Kwanini hakuna Transfer of Ownership ya Simu za Mkononi?

Slim5

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
28,108
37,644
TRANSFER OF OWNERSHIP

Kuna haja ya kuwa na TRANSFER OF OWNERSHIP ya Mobile phone.

Transfer of Ownership ya gari inafanyika baada ya Mamlaka ya Mapato kumpigia SIMU mmiliki wa awali na kumuuliza km anatambua mabadiliko ya Umiliki wa gari husika na lengo ni kujirdhisha!

Kwa nini Makampuni ya Simu hayajiridhishi juu ya mabadiliko ya umiliki wa simu pale inapotokea simu ilokuwa inatumiwa na Mtu X siku zote mpk Ijumaa jioni, ghafla Jumamosi Asubuhi au Mchana inatumiwa na mtu Z na huku yule Mmiliki wa awali Mtu X anaonekana ktk simu ameRENEW sim card!

Kuna wakati Makampuni ya simu yanaona wazi kuwa Mmiliki wa Simu A alikuwa anatumia simu kwa miaka akiwa SINZA lkn overnight simu ile inapewa sim cards mpya tena inaanza kusomeka ipo Tanga au Moro na sio Sinza, Dsm.

Kuna watu wanamiliki simu ghaĺi kiasi zina thamani sawa ama zaidi ya gari. Iweje magari yana TRANSFER of OWNERSHIP lkn sio simu?

Inawezekana simu ya Maxence Melo ikawa ya bei ndogo mf 180k lkn unyeti wa simu yake ktk saa za kazi unaifanya simu yake kufika mpk 10m hususani ukihusisha athari endapo simu yake ikapotea ama kuibiwa. Je hakuna haja ya TRANSFER OF OWNERSHIP kwa simu?

Mtu kama Mkuu Mshana jr upo uwezekano simu yake ina maFILE kama yote ya Kanuni mbali mbali za Ulimwengu wa giza ambazo disclose yake ni kosa kubwa sana na pengine kwa usiri wa info hizo ni chanzo cha mapato!

Sasa mtu km Mshana jr anapotezaje simu yake afu kampuni ya simu inaruhusu TRANSFER of OWNERSHIP pasi na kumshikirisha! Hapa pana shida!

Transfer of OWNERSHIP ya simu inaweza ikapunguza matukio ya wizi wa simu!

Tufikirie!
 
Na inawezekana kabisa, na pia wanajua kabisa simu inapobadilisha SIM cards, ni ufuatiliaji tuu.
 
No. Sio lazima kwenda Mamlaka husika. PTER mf Voda wanaona simu yk inawekwa simcards mpya, wanafanya kukupigia ama kukuTEXT tu! Hii ni sehemu ya Customer care. Mbona wanatuma sms kama zote za promo why wasitume SMS kukuuliza kama unatambua simu yk kwa sasa inatumika Nachingwea?
Simu na utakapotaka kuuza utaenda kwenye mamlaka husika kufanya transfer.

Lazima mlolongo huo utaambatana na tozo vipi utaziweza ?
 
No. Sio lazima kwenda Mamlaka husika. PTER mf Voda wanaona simu yk inawekwa simcards mpya, wanafanya kukupigia ama kukuTEXT tu! Hii ni sehemu ya Customer care. Mbona wanatuma sms km zote za promo why wasitume SMS kukuuliza km unatambua simu yk kwa sasa inatumika Nachingwea?
Kitu pekee ambacho vodacom kinatengeneza mahusiano na wewe ni hiyo Simcard wala hawana mpango na hiyo simu yako.

Hivyo kubadili laini na kuweka nyingine walah hawaisumbui chochote it is your personal property.

Hii process za transfer lazima ziwe chini ya mamlaka itakayohusika na utambuzi wa simu na siyo service providers kama vodacom au Airtel.

Kingine utawaongezea operating costs hivyo utalazimika kulipia hiyo huduma ya transfer.
 
Back
Top Bottom