Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,226
- 26,048
Amani iwe nanyi wadau
Kama mada inavyojieleza hapo juu, hizi ndo sababu za Kwa nini Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu ndo uchaguzi Mgumu zaidi kwa CCM?
1. Mwaka 2015 Chadema walikuwa na mgombea aliyependwa na watu Lowassa Ila hakuwa mgombea makini
CCM waliweza kumchafua sana Lowassa kutokana na kashfa zakena madhaifu yake. Mwaka huu Chadema hawajarudia makosa 2020. Wana mgombea makini sana Tundu Antiphas Lissu mwenye akili sana na uwezo mkubwa sana kama mwanasiasa. Wengikwa uwezo wake wa akili na kujenga hoja wanamfananisha na Mwl Nyerere pamoja na Oscar Kambona ambao ndo wanachukuliwa kama wanasiasa bora zaidi kuwai kutokea Tanzania.
2. Mgombea wa CCM kuyaumiza makundi mengi isivyo kawaida katika kipindi chake cha miaka 5
Ni ukweli ulio dhahili kuwa kila kundi katika nchi hii limeguswa vibaya sana kwenye awamu ya tano, hali ya uchumi na kodi mbaya za TRA zimeathili sana wafanyabiashara, wafanyakazi kutopandishwa mishahara kwa miaka 5, Wakulima wa mazao kama korosho, mbaazi, tumbaku, kahawa na mahindi kuharibiwa masoko yao kwa amri za serikali pamoja na kundi kubwa la vijana kukosa ajira kutokana na uchumi kutokuwa vizuri. Kufunguliwa makesi kwa wanaharakati na watu wanaompinga magufuli pia
3. Awamu ya Tano kutokuwa na mahusiano mazuri na wadau wa maendeleo wa Tanzania wa miaka yote
Hili hata mtu asiye na akili ameliona. Katika awamu ya tano ndo Tanzania imesemwa vibaya zaidi kimataifa na hata kutolewa matamko mbalimbali yasio mazuri na ya tahadhari na balozi za hapa nchini. Hiki ni kiashiria kuwa hata wadau wa kimataifa wamemchoka Magufuli
4. Lissu kuwa Mhanga wa Jaribio la Mauaji
Hii kete ingawa CCM wanaidharau ila hili ni moja ya jambo linalombeba sana Lissu. Watu wengi wanamuona Lissu kama muujiza unaotembea. Shambulio dhidi yake tena kwenye awamu ya Tano linamfanya awe rahisi kueleweka kwa watu na hata watu kumpenda zaidi.
5. Hali ya uchumi
Hali ya uchumi ya Tanzania imekuwa mbaya sana hasa kwa watanzania. Wengi maisha yao yamezidi kuwa magumu zaidi ukiangalia kama wakulima, wafanyakazi na vijana. Hawaoni ahueni mbele na wengi wanaona ni ngumu hali hii Kubadirika kwa aina ya utawala wa magufuli
Nimalize kwa kusema, katika survey yangu Kuna jambo kuu nimeliona. Kuna uwezekano mkubwa sana Watanzania wakaandika historia kuu mwaka huu. Tundu Antiphas Lissu anaenda kuishangaza dunia mwaka huu.
Raisi wa Jamhuri ya Muungano Tanzania 2020-2025 ni Tundu Antiphas Lissu.