaka wengi walio comment humu wana insecurity balaa....sijui ndio ile fragile ego ya wanaume.

Kama mwanaume unaona hutaweza kuoa mwanamke aliyesoma na mwenye kazi nzuri basi oa huyo ambaye hajasoma na hana kazi nzuri. Kila mtu afanye analoweza.

Halafu wakaka wengi hawapendi wanawake wenye elimu maana sio rahisi kuwa control plus anakua na ile logical thinking ya kum challenge mwanaume.

Mimi naona mwanaume ukiweza kuwa a provider, protector na an authoritative figure in a relationship hakuna mwanamke anaweza kukuzingua hata awe na elimu vipi.
 
Kee_tah

Kee_tah

Member
Joined
Feb 26, 2019
Messages
62
Points
150
Kee_tah

Kee_tah

Member
Joined Feb 26, 2019
62 150
Wanawake waliosoma wanaponzwa na
1. Ujuaji
2. Kiburi
3. Dharau
4. Ujeuri

Kiufupi hawaoleki, na ukiwaoa watakusumbua sana mpk utajuta.. Inaaminika kuwa kadri mwanamke anavyoongezeka elimu ndvyo anavyozid kuwa mjinga.. Na anapoteza sifa kabisa ya kuwa mke... WACHACHE SANA HASA WALE WALIOLELEWA KTK MISING MIZURI YA DINI NDYO HUOLEWA NA KUDUMU, KWA SABABU WAMEWEKA MBELE MISING YA ELIMU YA DINI KULIKO MISING YA ELIMU YA DUNIA..
Ina maana hakuna wanawake ambao hawajasoma na hawana hizo tabia au?

Ukiona mwanamke ana display hizo tabia kwako muache aende zake atakutana na mtu anayewezana naye huko mbeleni.

Shida wanaume mkiwa challenged kidogo tu mnahisi kama mnadharuliwa sijui. Au maybe lugha zinazotumika kuwa challenge ndio ambazo hamzipendi? Maana kama unakaa na mtu asiyeku challenge kuna uwezekano mkubwa usipige hatua kimaisha na kiakili pia
 
Kee_tah

Kee_tah

Member
Joined
Feb 26, 2019
Messages
62
Points
150
Kee_tah

Kee_tah

Member
Joined Feb 26, 2019
62 150
Tatizo akili yako inashindwa kuchambua mambo. Mwanamke anayejilinganisha na mwanaume ni dalili ya ushetani. Halikadhalika na mwanaume anayejilinganisha na Mwanamke.

Uchafu wa mwanaume nni tofauti na uchafu wa mwanamke ndio maana hata kwenye kutakasa kwenye Biblia ni kuwa mwanaume anajitakasa kwa siku saba wakati mwanamke ni siku kumi na nne.

Sasa unadhani kwa nini Mungu aone uchafu kwa mwanaume unaondoka kwa siku saba wakati mwanamke siku kumi na nne.
Unajua men and women are equal but not the same. We are very different from one another, na hizo tofauti zetu should not be perceived as weakness. Men and women work best if they complement each other instead of competing with each other.

Shida ni ile kutaka kuonekana kundi fulani liko sawa na kundi lingine limekosea. We could both be right and be wrong at the same time.

Kuhusu suala la wanawake kupewa muda mrefu kujiswafi kwenye biblia nahisi ni sababu ya hedhi na vitu kama hizo. Ila sio sababu ya kusema mtu ni mchafu sababu kapewa muda mrefu wa kuji swafi.
 
Mkaruka

Mkaruka

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Messages
11,262
Points
2,000
Mkaruka

Mkaruka

JF-Expert Member
Joined Feb 5, 2013
11,262 2,000
Wanawake automatically wana roho mbaya ndani kwa ndani.

Ni Kama Tulivyo Watu Weusi.

Laiti Kama Wangekuwa Na Nguvu Fulani Ambayo Wanaume Wanaoonekana Kuwa Nayo,

Dunia Ingekuwa Mahali Pabaya Zaidi Kuishi Kwa Wanaume
 
Equation x

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Messages
7,959
Points
2,000
Equation x

Equation x

JF-Expert Member
Joined Sep 3, 2017
7,959 2,000
Nadhani mazingira ya chuo yaliwafanya kuwa na wanaume wasiokuwa na malengo ya ndoa,mwisho wa siku wanajikuta wamepotezewa muda.
 
PETER PIERE

PETER PIERE

Member
Joined
Mar 8, 2013
Messages
83
Points
150
PETER PIERE

PETER PIERE

Member
Joined Mar 8, 2013
83 150
Kee_tah na Karma tunavyosema kuwa mwanamke kadri anavyozid kusoma anazid kuwa mjinga, mjuaji, kiburi na dharau hatumaanish kwenye dhana ya kumchalenge mwanaume la hasha..

Wanawake weng waliosoma wanaleta harakati ktk ndoa.. Majukumu yake kama mke anaona kama hayamhusu mfano
1. Anaamka muda anaojisikia
2. Kumfulia nguo mumewe anaona cyo wajibu wake, yey msomi
3. Kumpa mapenz mumewe anaona cyo lazma
4. Anaona ana uhuru wa kumjbu mumewe anavyojiskia, iwe vzur au vbaya
5. Kupika na kaz nyumban anaona cyo muhmu afanye yey, hata mume afanye
6. Hawajui namna ya kuzungumza na mume yan ful roporopo na ujeuri.. Kiufupi hawana maner, ndan ya nyumba matokeo yake hajulikan mke wala mume.. Kila unalomwelekeza ni mwendo wa kujbu vbaya tu na hawez kumskiliza mume..

Jeuri yote hii inatokana na wanachodai kuwa, wamesoma na wana kaz hvyo hawez kuwa chn ya mtu...
 
Devion

Devion

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Messages
1,091
Points
2,000
Devion

Devion

JF-Expert Member
Joined May 29, 2018
1,091 2,000
Swala siyo kushindana ila tuambiane ukweli kwanini wanaume mjihalalishie makosa??

Halafu sijui kwanini mnapenda kutumia hiyo kama sababu yaani mfano eti mwanaume kuchepuka ni sawa na mwanamke hatakiwi kusema chochote eti kwa sababu tu mwanamke hatakiwi kushindana na mwanaume??
Edelyn mbona unabadili badili sana majina

Edelyn-Mariana- Karma

Kwa taarifa yako tunakujua...comment zako hazijifichi
 
Karma

Karma

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Messages
8,971
Points
2,000
Karma

Karma

JF-Expert Member
Joined May 20, 2019
8,971 2,000
Edelyn mbona unabadili badili sana majina

Edelyn-Mariana- Karma

Kwa taarifa yako tunakujua...comment zako hazijifichi
Wewe na nani mkuu?? Mbona wenzio wengi wanajua tangu muda mrefu na mimi ndiye niliyewaambia?? Sema wewe ndiyo ulikuwa haujui au ulitaka hadi nikuombe ruhusa ya kubadili username?? Kuwa mpole!!
 
Karma

Karma

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Messages
8,971
Points
2,000
Karma

Karma

JF-Expert Member
Joined May 20, 2019
8,971 2,000
Kee_tah na Karma tunavyosema kuwa mwanamke kadri anavyozid kusoma anazid kuwa mjinga, mjuaji, kiburi na dharau hatumaanish kwenye dhana ya kumchalenge mwanaume la hasha..

Wanawake weng waliosoma wanaleta harakati ktk ndoa.. Majukumu yake kama mke anaona kama hayamhusu mfano
1. Anaamka muda anaojisikia
2. Kumfulia nguo mumewe anaona cyo wajibu wake, yey msomi
3. Kumpa mapenz mumewe anaona cyo lazma
4. Anaona ana uhuru wa kumjbu mumewe anavyojiskia, iwe vzur au vbaya
5. Kupika na kaz nyumban anaona cyo muhmu afanye yey, hata mume afanye
6. Hawajui namna ya kuzungumza na mume yan ful roporopo na ujeuri.. Kiufupi hawana maner, ndan ya nyumba matokeo yake hajulikan mke wala mume.. Kila unalomwelekeza ni mwendo wa kujbu vbaya tu na hawez kumskiliza mume..

Jeuri yote hii inatokana na wanachodai kuwa, wamesoma na wana kaz hvyo hawez kuwa chn ya mtu...
Sasa mkuu hiyo hoja ya mwanamke kumkosea heshima mume wake hiyo ni hulka na tabia tu ya mtu na haihusiani na kusoma wala kutokusoma mimi ninawajua wanawake waliosoma na wana heshima na vile vile ninawajua wanawake wasiosoma na wana jeuri!!

Kuhusu majukumu mimi naona inategemea kama mwanamke ana kipato au la lakini hata ninyi wanaume nanyi msiwe wabinafsi muwe mnafikiria sasa kama mke wako anakusaidia majukumu yako wewe unaona ubaya gani kumsaidia majukumu yake muwe na huruma jamani hata wanawake nao wanachoka yaani mahitaji ya nyumbani mtoe wote watoto msomeshe wote ila kazi za ndani na kulea watoto afanye mke peke yake kweli??
 
rikiboy

rikiboy

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Messages
11,422
Points
2,000
rikiboy

rikiboy

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2017
11,422 2,000
Sasa mkuu hiyo hoja ya mwanamke kumkosea heshima mume wake hiyo ni hulka na tabia tu ya mtu na haihusiani na kusoma wala kutokusoma mimi ninawajua wanawake waliosoma na wana heshima na vile vile ninawajua wanawake wasiosoma na wana jeuri!!

Kuhusu majukumu mimi naona inategemea kama mwanamke ana kipato au la lakini hata ninyi wanaume nanyi msiwe wabinafsi muwe mnafikiria sasa kama mke wako anakusaidia majukumu yako wewe unaona ubaya gani kumsaidia majukumu yake muwe na huruma jamani hata wanawake nao wanachoka yaani mahitaji ya nyumbani mtoe wote watoto msomeshe wote ila kazi za ndani na kulea watoto afanye mke peke yake kweli??
Mwanamke ukimsaidia majukumu yake anahisi ni wajibu wakoo...!! Dharau zinaanza aisee bora kuwa dikteta
 
Ulweso

Ulweso

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2016
Messages
12,405
Points
2,000
Ulweso

Ulweso

JF-Expert Member
Joined May 24, 2016
12,405 2,000
Mkuu, bila shaka mnaposema mwanamke anavyozidi kuelimika ndivyo anavyozidi kuwa mjinga mnamaanisha kwamba ndiyo anazidi kufunguka akili kuhusu unyanyasaji wa mwanaume kitu ambacho ninyi hamtaki mwanamke awe aware nacho ndiyo maana mnaona kama kuelimika kwao ni tatizo.

Imagine mwanaume anataka akichepuka mke wake asimuulize chochote bali avumilie tu kitu ambacho hata mwanaume hawezi kukifanya endapo mke wake akichepuka, mwanaume anataka akichelewa kurudi nyumbani mke wake asimuulize chochote avumilie tu kitu ambacho hata mwanaume hawezi kukifanya endapo mke wake akichelewa kurudi nyumbani.

Kuna wanaume wengi tu huwa nawasikia wanasema eti "kuoa mwanamke asiye na elimu raha sana yaani unamdanganya tu kwamba unasafiri unaenda kufanya (anataja neno lolote la kiingereza hapa ambalo anajua mke wake hatalielewa) halafu mke anakubali tu kumbe unaenda kwa mchepuko unashinda naye wiki nzima", sasa hebu ona tu ni jinsi gani huyo mwanaume anavyojisifia upumbavu.

Tunajua wanaume wengi wanapenda kuoa wanawake wasio na elimu sababu wanawake wa aina hiyo hawana uwezo wa kuhoji chochote hata kama ni haki yao maana wanachojua wao ni kwamba mwanaume ni mungu akikosea hatakiwi kuambiwa chochote anatakiwa kuchekewa na kuachwa afanye anachotaka hata kama anachofanya ni kosa, lakini mwanamke akikosea anatakiwa apigwe au atalikiwe.
Wawaoe hao hao mbulula, kama hawataki walioeda shule haina shida,
kuna mikoa binti mwisho la saba kisha unyago wakawachukue tu, pia na wao kbinti zao wasiwapeleke shule ili waolewe tu halafu wanaochonga sana wasomeshwa na mama zao ambao baba zao walikimbia majukumu na kwenda kwa michepuko
 
Prisoner of hope

Prisoner of hope

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2017
Messages
2,392
Points
2,000
Prisoner of hope

Prisoner of hope

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2017
2,392 2,000
Kee_tah na Karma tunavyosema kuwa mwanamke kadri anavyozid kusoma anazid kuwa mjinga, mjuaji, kiburi na dharau hatumaanish kwenye dhana ya kumchalenge mwanaume la hasha..

Wanawake weng waliosoma wanaleta harakati ktk ndoa.. Majukumu yake kama mke anaona kama hayamhusu mfano
1. Anaamka muda anaojisikia
2. Kumfulia nguo mumewe anaona cyo wajibu wake, yey msomi
3. Kumpa mapenz mumewe anaona cyo lazma
4. Anaona ana uhuru wa kumjbu mumewe anavyojiskia, iwe vzur au vbaya
5. Kupika na kaz nyumban anaona cyo muhmu afanye yey, hata mume afanye
6. Hawajui namna ya kuzungumza na mume yan ful roporopo na ujeuri.. Kiufupi hawana maner, ndan ya nyumba matokeo yake hajulikan mke wala mume.. Kila unalomwelekeza ni mwendo wa kujbu vbaya tu na hawez kumskiliza mume..

Jeuri yote hii inatokana na wanachodai kuwa, wamesoma na wana kaz hvyo hawez kuwa chn ya mtu...
Peter leo unanifurahisha sana!! Unatema logics tupu.....big up chief!
 
Ulweso

Ulweso

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2016
Messages
12,405
Points
2,000
Ulweso

Ulweso

JF-Expert Member
Joined May 24, 2016
12,405 2,000
Swala siyo kushindana ila tuambiane ukweli kwanini wanaume mjihalalishie makosa??

Halafu sijui kwanini mnapenda kutumia hiyo kama sababu yaani mfano eti mwanaume kuchepuka ni sawa na mwanamke hatakiwi kusema chochote eti kwa sababu tu mwanamke hatakiwi kushindana na mwanaume??
Hata cha maana hakuna, watoto wao wakiwa na tabia za umalaya hapo hapo anasingiziwa mama , na wakipata maradhi ndiyo aakwanza kunywa dawa kimya kimya wakati mwingine Mungu huwaona wanawake kama wahanga
 
Forum statistics

Threads 1,342,652
Members 514,741
Posts 32,758,759
Top