Kwanini "hakuna" Ufisadi Serikali ya Mapinduzi ZNZ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini "hakuna" Ufisadi Serikali ya Mapinduzi ZNZ?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MNDEE, Oct 11, 2009.

 1. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Wanajamvi inaonekana tatizo la uhujumu uchumi na ufisadi liko huku upande wa serikali ya Muungano. Kule Serikali ya mapinduzi Zanzibar sijasikia huu uozo. Fisadi au mhujumu uchumi sio lazima ahujumu mabilioni hivyo kama Zenji kuna mafisadi wa vijimilioni tungewasikia.

  Je huu usafi wa wenzetu unasababishwa na nini? Wako watakaong'aka naingiza udini, lakini angalia majina ya mafisadi utaona wakristo wanaongoza. Wako watasema nafasi nyingi za uongozi zimeshikwa na wakristo hii kusababisha kuwa na wakristo wengi mafisadi zaidi ya waislamu, kama ndivyo iweje Zenji kwenye viongozi almost wote waisilamu kusiwe na mafisadi japo wa vimilioni?
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Adhabu ya kaburi aijuwae maiti....SMZ kuna ufisadi wa kutisha,ila ukijaribu...just kujaribu tu kuuliza au kuhoji...utakiona cha mtema kuni...kama mwana CCM utaambiwa "si mwezetu", "kesha haribika siku hizi" , "anatumiwa na wapinzani" n.k
  Labda nikupe mfano ww angalia mashirika ya umma yalivyokufa Zanzibar na yaliyobaki yanavyopumua kwa mashine, ww angalia wakati wa kampeni, mamilioni ya shilingi za walipa kodi zinavyotumika kwa manufaa ya chama tawala, mbali na hayo hata taasisi za umma zinavyotumika kisiasa zaidi kwa faida ya wachache tu n.k huu ni ufisadi mkubwa...achilia mbali huo wizi wa fedha za wananchi...takribani viongozi wengi wa CCM wana utajiri wa ajabu ajabu na vitega uchumi nchi za nje kama Mauritius, Libya, Kenya..."wazee wa nyumba kubwa" wamewekeza mpaka Uingereza na Marekani...ndo maana wanakuwa mabalozi wao tu siku zote na ukisikia wamekwenda ziara za kimatibabu huko, ujuwe wananchi weshaliwa hapo. Yapo mengi mkuu...kumbuka tu serikali ya komandoo ilivyokuwa ikichota na kula kwa matonge...japo walijaribu kula na vipofu vizuri kiasi ya kuwafumba midomo yao..lakini siku zote dhamira njema haifanyi kosa kuwa si kosa...Angalia utawala wa Amani Karume...kuna wafanya biashara wa mitumba tu wanaiibia serikali...kwa jina la "nyumba kubwa" na hawaulizwi chochote, ni hivi karibuni tu, mfanya biashara mmoja maarufu zanzibar, anadaiwa kubebwa kwa "mbeleko ya chuma" na "nyumba kubwa" aliibia Benki Ya Watu Wazanzibar, mamilioni ya dola, nazungumza dola, na ilipobainika akakamwatwa na kufunguliwa mashitaka, nini kilitokea...Nellei Prosequi...kutoka kwa DPP...agizo kutoka "juu", siku chache tu baada ya kusomewa mashitaka yake...wakabakishwa masikini ya mungu wale...pengine walitia sahihi...karatasi za wizi...huu si ufisadi ni kitu...gani?
  "Yana Mwisho..." Shafi A.Shafi
   
 3. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  kule kuna ufisadi wa madaraka.raia wote wavuvi na wanakata siku na kumshukuru mungu kufanikiwa kumaliza siku bila njaa.
   
 4. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Mkuu umenifungua macho, inaonekana kukosekana kwa uhuru wa habari pale ZNZ ni tatizo. Mambo mengi yamefichwa na hakuna anayethubutu kuyaongelea hadharani. Inasikitisha kuona CCM wanauportray upinzania kama dhambi, na wanautumia huo mwanya kuficha madhambi yao.
   
 5. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,680
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Mndee
  Nimeona kama ulivyosema umeingiza kaudini kidogo hasa baada ya kuona mafisadi wengi bara ni wakristo wakati SMZ ambao ni waislam hakuna ufisadi.Mndee hapo hauko sahihi hata kidogo bali umeingiza ubaguzi ambao tumeshaonywa siku nyingi mkianza kubaguana mtaendelea kubaguana. Sasa kwa maada yako hiyo sasa ngoja tuendelee kubaguana. Mafisadi wengi ni wakristo nakubaliana na wewe lakini ni wakristo wa kutoka Kilimanjar na Arusha. Hata ukiangalia kwa makini tofauti zilizopo kwenye jamii yetu kimapato kuna wanaojiita watafutaji (wachagga) lakini ni mafisadi na majambazi wa kutupwa. Anyway nilitaka kuendeleza kuubaguzi ambako Mwl ameshatuonya tusikafanya sasa na wewe umechemka kusema eti mafisadi wengi ni wakristo huku bara
   
 6. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Mkuu inabidi tuwe na mazoea kudiscuss issues basing on facts bila kujali uko upande gani, penye ukweli tujadiliane na kutofautiana kwa amani. Nilijua italeta shida, lakini nilitaka kuona kama kule hakuna ufisadi ambao nilikuwa siiufahamu je ni nini kilikuwa kinasababisha hali hiyo. Kama ni maadili waliyokuwa nayo wenzetu au la.

  Umetoa mfano wa majambazi ni kweli huwezi kuongelea majambazi bila kutaja Moshi au Arusha, umeongezea kwa kusema wachaga ni mafisadi na majambazi wa kutupwa hapa ukweli unabaki kuwa ukweli. Kwa wale wasio na hoja watasema umeingiza ukabila. Ni sawa na mwanachama damu wa CCM kufumbia macho madhambi ya CCM kisa yeye ni mwanaccm. Hili ndilo tatizo tulilonalo tunaogopa kujadili issue tusionekane wakabila, wadini au 'sio wenzetu' au 'sio wazalendo'.
   
 7. h

  holowane Member

  #7
  Oct 13, 2009
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Junius hayo uliyoyaeleza ni kwa uchache tuu. Hebu angalia mtiririko wa watalii wanaoingia zanzibar wakati wa msimu mapato hayo yanaenda wapi? kwa utalii tuu zanzibar ingekuwa kama peponi lakini cha ajabu ni kwamba malipo yote ya gharama za hoteli na kila kitu zinalipiwa ulaya, watalii wanakuja na dola 100 tuu za kununulia madafu. Unajua kwa nini? hoteli nyingi za fukweni zinamilikiwa na WATAWALA na kwa sababu hiyo hakuna anayeweza kuhoji mapato yatokananyo na utalii maana mapato yote yanaingia mifukoni mwao. Ufisadi ni mkubwa kuliko wengi wanavyofikiria ila uhuru wa vyombo vya habari haupo,.
   
 8. L

  Lampart Senior Member

  #8
  Oct 13, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nd. Mndee,
  Mimi nakubaliana na observations zako. ZNZ hakuna ufisadi kama huu wa huku kwetu Bara. Kwa hilo tuwape hongera Wazanzibari na hata siku za Mwinyi ufisadi haukuwa kama ulivyokuwa siku za Mkapa na sasa siku za JK. Tumpeni uraisi Salim Ahmed Salim mwakani na tutaona ufisadi utakapopungua. Sisi watu wa Bara kinachotuharibia zaidi ni moja moto moja baridi - lazima tupate kila siku.
  Tukitizama sana hata sisi wana_Forum hapa JF ni mafisadi sawa na Rostam na sawa na Chenge na Lowassa at a different level. Sote tunajua kuwa hii JF inalipiwa na tunatakiwa tutoe chochote kusaidia, ni wachache tu wanaotoa na wengine tunabakia kupandia bure. Huu sio UFISADI jamani????? Kwani ufisadi maanake ni nini??? Hata ukimnyonya mwenzio nguvu zake basi wewe ni fisadi!!
  Mimi mwenyewe bado sijatoa mchango na ninajiona ni fisadi tu na ndio maana siwalaani sana hao mafisadi wenzangu wakubwa akina Rostam, lakini nipo njiani kutaka kutoa mchango wangu na mwezi huu hautokwisha.
  Sisi tusiotoa michango jamani tunakula nguvu za wenzetu? Sasa sisi na Rostam ni tafauti nini?
  Mimi nangojea nitoe mchango wangu tu na baadae nitakuwa mkali sana hapa ukumbini. Mtu ambae atakuwa anatajataja mafisadi na kama ikiwa hajatoa mchango wake basi NITAMNADIA KUWA YEYE NDIO FISADI MKUBWA.
  Kati yetu hakuna hata mmoja asiweza kumiliki angalau TSHS10,000/- lakini kwanini hatuchangii? Sababu ni kuwa deep down sisi sote ni mafisadi na sote tunazo hizo roho za ufisadi na tukipata nafasi tu basi tutakwapua kuliko huyo Rostam!!
  Hao mafisadi wakubwa wameanza hivi hivi kidogo kidogo kula nguvu za wengine na halafu wakaigeukia kuila nchi!!! Tafadhalini ndugu zanguni tusiwe MAFISADI. Tuupinge ufisadi wa aina yoyote kwa nguvu zetu zote!
   
 9. K

  Kibongoto JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2009
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Bado kauli hiii haitoshi kutushawishi kwamba wewe sio mdini. Kwanini usilinganishe Bara na visiwani tu ukaachia hapo? Ni kitu gani hasa kilichokufanya ukaenda kwenye kulinganisha wakristo na waislam ktk analysisis yako ya ufisadi? Ninashawishika kusema hoja hii ni ya kidini na huna roots za kujenga reasonable argument either kutokana na kutoelewa kwako/shule ndogo/uko ktk mazingira ambayo hayakupi nafasi ya kuona jinsi gani analytical arguments zinatengenezwa. Kipindi tupo shuleni tulikua tunawaita watu kama wewe SHALLOW!!! Achana na udini, elekeza mtazamo wako ktk kutetea taifa lako sio dini yako. Umepelekea mpaka watu kuanza kutaja makabila fulani bila sababu,hiyo ni live example ya jinsi gani mada kama hizi zinawabagua wananchi wa taifa hili. Read,learn,be informed mkuu.
   
 10. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2009
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe mkuu. Huyo Mndee atakua ana shule ya kifisadi tu. Inawezekana ana vyeti vya kununua au kasoma shule za ajabuajabu tu duniani hapa ndio maana anashindwa kabisa kujua hoja yake aijenge vipi. Tatizo humu JF hatujuani tu manake watu kama hawa wangeumbuka sana!
   
 11. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Mkuu umenena kwa mtaji huu utalii unawanufaisha wajanja wachache.
   
 12. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Waswahili wanasema debe tupu haliishi kutika, sishangai watu aina ya Kibongoto na Bao3 nao kujiita ‘wasomi’, si hata Kihiyo Temeke nae alijiitaga msomi. ‘Msomi’ Kibongoto lengo halikuwa simply kulinganisha bara na visiwani bali kujadili hoja, nimekuja na premise na assumptions ambazo wanaotaka kujadiliana watacritique kwa hoja. While we are there kuna high expectations kwa ‘msomi’ kama wewe na utumiaji wa maneno hivyo rudi kwa aliyekuandikia akupatie neno sahihi badala ya roots, pia usisahau kumwambia akufundishe kutumia spell checker.
   
 13. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Bao3 tujadiliane kwa hoja na si kwa matusi, kama unauwezo mdogo wa kuelewa issue sio lazima uijadili. Nikisoma ulichoandika sioni tofauti kati yako na ‘wasomi’ wenzio makonda wa daladala. Vipi ‘Profesa’ wako kule uwanja wa fisi alisahau kukueleza kuwa unapocritique kazi ya mtu haijalishi unaikubali au kuikataa ufanye hivyo kwa facts, tena hizo urguments zako ziwe supported.
   
 14. E

  Ex-Fisadi Member

  #14
  Oct 14, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rostam Aziz, Kighoma Malima, Yusuph Manji, Jeetu Patel,Idris Rashid,Yusuf Makamba, Kingunge Ngomable Mwiru, Msabaha, nk. just to mention few, Hawa ni wakristo? Ubaguzi wenu Waislam utawaandama subiri tu. Ndiyo maana hamtaki kuwakamata mafisadi wote, mnabakia kuwaonea Basil Mramba, Yona na Mgonja tu!! Ufisadi hauna dini na wala hauna chama. Watanzania tujifunze kuona dhambi kama ya wote na wala si kuwalinda wahalifu kwa kuwa wako kwenye chama chetu au klabu yetu!!
   
 15. Gavana

  Gavana JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2009
  Joined: Jul 19, 2008
  Messages: 17,995
  Likes Received: 1,568
  Trophy Points: 280
  zanzibar yenyewe imo kwenye ufisadi wa nyerere ilivamiwa na nyerere kwenye hayo yaitwayo mapinduzi na kubatizwa kwa jina la muungano

  kwanza wajitahidi waondoe huu ufisadi wa ubatizo wa muungano kwani lilikuwa lengo la crusader nyerere
   
 16. E

  Ex-Fisadi Member

  #16
  Oct 14, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Diverting the attention purposely?? Tusimuingize kwenye Ufisadi Mzee wetu! aliuchukia ufisadi kwa mawazo, kwa maneno na kwa matendo!! tatizo lake wale aliowaamini wamemwangusha sana!! Lakini kuna wale walio aminiwa na watu alio waamini yeye, nao wakainajisi nchi nchi yetu.
   
 17. m

  mimi-soso Senior Member

  #17
  Oct 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 151
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kifupi hawajapata bado mtu mwenye mdogo mkubwa wa kuongea
   
 18. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #18
  Oct 14, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Weka sawa kauli yako...:(
   
 19. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2015
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,683
  Likes Received: 21,946
  Trophy Points: 280
  Nimeifuma hii, hili ni swali la msingi sana kwa sasa ila umelimalizia vibaya kwa kuingiza udini maana hata huku wapo mafisadi wakubwa ambao ukiangalia majina yao utagundua kuwa hukuwa sahihi katika kutaja dini.
   
 20. coscated

  coscated JF-Expert Member

  #20
  Jun 13, 2015
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  muumini mzuri wa dini hawezi kua fisadi
   
Loading...