Kwanini hotuba za Mwinyi Hazirudiwi? Vipi za Nyerere kuelekea Oktoba?

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,276
8,820
Tumebakiza miezi kadhaa tuingie kwenye uchaguzi wa rais wabunge na madiwani,Ila kuna jambo moja nimejiuliza ni kwanini Tv stations zetu hazirudii hotuba za mwalimu Nyerere?Ambazo kimsingi ni za muhimu kwa kipindi hiki wananchi wanaenda kufanya maamuzi ya kuchagua kiongozi wao wa taifa.

Hotuba zile zingewafungua vijana wengi ambao hawakumjua mwalimu na hawakujua alifikiri nini juu ya taifa hili haswa kwa kizazi hiki cha sasa,Yupo pia mzee Mwinyi huyo binafsi sijawahi kushuudia hotuba zake zikirudiwa popote.

Nimejiuliza ina maana mzee mwinyi hakuwa na speech zenye shibe?Au alitoa hotuba za mrengo mmoja?Nazo kama zipo ziwe zinarudiwa kwa faida ya watanzania.

Mzee mkapa na Kikwete hotuba zao nina imani zitatumika miaka ijayo may be 2035 na zitawafunza watanzania wa kizazi cha wakati huo.

Ni vema tujikumbushe hotuba za wazee wetu,Tupate maneno yenye hekima na busara,Hazikurekodiwa ili ziifadhiwe kwenye makumbusho zilirekodiwa kwa sababu maalum tuzitumie kujifunza.
 

lutemi

JF-Expert Member
Dec 24, 2013
1,731
1,340
Kwani nae alikuwa Rais? ???? Mbona sijui jaman. Au kiongozi ambae hakuwa na vision yeyote? Hivi anaweza kukumbukwa kwa lipi?
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom