Kwanini hili Jukwaa ushawishi wa Wanawake upo juu?

Drone Camera

JF-Expert Member
Jul 25, 2017
14,007
13,799
Habari wana MMU

Mimi si mpenzi wa hili jukwaa ila ndani ya masaa 24 huwa siachi kutupia jicho huku.

Swali langu ndo hilo kama linavyosomeka kwenye heading,wanawake wana ushawishi zaidi kwenye hili jukwaa kuliko Sie.Ukitaka kuamini hili,anzisha uzi unaofanana maudhui na mwanamke hili jukwaa halafu utaona upi utakaotembea;wako ukiwa page ya pili,wake utakuwa page ya saba.Au fanya hivi nenda lile jukwaa la love connect kisha uone nyuzi za kina nani ndo zinatembea sana.

Halafu kuna hiki kitu,ID ya kike kusingiziwa kuwa ya kiume,sijui wanaangalia vitu gani kujaji mi sijui.Ila honest Mimi sijawahi ona humu ID ya kiume inasingiziwa kuwa ni ya kike.

Kitaani kwetu ratio ya Mwanaume kwa mwanamke ni 40:60. Ila hili jukwaa nadhani ni 90:10 Kuna dunia ya peke yake humu.

Nawasilisha.
 
Kasome habari za
Adamu na Hawa,
Samsoni na Delila,
Daudi na mke wa Uria Mhiti
Na wengineo Utaelewa,

Comment tayari.
 
Wanawake wanapenda sana story, udaku,utani huwa hawapendi sana vitu vyakuumiza kichwa ndio maana kwenye jukwaa la siasa au tech nk.. wachangiaji niwachache sana huwa wanapenda vitu simple wao sio watu vyakuumiza sana kichwa na hili ndio jukwaa lao pendwa.
 
Inategemea ntu na ntu mkuu!!
Kuna jamaa anaitwa mshana, mwingine Hazard na wengine wenye ushawishi nyuzi zao huwa zinapepea balaa!!
Hao ni mmoja mmoja boss...ila Mimi nimelinganisha kwa makundi;kundi la KE na ME
 
Si mnasemaga kuwa "Mwanamke ndo anarun dunia" ?!

Wacha waturun tu mkuu. Kwanza wanatupa raha na mautamu hapa chini ya jua.

-Kaveli-
 
Hutakiwi kuumiza kichwa sana mkuu,huku ni sehemu ya kuondolea stress tu baada ya miangaiko yetu, ukiona mada iko upande wako we changia tu...kwa sababu sidhani kama kuna malipo katika kuanzisha hizi nyuzi.
 
huku kuonea wivu wanawake jinsi wanavyopata attention ndo kumechangia wanaume wengi kuiga tabia za kike kama kupost video za kulamba lips, kutumia filter waonekane wazuri, kuweka pozi za kike na kuongea kikikekike.

mwanamke lazima apewe attention na wanaume na ipo hivyo miaka nenda miaka rudi, sasa kama na wewe unaona wivu na unataka tukupe attention kama tunavyowapa wanawake, tupia picha umevaa kimini.
 
Back
Top Bottom