Kwanini hatukubadili reli ya kati kiwa SGR badala ya kujenga mpya?

aka2030, tupo kwenye mchango namba 19 katika mada yako hii.

Je, katika majibu yaliyotolewa katika michango hiyo umepata majibu ya kukidhi swali lako ulilouliza?
Mimi nimejaribu kusoma kwa makini, lakini sijaona jibu hasa lililofanya reli ya zamani ising'olewe na kwenye njia hiyo ijengwe hii mpya ya SGR.

TRC huwa wanaleta habari zao humu JF mara kwa mara, ingependeza kama wangewza kusaidia kwa kutolea maelezo hasa sababu zilizofanya hali iwe kama ilivyo sasa..

Kuna baadhi ya majibu yaliyotolewa hapa yanasaidia kueleza, kama vile kuwa na "njia iliyonyooka zaidi" au "kuwa na tuta imara zaidi"; yote haya ni marekebisho yanayoweza kufanyika katika ujenzi wa reli mpya katika njia ile ile ya reli ya zamani.

Kuhusu kiasi cha mizigo inayosafirishwa kwa reli ya zamani, TRC wanaweza kutueleza kiasi cha mizigo hiyo, ambayo mimi nadhani imepungua sana. Mizigo mingi imechukuliwa na malori.

Inafahamika ushauri wa Benki ya Dunia ulikuwa ni kukarabati reli ya zamani na ndio maana mpango huo ulikuwa tayari katika hatua ya utekelezaji.
Mimi nadhani ujenzi wa SGR ya Kenya huenda ilitupa msukumo nasi tuweke yetu ya aina hiyo hiyo.

Kuna anayeweza kuwasiliana na TRC watupe jibu?

Hakika umeona ngoja niwafuate DM kwenye account yao humu jf
 
Back
Top Bottom