Kwanini hatuitangazi Tanzania yetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini hatuitangazi Tanzania yetu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Materanus, Feb 19, 2009.

 1. M

  Materanus Member

  #1
  Feb 19, 2009
  Joined: Jan 18, 2008
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna asiye fahamu kuwa biashara katika karne hii ya utandawazi, matangazo ni lazima. Mimi huwa nashangaa kila kukicha nchi kama Angola iko kwenye CNN au BBC. Wanatangaza uwekezaji na utalii na wanatangaza kweli. Hivi karibuni Pakistani nayo haiko nyuma kwenye utangazaji, jamani hata Pakistani? CNN waliturusha hewani siyo zaidi ya mara mbili tangu JK aingie madarakani na kuahidi kuwa tutainadi nchi yetu kwa hali na mali. Kenya pamoja na matatizo yao ya kisiasa lakini hazipiti siku mbili bila kuiona kwenye vyombo vya dunia. WEBSITE YA TANZANIA INAONYESHA KUWA TANZANIA INAHITAJI UWEKEZAJI KATIKA KILIMO, VIWANDA NA UTALII SASA WAWEKEZAJE WATAJUAJE, WATALII WATAJUAJE KUHUSU BONGO? NA LA MSINGI ZAIDI, WATAJUAJE KUHUSU AMANI NA UTULILIVU TULIONAO AMBAO NDO ADVANTAGE TUNAYO WAZIDI WENZETU?
   
 2. s

  skasuku Senior Member

  #2
  Feb 19, 2009
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hela zilitengwa, zinatengwa ila hao wahusika hawana ujuzi wa marketing, na full of fisadis.

  mwaka jana kulikua na promotion kubwa ya Tanzania hapo London, wakaishia kuweka matangazo katika mabasi yaendayo waishio watu wa kima cha chini. Sasa sijui how does one justify this? Pia nasikia wameweka matangazo Airport Heathrow Terminal 3, kwa kweli wanaotumia hiyo terminal ni wageni na sio wale high spenders.

  Je ni watalii wa nchi gani wanaongoza kwenda Tanzania? kwa nini hawa wahusika wai target hizo nchi na kufanya mass marketing?

  Ila hayo matangazo ya Angola, nimeona and seriously ni well thought of. Iwe somo kwa wenzetu wa Maliasili na Utalii. We cant keep blaming JK, yeye ni human na can only do so much.
   
 3. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Naona upo mbali kweli na Tanzania, mbona ni hivi majuzi tu Tanzania ilikuwa ikitangazwa sana kwenye CNN, mpaka mabasi ya ghorofa ya London yalikuwa na matangazo ya Tanzania.

  Yote hayo matangazo katika kipindi kichache cha Jakaya, pia katuletea mkutano wa Sullivan, G. Bush, nk. Yote hayo ni katika jitihada binafsi za JK kuitangaza Tanzania.

  Kwa kifupi inachotakiwa kufanyika ni kila nyanja ibuni mbinu za kuitangaza nchi na tusingoje mpaka Rais aanze au aseme. Michezo, wanamichezo na wadau wamichezo wangejitahidi kuitangaza nchi kivyao, lakini tunaona kwenye habari kuwa wanamichezo wetu badili ya kuwa mabalozi wa kuitangaza nchi kwa mazuri yake, wao wanaenda kushikwa na madawa ya kulevya, kha!

  Kuna mengi ya kufanya, tatizo wa-Tanzania tunangoja tufanyiwe, hatufanyi wenyewe kwa kujituma, la hasha, mpaka tuburuzwe.

  Huyo Rais mmoja atafanya mangapi bila ya kuwa na raia wenye msimamo wa kujituma na sio kutumikiwa?
   
Loading...