Kwanini hotuba za viongozi hazina mvuto siku hizi?

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,332
2,000
Zaman enz za mwalim kiongoz wa nchi akitaka kuongea na halaiki yeyote wananchi tulikua tunakua na antention kubwa sana. Hata kipindi cha mkapa kidogo pia hotuba zake na matamko yake yalikua na nguvu kidogo. Lakn siku hz hotuba za viongoz sion mvuto wake, kias cha kuogopesha wananchi au kufundisha raia. Zaid tunazijadili kwa kuzikosoa.Zaman ukisikia rais anataka kuongea na wananchi unakimbilia kwenye tv usikie kaongea nn. Enzi za mwalimu tulikua tunawasha radio.

Mwalim nyerere hotuba zake mpaka leo tunazinukuu na kukumbuka zilitolewa lini na wap. Kauli za waziri mkuu Molinge sokoine tunazikumbuka zilivo watiisha watu kias cha kutupa fedha barabaran. Tunakumbuka kauli ya mrema enzi hizo akiwa hai kiutendaji majambaz wamewahi kurudisha siraha.sasa tuje kwa hawa wa leo.

Hotuba za viongoz wa leo sion zikiwa na mvuto kama za zaman. Zaid tunaona makosa mengi katka hotuba zao. Mkuu wa mkoa zaman akiongea tulikua tunatii. Kwamm niliye hapa dar mkuu wetu karibu kila siku anatoa matamko sion matokeo yake wala uzito unaochukuliwa na wananchi.kwamba wananchi siku hizi sio watiifu?? Zaid tunajadili kauli zenye utata zinazotolewa naye.
Hata mkuu wa nchi sion atention kwa wananchi kutaka kusikia kaongea nn ili wazifuate, ila tunaangalia kaongea nini kimakosa ili tumkosoe. Kwa mfano jana anawaambia police kupewa 5000 sio rushwa ile ni ya kubrashia kiatu.kauli tata yenye kueneza rushwa badala ya kupiga vita rushwa. Maana rushwa ndogo ndogo ndio kero kubwa kwetu wananchi wa hali ya chini.

Mkuu wa mkoa alitoa agizo siraha ziandikishwe upya ikiwa ni pamoja na kusalimisha zisizo na vibali sijaona hata moja ikisalimishwa. Huyu katoa matamko mengi sion hata moja likikamilika na kufuatwa na raia wake, kwanini? nenda kwa mawaziri nenda kwenye secta mbali mbali.

Swali, kwanini hotuba zao na kauli zao mbalimbali zimekosa mvuto??
 
jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,592
2,000
Siku hizi Ni afadhali usikilize mazungumzo baada ya habari kuliko hotuba za viongozi wetu. Yaani ni full ubabe, kejeli, majigambo na makidai kibao.

Kuna waziri toka ateuliwe kazi yake ni kukimbizana na dokta mwaka kama paka na panya.
 
chikutentema

JF-Expert Member
Dec 10, 2012
7,394
2,000
Sababu in nyingi kama ifuatavyo;-
1. Hotuba za kejeri kwa watu wasio wa vyama vyao bila kujua sio wote ni Ccm.
2. Sio viongozi wa kifalsafa(philosophical leader). Wengi wanaingia siasani kwa njaa.
3. Matendo yao hayaendani na wanachokisema.
4. Ubabe wa viongozi wa Afrika.
Etc.
 
Gefu

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
6,935
2,000
....viongozi wenyewe hawana mvuto, wanachoongea kitakuwaje na mvuto....
 
Mechanist

JF-Expert Member
Jan 31, 2015
724
500
Hotuba za viongozi zinaonekana kupoteza mvuto kutokana na idadi ya illiterates kupungua ukilinganisha na miaka ya nyuma. Hao unaowasifia walikuwa na hotuba nzuri ilikuwa ni katika kipindi chao, wakirudi katika uongozi kipindi hiki nao watakosolewa tu. Hata hivyo matatizo ya watanzania kamwe hayawezi tatuliwa na hotuba zenye mvuto. Hotuba zaweza kuwa na mipango na mikakati mingi tu mizuri lakini utekelezaji ukawa zero.
 
So maoni yako siku hiz viongoz wetu hotuba zao hazina mvuto na zina ukakasi ila mipango yao inatekelezeka kuliko hotuba zao??
 
Malilambwiga

JF-Expert Member
Jul 19, 2015
485
500
Ufahamu wako mdogo wa kuchanganua mambo ndiyo unakufanya uone hotuba za viongozi leo hazina mvuto. Kama siyo hilo basi pengine unachotarajia kizungumzwe na viongozi hao hakijasemwa na muda wake bado. Nikutie moyo tu hakuna kipindi ambacho hotuba za viongozi zina mvuto kama sasa. Fuatilia kila neno analotamka JPM hakika utabarikiwa.
 
Amanijua

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
1,714
2,000
Mkuu wa mkoa anaita vyombo vya habari anaanza kuongea pumba tupu.

RC's and DC's hawana mashiko tena maana hata uteuzi wao ni kama kulipana fadhila.

Kama unamteua MTU kuwa DC kwa kutaka kumpiga mzee Warioba unategemea huyo mtu atafanya lolote la maana.
 
tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,332
2,000
Ufahamu wako mdogo wa kuchanganua mambo ndiyo unakufanya uone hotuba za viongozi leo hazina mvuto. Kama siyo hilo basi pengine unachotarajia kizungumzwe na viongozi hao hakijasemwa na muda wake bado. Nikutie moyo tu hakuna kipindi ambacho hotuba za viongozi zina mvuto kama sasa. Fuatilia kila neno analotamka JPM hakika utabarikiwa.
Asante ndugu. Lakn sidhan kama atention ya raia ya kutaka kusikia mkuu wao kaongea nn ili waitekeleze imekua kubwa siku hz kuliko zaman yaan sidhan. Nitaamini pale kauli ya raisi ikitekelezwa ya mwalimu kukatwa mshahara mwanafunzi akipasua dawati.
Ukisikia hilo niite nimi nitaitika
 
Malilambwiga

JF-Expert Member
Jul 19, 2015
485
500
Asante ndugu. Lakn sidhan kama atention ya raia ya kutaka kusikia mkuu wao kaongea nn ili waitekeleze imekua kubwa siku hz kuliko zaman yaan sidhan. Nitaamini pale kauli ya raisi ikitekelezwa ya mwalimu kukatwa mshahara mwanafunzi akipasua dawati.
Ukisikia hilo niite nimi nitaitika
Tulikuwa na taifa ambalo lilikosa usimamizi ktk idara na sekta zote za umma ndiyo maana mambo yalikwenda shagalabagala. Kauli ya Rais kuwataka walimu wakatwe mishahara pindi mwanafunzi akivunja dawati lengo lake ni kuwafanya walimu wayasimamie madawati husika kwani wakati mwingine wanafunzi hufanya michezo juu ya hayo madawati na hivyo kupelekea kuharibika mapema.

Uwezo wako mdogo wa kuchanganua mambo ndiyo maana ukashindwa kuitafsiri kwa vitendo kauli ya Rais. Itoshe tu nikwambie kwamba hata wewe nyumbani kwako pengine unao watoto, na kuna makatazo fulani unayaweka watoto wasichezee vitu fulani au maeneo fulani, lengo lake ni kuweka usimamizi mzuri.

Mbali na shuleni kila mtu hujifunza kwa mwenzake au kwenye jamii inayomzunguka. Endelea kujifunza.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom