Kwanini hakuna chuma ulete katika Mabenki?

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,395
Habari wanaJF,

Kwasisi wafanyabiashara tumewahi kukumbana na kitu kinaitwa CHUMA ULETE, nimebahatika kuwa na kijiofisi cha M-Pesa mitaa ya Mbagala hapa basi huyu Mwanadada niliyemuweka hapo aliniambia kiasi cha 450K zimepotea na yeye hajui imekuaje lakini mteja wa mwisho alikuwa ni Mama wa makamo aliyekuja kuomba chenji. Iliniwia vigumu kumuamini.

Sasa jana nimekutana na mtu analalamika kuwa ameibiwa fedha kwa miujiza akiwa katika duka lake na yeye akasema ni CHUMA ULETE.

Najiuliza kwanini hakuna malalamiko kwenye taasisi za kifedha kuwa wanafanyiwa uchawi huu?

Nini siri iliyonyuma na taasisi hizi?

CC: mshana jr, Mtu mzito, jichawi, Zurie
 
Bank kuna siri nyingi ambazo hizijui kwa macho ya nyama ila jua huyo chuma ulete hawezi kuiba
 
Sheria ya uganga na uchawi ni marufuku kuchukua pesa bank au kuingia kumuwangia mtu ukakuta pesa mezani au popote huwezi chukua. Ukichukua hutoki ndomana wanga watakuchezea watakavyo ila pesa yako asubuhi utaikuta pembeni ya kitanda
 
Mkuu kwa habari za mtaani chuma ulete ni uchawi wa kuchukua pesa...
 
Mkuu kwa habari za mtaani chuma ulete ni uchawi wa kuchukua pesa...
Ni kweli ila kuchukua bank sheria za uchawi zinagoma.
Zaid unatumika kweny kurudishiana chench au hawa ombaomba unampa pesa ndo unapoteza hivyo
 
Sheria ya uganga na uchawi ni marufuku kuchukua pesa bank au kuingia kumuwangia mtu ukakuta pesa mezani au popote huwezi chukua. Ukichukua hutoki ndomana wanga watakuchezea watakavyo ila pesa yako asubuhi utaikuta pembeni ya kitanda
wewe hujui, wajanja wanaiba na ni matajiri wakubwa mpaka dola majini yanakuibia!
 
Watanzania wengi wana imani za uchawi ambao hawawezi kuuthibitisha wala kuuelezea.
 
unaish wap??? zunguka huku mikoani uone matajiri washirikina aisee
tofautisha MSHIRIKINA NA MCHAWI MKUU..
MSHIRIKINA YEYE ANAVIABUDU VITU VINGINE ambavyo havina sifa ya UMUNGU KWA MASLAHI YAKE flani..
na MCHAWI NIYULE ANAEROGA WATU NAKUWATUPIA MAJINI ..MARADHI .anapaa na ungo e.t.c
 
unaish wap??? zunguka huku mikoani uone matajiri washirikina aisee
Hao sio wachawi. Bali wanatumia nguvu za Giza kupata Mali.
Umeanza kwenda kwa waganga ukubwani. Utajiita mchawi?
kuwa mchawi sio mchezo
 
Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom