Kwanini hamna magari ya kuzoa takataka Masaki na Oysterbay?

Riziki1981

Member
Jan 8, 2019
8
0
Tangu wiki iliyopita taka zipo mtaani alafu magari hamna. Mtendaji hapokei simu, manispaa nawao awajatoa majibu.
Jana nilipita maeneo ya masaki nikasikia wiki ya tatu hadi ya nne uchafu haujachukuliwa, kuna tatizo gani?
 
Wiki nne tu mnalalamika gari la taka halijapita kuchukua uchafu

Kuna Watanzania wenzako Hapa Hapa Mjini tangu Wakandarasi wanakutana kutengeneza Mimba mpaka Mtoto anaanza Darasa la kwanza hawajui gari la taka kupita Mtaani Kwao kuzoa uchafu!
 
Rushwa
Kampuni ya Green Waste Pro na Abilo S Peter ofisa mazingira Manisipa ya Kinondoni
Mkurugenzi?????
d40e0efb-0e0f-470b-b063-f4aa52b98756.jpg
 
Huku Salasala magari hakuna since November. Mkandarasi wetu amenieleza kwamba kuna mvutano wa kiutendaji kati ya makandarasi wazoa taka na ofisi ya Mkurugenzi. Mkandarasi anadai Mkurugenzi analazimisha malipo ya taka kutoka kwa wakaazi yasilipwe kwa mzoa taka bali yalipwe kwa ofisi ya Mkurugenzi kinyume na mkataba wao. Hali hii imepelekea wakandarasi wengi kugoma kuendelea kuzoa taka.
 
Duh kumbe inaonyesha maeneo mengi sana taka hazija zolewa
 
nimewapata barua ya wito kwenda kata kwasababu sijalipia takataka. Takataka zenyewe azijazolewa, faini inazidi ada ya mwaka ya taka. Nimeenda ofisi za serekali ya mtaa mara nne ila mtendaji Chema mara nyingi hayupo. Na siku ukimpata anakuwa tu mkali na hakusikilizi shida zako.
 
Back
Top Bottom