Kwanini Hapi anakaimu nafasi ya Makonda?

Mkonongo

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
313
189
Heshima kwenu wana Jf, nikiwa naangalia taarifa ya habari ITV leo saa mbili jioni, nimemwona mkuu wa wilaya ya kinondoni Mh Ally Hapi akiwapongeza Zantel kwa kulipa deni la Ml300, hapo hapo mtangazaji akimwita "kaimu mkuu wa mkoa wa dar es salaam." Mwenye kujua atujuze sababu ya Mh Paul Makonda kukaimiwa, au yupo likizo? Natanguliza shukrani.
 
Kukaimu ni jambo la kawaida sana na sioni kwa nini liwe ishu. Mtu anaweza kufa au kuwa kikizo au mgonjwa na mtu mwingine, kwa ruhusa ya mwenye nafasi husika au mamlaka ya uteuzi, anaweza kukaimu nafasi hiyo!
Swali hapa ni sababu ya Mkuu wa mkoa kukaimiwa, hatakama angekuwa amekaimiwa na mtu yeyote, nini hasa sababu ya yeye kukaimiwa? je anaumwa?, ama yuko likizo? just curious.
 
Picha
 
Attachments

  • FB_IMG_1482948975517.jpg
    FB_IMG_1482948975517.jpg
    32.7 KB · Views: 116
Kukaimu ni jambo la kawaida sana na sioni kwa nini liwe ishu. Mtu anaweza kufa au kuwa kikizo au mgonjwa na mtu mwingine, kwa ruhusa ya mwenye nafasi husika au mamlaka ya uteuzi, anaweza kukaimu nafasi hiyo!
Kwa kawaida RC akiwa safari au likizo kuna DC mmoja wapo huwa ana kaimu nafasi hiyo. Lakini ni yule Senior zaidi ya wengine na sidhani kama Hapi ni senior kwa wengine waliopo. Mambo yanakwenda shagalabagala sasa hivi kama club ya pombe ya Wanzuki au dengerua
 
si lazma awe senior ila anayeaminika kwa boss.. hata kwako ukiondoka sio lazma majukumu umuachie mtoto mkubwa ila Yule atakayeweza kutimiza majukumu we uliwa haupo
 
Wadau samahanini.
Kwani mkuu wa mkoa si hua anakaimiwa na mkuu wa mkoa wa karibu yake au nimechanganya hii mambo??
Please msaada hapo.
 
Heshima kwenu wana Jf, nikiwa naangalia taarifa ya habari ITV leo saa mbili jioni, nimemwona mkuu wa wilaya ya kinondoni Mh Ally Hapi akiwapongeza Zantel kwa kulipa deni la Ml300, hapo hapo mtangazaji akimwita "kaimu mkuu wa mkoa wa dar es salaam." Mwenye kujua atujuze sababu ya Mh Paul Makonda kukaimiwa, au yupo likizo? Natanguliza shukrani.
Kweli Dr.Slaa aliondoka na akili zote Chadema.
 
Sijui kama ameshaanza kuhesabu miaka iliyobakia maana sijui atafanya kazi na waziri gani kwa sasa akija kuwa Rais! Amewavuruga wana ccm wote kw kiherehere!! Ikiisha miaka 10 ya huyu aliepo na yeye ajiandae kustaafu siasa maana wata dump sababu misifa yake ya kijinga!! Atafute cha kufanya.........!!!
 
Back
Top Bottom