Somo letu: Wajua kwanini namba 13 ni namba ya mkosi? Je, umezaliwa tarehe 13?

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,635
29,967
Mara Nyingine number 13 watu huichukulia kama namba ya mkosi ,

Lakini tunajiuliza sana kwanini watu huchukulia namba 13 kama namba ya mkosi, yanayosemwa yana maana kubwa sana ndio maana leo hii katika
1.Hotel kubwa za kimataifa ukiangalia vyumba vyote kwa namba ukifika namba 12 wanairuka namba 13 wanaandika chumba kifuatacho namba 14, nimefanya research hii kwa muda mrefu sana na kwa umakini zaidi, nimegundua hotel kubwa tena zinazoheshimika kimataifa hawana chumba namba 13.

2. Kwenda ndege, hakuna siti namba 13 ukifika kumi na mbili wanaruka kwenda 14, ni ndege kubwa sana zaidi ya bomberdier, namaanisha kwa wale mnaosafiri Mara kwa Mara chunguza kwenye ndege kubwa kama Emirates, Fly Dubai, Etihad, KLM, Qatar airways, British airways na nyinginezo hawana namba 13, bali wana 12 na 14, tu

3. Ijumaa ambayo tarehe yake ni 13 huwa ni siku ambayo watu wengi hawapangi mipango yao kabisa kufanya biashara au safari usitisha mpaka siku inayofuata,

4. Waliozaliwa tarehe 13 Mara nyingi huwa inakuwa ngumu kutoka kimaisha mpaka watumie nguvu kubwa sana kuweza kufika malengo yao, na saa nyingine hukusanya mtaji na kuibiwa, huchikiwa, usingiziwa kila Mara na huonekana hawana maana ndani ya jamii, inahitajika nguvu ya ziada kuyakwepa

KWANINI HASA NAMBA 13 HUSEMEKANA NI NAMBA YA MKOSI?? NA ILIANZAJE

Kwanza watu wanaoendekeza kuogopa namba 13 wana kitu kinaitwa triskaidekaphobia yaan waoga wa namba 13

Namba au mkosi wa namba 13 uhusishwa na ukristo kwa maana kwamba namba 13 katika biblia ina maana yake,
1. Mlo wa mwisho wa yesu alikuwa na wanafunzi wake 12 lakin yule wa 13 ambaye hakuwepo ni Yuda aliyemsaliti , kwahiyo inaonekana usaliti wa huyo mtu wa 13 ulipelekea Yesu kuteseka mno,,

2.Katika wathesalonike inaonesha kwamba ishara ya shetani imejitokeza Mara 13

3.Ilithibitika kwamba kuna tabia au sifa 13 za watu wafuasi wa Shetani soma warumi (1:28-32)

3.Siku ya 13 ya mwezi wa kwanza Haman alisaini makubaliano ya kuwa wayaudi wanapaswa kuuwawa siku ya 13 ya mwezi wa 12 (Esther 3:7 - 9).

4.Kuanguswa na kusurubiwa kwa yeriko ilitiwa muhuri na namba 13

5.Mfalme Suleiman alitumia miaka 7 akijenga mnara wa Yerusalemu, lakin cha kushangaza alitumia miaka 13 kwa tabu kujenga nyumbani kwake

(1wafalme 6:38). Na (1wafalme 7:1)!

6.Kuna njaa 13 zilitajwa kwenye biblia
(Mwanzo 12:10, 26:1, 41:54; Ruthu 1:1; 2Samuel 21:1; 1wafalme 18:1; 2wafalme 4:38, 7:4, 25:3; Nehemiah 5:3; yeremia 14:1; Luke 15:14 na matendo ya mitume 11:28.

7.Ishmael, mtoto wa kwanza wa Abraham (kwa Hagar), alitahiriwa(kuondoa uchafu kuwa mwana wa mungu kamili) akiwa na miaka 13 (mwanzo 17:25)

NAMBA 13 NI YA KUANGALIA KWA MAKINI

Britannica
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom