Kwanini hatujamsikia Jakaya Kikwete akitoa tathmini ya uchaguzi mkuu uliomazika nchini Kenya?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,483
30,155
Watanzania tulikuwa na hamu Sana ya kumsikia kiongozi wa Jopo la waangalizi wa ukanda huu wa Afrika Mashariki, Jakaya Kikwete, ambaye aliongoza Jopo hilo, kwa upande wa Afrika Mashariki, mara tu baada ya kuridi nchini, kutoka huko Kenya, akitoa tathmini ya namna uchaguzi huo ulivyoendeshwa.

Hamu hiyo iliongezeka baada ya kumsikia Jakaya Kikwete, akiwa huko nchini Kenya, akiwasihi wagombea wakuu wa uchaguzi huo, Raila Odinga wa kundi la Azimio na William Ruto wa Kenya kwanza, akiwaelekeza viongozi hao kabla ya matokeo ya uchaguzi huo kuwa, Tume ya uchaguzi wa nchi hiyo, itakapotangaza mshindi, yule ambaye hataridhika na matokeo hayo, itabidi apeleke shauri lake Mahakamani.

Nimekuwa najiuliza, hivi inakuwaje mwangalizi mkuu wa kipande huki cha Afrika Mashariki, nchi yake ya Tanzania, haitoi Haki hiyo kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

Inakuwaje kwenye Katiba ya nchi hii ibara ya 41(7) inazuia mgombea yeyote wa kiti cha u-Rais kwenda Mahakamani, kupinga Tume ya uchaguzi kwa kumtangaza, mshindi wa kiti cha u-Rais?

Je yeye Kikwete haoni kuwa Katiba yetu ina mapungufu makubwa, kwa kuweka zuio hilo, kwa wagombea wa u-Rais wa nchi hii?

Nashukuru kwa Jaji Mkuu mstaafu, Othman Chande, ambaye naye alikuwa mwangalizi wa uchaguzi huo, lakini yeye mara tu baada ya kurejea nchini, akaomgea na aaandishi wa habari, kuhusu tathmini yake kuhusu uchaguzi huo mkuu wa Kenya uliomalizika na kuisifu Sana Katiba ya nchi hiyo kwa kuweka ibara ndani ya Katiba yao kwa kupinga matokeo yanayotangazwa na Tume ya uchaguzi na akatusihi watanzania, kuwa tusiwe na hofu ya kuandika Katiba mpya ya nchi, itakayoruhusu wagombea wa kiti cha u-Rais kwenda Mahakamani, pale ambapo wayakuwa hawajaridhika na matokeo yatakayotolewa na Tume ya uchaguzi.

Kwa hivi sasa, hizi kelele za wananchi za kudai Katiba mpya, hazitaisha, hadi pale watawala wetu wa Serikali ya CCM, watakaposalimu amri na kuridhia Katiba hiyo mpya iandikwe kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na kuandika Katika Katiba hiyo mpya ya ruhusa kwa wagombea wa kiti cha u-Rais , kwenda Mahakamani, pale ambapo hawataridhika na matokeo hayo, kama yalivyotangazwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi.

Mungu ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom