Kwanini ibada kila imani zinahusisha sana viumbe kuliko Muumba?

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,697
Umakini flani kuelekezwa kwenye Viumbe badala ya Muumba, hili suala limekaaje?

1:Sanamu ya Mbao au Udongo kwenye mambo ya ibada.
2:Umakini mkubwa kupelekwa kwenye Mwezi, Nyota jua.
4:Kwa dini za kiafrika Miti.
5:Mawe
6:Wahindi Ng'ombe
7:Wengine Milima
8:Mwanadamu mwenzao wanaomuaminia sana.

Kitu chochote chenye sura ya kuvutia au kisicho cha kawaida kinaweza kugeuzwa kionjo chenye kuchukua umakini wa waabudu kwenye ibada zetu waafrika, zilizotoka Uarabuni na Uyahudi?

Maoni yangu: Wakati mwingine husuda kwa viumbwa huhafifisha hamasa ya utii kwa Mungu.

Nini maoni yako.
 
Unajua kuna utofauti kati ya mapambo ya sanamu/vitu na kuabudu vitu.... Kama ndugu mto uzi wewe ni muumini wa dini za kikristo na umeisoma biblia vizuri haswa agano la kale.... Kuna wakati wana wa israel waliambiwa wajenge hekalu nadhani ni katika kitabu cha wafalme ambacho kinaelezea mambo ya mfalme solomoni ambapo Mungu aliwaambia wajenge sanamu mbili ndani ya hekalu kama mapambo....

Nataka kukuelewesha tu kuwa kuchonga msalaba wa mbao au kuweka picha ya yesu kanisani sio dhambi.... Ila kitendo cha kuabudu ile picha/kuamini ile picha ndo mungu wako ndo dhambi...lakini ikitumika kama mapambo tu sio dhambi.... Na ndio wana wa israel waliuawa kwakuwa walijichongea ndama na kuanza kuiabudu.... Lakini wakati wanajenga hekalu enzi za mfalme solomoni waliambiwa wajenge sanamu mbili zenye mabawa waziweke kwenyw nyumba ya kuabudi na Mungu mwenyewe....

Katika dini yangu mimi tunaweka picha za yesu na misalaba kanisani ili kumjengea muumini taswira kuwa yuko kwenye nyumba ya ibada... Hata kama ikitokea kapitiwa lakini akiona picha ya yesu/msalaba pale itamsaidia kumrudisha katika hali ya ibada....

LAKINI HATUABUDU SANAMU HATA KIDOGO....
 
UMAKINI UKIPELEKWA KWA PAMBO NDIO HOJA YANGU MKUU.
Au kwa nini Watu wakimuasi Mungu, mara nyingi huwa wanakimbilia kwenye VIUMBWA na KUMUACHA MUUMBA?
Mfano, Wale jamaa Musa alipochelewa wakaamua Kutengeneza Ndama...
 
Kwanza eleza unasoma darasa la ngapi?
Haya mambo yana levels of thinking and understanding!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom